Bunge kufuta madeni ya shilingi 12 Bilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bunge kufuta madeni ya shilingi 12 Bilioni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mpaka Kieleweke, Aug 27, 2008.

 1. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kesho Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania linatazamiwa kufuta madeni yenye dhamani ya shilingi 12 Bilioni , hii ni kutokana na vile visingizio kuwa madeni haya hayalipiki, mara wadaiwa wamekufa n.k.

  Kama Nchi hii masikini inaweza kupoteza fedha nyngi kiasi hicho huku Rais wake akienda Marekani kupokea msaada wa Dola 20 elfu, hii ni fedheha kwa watanzania.

  Nitajitahidi kuwabandikia madeni hayo na hao wanaotazamiwa kusamehewa.
   
 2. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #2
  Aug 27, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  hata wale wa epa nao watasamehewa ??
   
 3. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2008
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Jambo hili litafanyika wakati wa kinachoitwa Appropriation Bill, na hii inatia uchungu sana kuona kuwa watu ambao wana makampuni makubwa tuu eti wanasamehewa madeni tena na Bunge .....
   
 4. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Sasa naona hawasikii la mwazini wala mnadi sala. Jamani sasa naona tuache hadi tuone mwisho wao nch itapouzwa na kila mtu achukue chake akaishi huko ughaibuni wanapokimbizia fedha zao. Au mnasemaje jamani. Kusamehe! Sijawahi kusikia kama serikali inasamehe. Nchi nyingine deni hulipwa na ndugu yaani next of kin kwetu si mabandidu? Hatuwezi kujumlisha na kutoa? Oh my GOD? Itafika siku turudie utawala wetu wa kijadi ambapo mtu akikosea huadhibiwa hapo hapo na kama hasara kulipwa na ndugu na ukoo wake ili kuleta discipline. KWELI!
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Huu ni utaratibu wa kawaida wa ki-hasibu!!! acheni kuleta bumba humu!!! uliza wahasibu watawaambia...
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Aug 29, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  kwa hiyo mahela yaliyolazimishiwa ktk fungu la upotevu yanasamehewa pia?
  kuzunguzungu
   
 7. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #7
  Aug 29, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Sheria siku zote huvunjwa kwa kufuata taratibu na urasimu wa serikali.
  Tumefanya kazi serikalini na ndani ya mashirika ya umma, ni kweli wako wazalendo wengi tu lakini kuna manunda kibao walindwao kwa kila hila ili mambo ya kipuuzi kama haya kwa ufisadi.

  Juzi amekuja Bush tumekenua kuchekele msaada wa Billion 6. Leo tunajifanya matajiri sana na wahasibu wa kukata kwa mundu kufuta madeni ya Billion 12!
   
 8. M

  Masatu JF-Expert Member

  #8
  Aug 29, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Nadhani la msingi ni kujua hao bad debtors wamekuwa written off kwa misingi ipi? otherwise kama alivyoeleza Mh hapo juu huu ni utaratibu wa kawaida wa kihasibu na upo hivyo kwa misingi ya kihasibu sio utajiri wa taifa au umaskini wake
   
 9. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Maelezo mazuri sema tu umechemsha!

  Huu ni utaratibu wa kawaida wa kusafisha vitabu vya serikali, kwa mfano... serikali inamdai Kasheshe ... sh. Bil. 3... lakini mazingira yanaonyesha Kasheshe hadi kufa hataweza lipa hiyo fedha au Kasheshe already amekufa...

  Kinachofuata ni Serikali inapeleka bungeni tena kupitia kwenye kamati ya bunge kusema Sh. Bil. 3 anazodaiwa kasheshe haziwezi patikana hivyo tunaomba tufute hili deni. (bad dept).. period. sasa Kamati ya Bunge au Bunge linaangalia kama bado kuna uwezekano, mfano wa kuchimba kaburi ya Kasheshe ili alipi serikali wanaambiwa kachimbeni kaburi lake na alipe... kama haiwezekani bunge linakupali deni kufutwa...

  Ni matumaini yangu mumuelewa what it mean.
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Aug 30, 2008
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,734
  Likes Received: 4,958
  Trophy Points: 280
  Kasheshe,Masatu,Madela,

  ..labda wangeeleza wanaohusika na hayo madeni.

  ..wakati mwingine ni yale mashirika na taasisi za umma zilizoshindwa kujiendesha.
   
 11. M

  Masatu JF-Expert Member

  #11
  Aug 30, 2008
  Joined: Jan 29, 2007
  Messages: 3,285
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Joka,

  Ndio maana nikasema la msingi hapa ni kujua/kujadili kilichopelekea madeni hayo kufutwa. Lakini kama kawaida yetu tunadandia gari kwa mbele na kuanza kukandia tu, no substance whatsoever
   
 12. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Labda ni Quote kutoka kwa hotuba ya Mh. Waziri Mkuu wakati akifunga Bunge; Ndio hii mijamaa itaelewa... maana siku hizi yule asiyejua ndiye anaonekana na kujigamba anayejua.

  "Katika Mkutano huu wa Bunge Lako Tukufu pia lilipitisha Azimio la Bunge la Kuridhia Kufuta na Kusamehe Madai ya Kodi pamoja na Riba na Hasara itokanayo na upotevu wa Fedha na Vifaa vya Serikali na Maduhuli yaliyoshindikana kukusanywa kwa kipindi kinachoanzia Mwaka wa Fedha 1990/1991 hadi Tarehe 30 Juni 2007"

  Sasa endeleeni kubwabwanya kama kawaida yenu. Ninyi ndio mnao jua wao hawajui.
   
 13. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Nakubali nimechemka lakini na wewe kubali kwamba ni kuni zinazoteketea mekoni.

  Huyo kasheshe kabla hajakopa ni lazima mkopo wake uwe backed up na asset fulani. Huwezi kuamka asubuhi na kumpa mtu 1Billion hivi hivi tu.
  Endapo mtu hana asset basi ni lazima adhaminiwe na mtu mwenye asset za kuaminika.
  Kuchimba kaburi la Kasheshe ili kuidai fedha maiti ya kasheshe si ununda ni matokeo ya ununda, ununda wenyewe ni kumkopesha mtu kifisadi kwa sababu tu tunajua siku moja bunge litaingilia kati.
   
 14. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  MADELA WA- MADILU,

  Kwi kwi kwi

  Huo ulikuwa mfano mmoja tu kati ya mifano mingi!

  Mfano mrahisi mwingine unaolezea utaratibu wa namna hiyo ni mfano... wizi wa fedha au kifaa cha serikali ... baada ya kukosa mwizi au mwizi kukamatwa akafungwa lakini hakurudisha fedha... ile fedha itakuwa kwenye vitabu mpaka mtakapo amua kuifuta kwa taratibu kama hizo zilizofanyika.

  Kwa taarifa yako... siku hizi ndio imepungua hata kufika bil. 12 kwa sababu ya good finance governance ya serikali na CAG, nadhani kama sio mwaka jana au mwaka juzi ilikuwa zaidi ya Bil. 50.

  Umeelewa nadhani twende mbele mkuu..
   
Loading...