Bunge la Chama kimoja tutegemee tena G55 mpya ikitokea?

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,269
Tanzania ina uzoefu wa kuwa na Bunge la chama kimoja, lkn pamoja na kuwa na bunge la chama kimoja kulikuwa na mijadala mikali na hoja nzito zilizojadiliwa ukiwamo ule wa kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika uliotokea kwenye miaka ya 1990 al maarufu kama G55.

Wabunge wa CCM wa wakati huo kina, Njelu Kasaka, Jenerali Ulimwengu, Philip Marmo na wengine, walikuwa ni watu waliojiamini waliojengwa kwenye chama na ambao walikuwa tayari hata kufukuzwa ndani ya chama.

Tofauti ya mabunge hayo ya nyuma na linalotarajiwa kuwa Bunge la sasa ni historia ya watakaounda kundi hilo.

Kwenye bunge la awamu iliyopita ukiwaondoa wabunge wa upinzani, kazi kubwa ya wabunge wa CCM ilikuwa ni kuitetea serikali, matusi ya akina Lusinde yalielekezwa kwa wapinzani, Spika alimalizia hasira zake kwa kuwafukuza wapinzani.

Kwenye bunge la awamu hii Serikali itakuwa inajitetea yenyewe, spika atakuwa anawafokea wanaCCM wenzake wabunge wa CCM watakuwa wanaihoji Serikali na kwa kufanya hivyo lazima kutatokea kupishana kati ya utawala na wabunge na kati ya serikali na baadhi ya wabunge wa CCM, baadhi yao wataonekana kama wasaliti wanaofanya kazi ya upinzani, na hapo ndipo tunaweza kupata kundi lingine kama la G55 ndani ya bunge la chama kimoja.

Wakati wa G55 zisingekuwa busara za Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kukemea CCM ingepasuka vipande viwili, safari hii bahati mbaya hatuna kiongozi wa kalba ya Nyerere, ukitokea mgawanyiko ndani ya Bunge la chama kimoja sioni mtu sahihi au kiongozi anayeweza kuwaunganisha pasipo kuwaumiza.

====

Zaidi, soma: Kundi la G55 walioidai Tanganyika mwaka 1993...
 
Tegemea bunge bubu, bunge zaidi ya kibogoyo..Bunge litakalokuwa linabariki kila kitu toka Serikali.

Ati nani aruhusu kuhoji mamlaka? Kwanza ajiulize mara mbili ..maana kura za maoni kasaidiwa, kura za uchaguzi mkuu kasaidiwa..afu ati alete fyokofyoko?? hiiìii!!
 
Nakuheshimu sana mkuu Quinine. IVI MKUU HUJUI KUWA TANZANIA HAINA BUNGE???

BUNGE lililokuwapo CAG aliliita DHAIFU.

Tanzania ina majengo ya Bunge na CCM ndio inafanyia MIKUTANO YA SELIKALI kwenye majengo ya bunge.

Mbunge mzima anasupport zito kuuwawa. ILO NI BUNGE AMA VIKAO VYA WJINGA.
 
Mimi mtazamo wangu tutaanza kuona rangi za CCM safari hii maana tayari ubunge washapata na huyu Jiwe yupo term ya mwisho nina amini hataogopwa na kupambwa kama mwanzo utakuja kuona.
 
Ni 'Upuuzi' uliopitiliza na 'usiovumilika' wa kutaka 'Kufananisha' yaliyotokea miaka ya 90 ukataka 'Kuilazimisha' iweze kutokea pia miaka hii ya 2020.

Mtani unashangaa hayo ya mwaka 90, wakati sasa hivi tunajivunia kuhamia Dodoma wazo la mwaka 73, enzi barua zinapelekwa kwa njia ya posta na kuchukua ziada ya siku 3 kufika?
 
Hayo sahau zama hizi... Zamani walau hata uzalendo kwa Taifa ulikuwepo, ila kwa sasa ni chama kwanza na tumbo lishibe..
 
....kwa wabunge gani asee hawa akina babu tale
Tusitegemee lolote kwa hiki bunge kibogoyo, sana sana tarajia Magufuli kuongezewa muda wa kukaa madarakani. Enzi za G55 wabunge hao waliingia bungeni kwa kura za wananchi, sio hawa waliongia bungeni kwa kubaka uchaguz
Tanzania ina uzoefu wa kuwa na Bunge la chama kimoja, lkn pamoja na kuwa na bunge la chama kimoja kulikuwa na mijadala mikali na hoja nzito zilizojadiliwa ukiwamo ule wa kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika uliotokea kwenye miaka ya 1990 al maarufu kama G55.

Wabunge wa CCM wa wakati huo kina, Njelu Kasaka, Jenerali Ulimwengu, Philip Marmo na wengine, walikuwa ni watu waliojiamini waliojengwa kwenye chama na ambao walikuwa tayari hata kufukuzwa ndani ya chama.

Tofauti ya mabunge hayo ya nyuma na linalotarajiwa kuwa Bunge la sasa ni historia ya watakaounda kundi hilo.

Kwenye bunge la awamu iliyopita ukiwaondoa wabunge wa upinzani, kazi kubwa ya wabunge wa CCM ilikuwa ni kuitetea serikali, matusi ya akina Lusinde yalielekezwa kwa wapinzani, Spika alimalizia hasira zake kwa kuwafukuza wapinzani.

Kwenye bunge la awamu hii serikali itakuwa inajitetea yenyewe, spika atakuwa anawafokea wanaCCM wenzake wabunge wa CCM watakuwa wanaihoji serikali na kwa kufanya hivyo lazima kutatokea kupishana kati ya utawala na wabunge na kati ya serikali na baadhi ya wabunge wa CCM, baadhi yao wataonekana kama wasaliti wanaofanya kazi ya upinzani, na hapo ndipo tunaweza kupata kundi lingine kama la G55 ndani ya bunge la chama kimoja.

Wakati wa G55 zisingekuwa busara za Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kukemea CCM ingepasuka vipande viwili, safari hii bahati mbaya hatuna kiongozi wa kalba ya Nyerere, ukitokea mgawanyiko ndani ya bunge la chama kimoja sioni mtu sahihi au kiongozi anayeweza kuwaunganisha pasipo kuwaumiza.
 
Tusitegemee lolote kwa hiki bunge kibogoyo, sana sana tarajia Magufuli kuongezewa muda wa kukaa madarakani. Enzi za G55 wabunge hao waliingia bungeni kwa kura za wananchi, sio hawa waliongia bungeni kwa kubaka uchaguz
Nasikitika Jana ilikuwa bahati mbaya kwangu nikaangalia UTV walikuwa na kipindi wanamuhoji mjinga mmoja sijui anaitwa nani ukweli moyo wangu uliumia sana...kuona mtu anaedhaniwa ameelika anaongea ujinga
 
Natoa pendekezo, wabunge wote walioshinda majimbo yaliyokuwa na wabunge wa upinzani, ndiyo wawe wapinzani (yaani hao ndiyo waunde kambi ya upinzani).

Hahahaha, kwa sisiyemu Hilo linawezekana
 
Back
Top Bottom