Bundi wavamia mkutano wa CCM!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bundi wavamia mkutano wa CCM!!!!

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Nyakipambo, Oct 1, 2012.

 1. N

  Nyakipambo JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 435
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, bundi wawili juzi walivamia mkutano wa uchaguzi wa viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani hapa na nusura waangukie meza waliyokuwa wameketi Mbunge wa Kahama Mjini, James Lembeli na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja.

  Kuingia kwa bundi hao katika uchaguzi uliokuwa unasubiri kwa hamu na wakazi wa Kahama kwenye Ukumbi wa Shule ya Msingi Rocken mjini hapa kuliibua hofu kubwa kwa wagombea, kiasi cha baadhi ya wanaCCM kugeuza tukio hilo kuwa ajenda kwa muda."Ni ajabu kwa bundi kuingia katika ukumbi wa mkutano, hawakuogopa kelele za watu cha ajabu ni kutaka kuangukia meza za viongozi. Ni tukio la kustaajabisha sana," alisema Damas Joseph, Diwani wa Kata ya Chambo wilayani Kahama.

  Aliongeza kuwa, kama tukio hilo lina aina yoyote ya nguvu za giza, linapaswa kukemewa kwa nguvu zote kichama, kwa kuwa viongozi wa kweli wanapaswa kuchaguliwa bila `kuchezea' akili za wajumbe ambao ni wapigakura.

  MwanaCCM mwingine, Deo Ndilima kutoka Kata ya Ukune, alikiri kufadhaishwa na tukio hilo, huku akielezea hofu ya kutopatikana kwa viongozi wasio na sifa kukiongoza chama, hasa endapo bundi hao wanahusishwa na masuala ya ushirikina.

  Ukiondoa tukio hilo, wajumbe wengi walisifu hali ya utulivu iliyokuwa inaendelea katika uchaguzi huo.

  http://habarileo.co.tz/index.php/habari-za-kitaifa/4556-bundi-wavamia-mkutano-wa-ccm


   
 2. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Bundi ni ndege kama walivyo mwewe, kunguru, tai, njiwa n.k., tofauti ni kuwa yeye hujitafutia riziki usiku kutokana na macho yake kuathiriwa na mwanga mkali wa jua! Sasa kuna ajabu gani hapo! Huenda kuna kiota chake jirani!

  Acheni ushirikina!
   
 3. v

  valid statement JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Bundi wanaonekanaga kama alama ya mkosi!Sijui kwanini!
   
 4. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,320
  Likes Received: 2,299
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka mbunge wa Sumve Richard Ndasa akihojiwa na BBC miaka kadhaa iliyopita alisema yeye bundi alikosakosa kumgonga akiwa amekaa meza kuu.......kilichomsaidia ni kuwa alimkwepa!
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,328
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  Bundi arudi kwao Chama cha Manyang'au mchana kweupeee
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  teh kwa kuwa katokea shinyanga sina ubishi KUNA UNANILIU HAPO ULIKUA UNATENDEKA............
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Hizi siasa za Tanzania mbona kazi ipo!!
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mwl wangu wa english wa o level frm 3 alikuwa mama wa wa ki irish, huko kwao ireland bundi akitua home kwako ni sign ya good omen bahati kwao, wao kunguru ndo anashirikishwa na hayo mambo ya ulozi. Bongo bundi ht km ni ndege wa kawaida akilia hapo nje kesho watu wanahamia kwa fundi
   
 9. M

  Mercyless JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 652
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Chama cha wakulima na wafanyakazi hicho.
   
 10. Philipo Kidwanga

  Philipo Kidwanga Verified User

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Jul 12, 2012
  Messages: 2,063
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  yaani chama kikikaribia kufa kumbe ni kama kukata roho kwa ngamia,tutaona mengi sana miaka hii.
   
 11. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,746
  Likes Received: 12,827
  Trophy Points: 280
  Huyu sio bundi ni mbwembwe za uchaguzi
   
Loading...