Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 14,939
- 20,400
Tunahitaji ufafanuzi. Maana blackmail upande nwingine unaweza kutafsirika kwamba Magufuli kamwambia faili lako ninalo na naweza kukufanyia mbaya, bora uwe mdogo kabla sijakutumia TAKUKURU wakuchunguze upya.
Kwa serikali kuwa na makabrasha ya Lowasa au TAKUKURU, hilo ni jambo la kawaida.
Ila kama Edward Hosea alishindwa kulifanyia kazi mafaili hayo wakti ule, basi huu ni wakati wake.
Na kama kuna vizuizi kwa TAKUKURU kwanini mzee mwenyewe asiitwe akajieleza, au akaomba kumuona raisi mwenyewe (kwa mujibu wa mkuu G Sam) ?
Edward Lowasa ni mtu mzito sana kwenye nchi hii lakini hawezi kuishinda serikali na kinachofanyika sasa ni damage limitation.
Na hiyo hatuwezi kuita ni blackmail kwani inakuwa inaingia kwenye ramsom kwamba unahitaji malipo ya fedha ili kupata kitu fulani.
Sasa raisi hawei kufanya blackmail.
Hapo tena tunakuwa tunapoteza maana ya mjadala.