Bundi CHADEMA na Wakati wa Malipo - Lowassa Huyu Huyu?

Bundi CHADEMA na Wakati wa Malipo - Lowassa Huyu Huyu?

Ngoja nikuulize swali, hivi unaamini kabisa Mbowe hakujua chochote kuhusu uamuzi wa Lowasa kwenda Ikulu? Jaribu kuunganisha matukio, Raisi alikwenda kumjulia hali Mzee Kingunge na Mzee Kingunge akatamka yake siku iliyofwata Lowasa na Mbowe wakaonekana kwa Mzee Kingunge, leo hii Lowasa katia timu Ikulu, je unaamini kabisa Mbowe hakufahamu hili hadi aje akane kwamba siyo msimamo wa Chama?

Binafsi naamini kabisa kilichomkimbiza Lowasa chadema ni tabia mbaya na ujeuri wa Tundu Lisu, hasa kitendo chake cha kuisema nchi yetu na Raisi wetu tena nchi ya kigeni na vyombo vya habari vya kigeni ni kitendo cha kifedhuri na dharau dhidi ya Raisi wetu na nchi yetu, na kuna Watanzania wengi sana kama vile Lowasa ambao wamechukizwa sana na kitendo kile hata wale ambao walikuwa wanamhurumia Tundu Lisu!

Na amini msiamini anayeiua chadema ni siyo Mbowe bali ni Tundu Lisu, hili nililiamini siku zote na limetimia, Tundu Lisu siyo intelligent man na ndiyo maana anaingiza jazba kwenye Siasa bila yakutambua kwamba huwezi kuanzisha Vita dhidi ya Raisi wa JMTZ na ukashinda, siyo kwa mfumo wetu huu, hivyo na bado muda utaongea wengi watamgeuka Tundu Lisu na atabakia mwenyewe labda na baadhi ya watu facebook!

Tundu Lisu ni kibaraka wa wazungu na watanzania wazalendo wa nchi hii tutaendela kuamini hivyo.
 
Kwanza nimesema wanachama wenzangu nimemtaja Nzi na wewe halafu nukasema na wengine, hivyo naomba hapo unielewe.

Pili, Lowasa amekwenda Ikulu kukiri kwamba kweli raisi John Magufuli anachapa kazi na yale anayoyafanya yanaonekana na apengine hata yeye (Lowasa) ameanza kuathirika na utekelezaji wa sera zake.

Mwisho, raisi Magufuli amemsifia Lowasa kwa kufanya siasa za kistaarabu.

Sasa niambie hili tukio la leo la Edward Lowasa kwenda kumtembelea raisi John Magufuli Ikulu, hata kama ni lake binafsi bwana Lowasa, lakini linamaanisha nini khasa?
Wapi wewe mimi ndiyo naelewa Lowassa kaenda ikulu kufanya nini na ana nia gani! Hivi unajua kuwa aliomba appointment karibia miezi miwili Magufuli akawa anamkatalia? Niombe nikuelezee anachokipigania Lowassa! Acha hizo porojo nyingine. Magufuli kwenye urais is useless!
 
What was that appointment for, tour of state house?
 
Kwanza mkuu mimi siyo nzi.

Pili naomba niungane na Mbowe kwamba Lowassa kaenda ikulu kwa issues zake binafsi. Ila unaanzaje kumueleza rais wa kiafrika matatizo yako bila kisifia kidogo? Hivi Lowassa kaongea mambo mangapi? Kaongea dakika ngapi? Kasema reli, umeme wa striglers na elimu bure? Mimi ningepata shida sana kama angesema Magfuli ametengeneza ajira kila sekta ila kasema ukitengeneza reli unaajiri vibarua hilo nalo tujadili? Kasifia kuhusu demokrasia? Emb acheni. Tatizo ni watu wanakuuuza eti Lowassa amesifia?Wapi?Vingapi? Mbona hamsemi na Magufuli kamsifia Lowassa?
Mkuu G Sam
Kuna member humu anaitwa Nzi
 
nachokumbuka ulitukanwa sana na makamanda humu kuhusu lowassa, hakuna tusi ambalo hujatukanwa humu! ngoja tuone lowassa akiondoka kama watakuomba msamaha
Hakuna atakayekuwa na ujasiri wa kuomba msamaha; wengi wataamua kuhamaisha matusi yao kwa Lowassa akiondoka kesho; watasema hakuwa mpinzani wa kweli, watamuita kila jina baya.. wale wale ambao walijitoa ufahamu sasa hivi watajifanya wameshukiwa na Roho Mtukutu!
 
1.jpg
(Picha na Ikulu)

Katika jambo ambalo limetafsiriwa na baadhi ya watu kama kuuchanganya upinzani leo Waziri Mkuu wa zamani Bw. Edward Lowassa amekutana na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar-es-Salaam kwa mazungumzo. Kufuatia mazungumzo hayo Lowassa alizungumza na waandishi wa habari na alimmwagia sifa Rais Magufuli na serikali yake kwa kazi nzuri inayofanywa. Maelezo yake hayakuelezea kama katika mazungumzo na Rais Magufuli kama Lowassa alizungumzia masuala ya haki za kiraia, masuala ya usalama na masuala mbalimbali ya kidemokrasia ambayo chama chake kimekuwa kikizungumzia sana siku za karibuni.

Kutokana na hilo baadhi ya viongozi wa Chadema na hata wanachama wa kawaida wameanza mara moja kumshangaa Lowassa kwa uamuzi wake wa kukutana na Magufuli na kummwagia sifa kama alivyofanya. Miongoni mwa viongozi walioonesha mwitikio wa kutofurahishwa na jambo hilo ni Mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbless Lema. Lema akiandika katika ukurasa wake wa Twitter alisema hivi “Mh Lowassa umeikosea Tanzania kwa kauli baada ya kutoka Ikulu. Mema yapi umeyaona katika Serikali hii? Wakati Mbunge Lissu bado anauguza majeraha ya risasi, maiti zinaokotwa, Uchumi unaanguka, Benki zinafungwa, Demokrasia imekufa Bungeni/Nje ya Bunge na Sioi mkwe wako bado yuko Magereza”

Mwenyekiti wa CHADEMA naye Bw. Freeman Mbowe ambaye alifanya juhudi kubwa kumleta Lowassa ndani ya Chadema na hatimaye kutengeneza njia ya kumfanya kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015 ameonesha kushangazwa na kauli hiyo ya Lowassa. Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Ujerumani (DW Idhaa ya Kiswahili) Bw. Mbowe amesema kuwa kauli za Lowassa Ikulu ni zake binafsi na hazikuwa zinawakilisha msimamo wa chama.

Wakati huo huo baada ya mkutano wake na Magufuli jioni hii taarifa zimekuja zinazoelezea kuwa Mzee Lowassa anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari kesho katika hoteli ya Serena. Haijajulikana anataka kuzungumzia nini hasa lakini kwa kuangalia wimbo wa kuhama Chadema unaoendelea sasa hivi na jinsi alivyogeuka na kuisifia Serikali ya Magufuli na kuacha kutetea misimamo ya Chadema wala ajenda zake hadharani hapo jana, ni wazi kuna uwezekano wa Lowassa kuamua kufanya mambo makubwa mawili.

Kuna uwezekano wa yeye kutangaza kustaafu siasa rasmi na hivyo kuamua kujivua nafasi zote za uongozi katika Chadema. Anaweza kufanya hivyo ili kutoa nafasi kwa wanasiasa vijana na wengine kuendelea kuijenga Chadema kuelekea chaguzi za 2019 na zile za 2020. Jambo jingine analoweza kulifanya atakapozungumza na waandishi wa habari ni kutangaza kukirudia chama chake cha awali cha CCM ambacho alichokulia na kukitumia kwa muda mrefu na ambacho kilimpa nafasi mbalimbali za juu uongozi nchini.

Endapo Lowassa ataamua kufanya hilo la kwanza ni wazi hilo la pili halitokuwa mbali; lakini kama ataamua kufanya hilo la pili ni wazi kuwa Lowassa atakuwa ameona kuwa hawezi kuendelea na siasa za upinzani kwani gharama ya kuwa upinzani ni kubwa sana na hakuwa tayari kuendelea kuilipa.

Kwa baadhi yetu ambao tumekuwa tunafuatilia siasa za upinzani hasa kufuatia Chadema kujivuruga kwa kumkumbatia Lowassa na kumtupa Dkt. Slaa kwa kejeli na dharau namna ile kuna somo ambalo viongozi wa Chadema watapaswa kuulizwa. Ni matumaini yetu endapo lolote litatokea kufuatia Lowassa kuamua ama kustaafu siasa au kujiondoa Chadema, wanachama na mashabiki wa Chadema watakasirishwa na uongozi wao na kutaka viongozi wote wa juu kuwajibika kwa kukivuruga chama.

Wakati umefika kwa wanachama wa kweli na wapinzani wa kweli ndani ya Chadema kuoneshwa kukasirishwa na uongozi wa chama cha kuanza kuoneshwa kukasirishwa na kutaka watu wawajibike kuanzia Mwenyekiti na Kamati Kuu nzima. Wasipoonesha hasira zao kwa viongozi wao na badala yake wakiendelea kumlalamikia Magufuli kwa kuvugura upinzani wataendelea kuwa kama mbuni aliyeficha kichwa chake mchangani na kama wale ambao wanazungumzia matatizo yote yaliyokuwemo ndani isipokuwa yule tembo aliyesimama pembeni!

Ni wakati wa malipo. Na alipo wataendelea kuwepo?

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

hakuna mwanachama yeyote wa chadema ambaye anaweza kukasirishwa na uongozi wa mbowe

ni kama wote ni kama mbwa wa kufugwa ambao they will never bark to their masters

hawa wanachama hawa! wanaosifia kila kitu..aisee
 
Huyu lowasa katuia mnyika wetu ni muda wa kukisafisha chama leo kanikera japo huwez kupinga kila kitu
 
Hakuna atakayekuwa na ujasiri wa kuomba msamaha; wengi wataamua kuhamaisha matusi yao kwa Lowassa akiondoka kesho; watasema hakuwa mpinzani wa kweli, watamuita kila jina baya.. wale wale ambao walijitoa ufahamu sasa hivi watajifanya wameshukiwa na Roho Mtukutu!

Hakuna atakayehamisha matusi kwa Lowassa .Labda mpumbavu tu.Huwezi kumtukana mtu anayerudi nyumbani.Sikuwahi kumuamini Lowassa na sitokaa nimuamini LOWASSA.kwangu mimi hata kesho naona anachelewa ni bora aende hata leo
 
Mkuu Mwanakijiji,

Mimi nimekuwa siku zote nikiwaambia baadhi ya wana JF hapa kwamba Edward Lowasa hakwenda Chadema kwa nia ya kufanya upinzani bali kwa nia ya kukiangamiza.

Wale wakuu wote kama Nzi, G Sam na co waje hapa kuekezea kuhusu hli la leo la Edward Lowasa kwenda Ikulu kumsalimia raisi John Magufuli na kukiri kwamba nchi sasa imenyooka.

Je, nini maana ya hiki kitendo?

..hapo unamuonea EL.

..yeye alikwenda CDM kwa nia ya kupata Uraisi wa Tz kupitia chama hicho.

..hakwenda CDM kwa nia ya kuangamiza chama.

..lakini hata ukimuangalia EL hana haiba ya ukamanda-kamanda ambayo mhusika anahitaji kuwa nayo ili kuendana na safu ya watu walioko CDM.

..Baada ya uchaguzi kuisha CDM na EL no longer had anything in common. Kwa hiyo ilikuwa ni suala la muda tu kila upande kumuacha mwenzake.

..EL needs to move on into his retirement and concentrate on taking care of his health.

..Na CDM nao waendelee na utaratibu wa KUJISAILI na KUJIPANGA UPYA baada ya kushindwa 2015.

..Pande zote zinatakiwa kuonyesha USTAARABU na UVUMILIVU wakati wa zoezi la kufikisha tamati mashirikiano yao.
 
Nitarudi kukupa details.. Ila kuna sehemu nimesoma unamuita Lissu kibaraka. Nitakupa somo hadi akili ibadilike. Narudi soon!

Mkuu, huwezi kunibadilisha msimamo wangu.

Sanasana mtaanza kutukana na kutoa maneno ya kashfa.

Lakini ukweli upo palepale.
 
..hapo unamuonea EL.

..yeye alikwenda CDM kwa nia ya kupata Uraisi wa Tz kupitia chama hicho.

..hakwenda CDM kwa nia ya kuangamiza chama.

..lakini hata ukimuangalia EL hana haiba ya ukamanda-kamanda ambayo mhusika anahitaji kuwa nayo ili kuendana na safu ya watu walioko CDM.

..Baada ya uchaguzi kuisha CDM na EL no longer had anything in common. Kwa hiyo ilikuwa ni suala la muda tu kila upande kumuacha mwenzake.

..EL needs to move on into his retirement and concentrate on taking care of his health.

..Na CDM nao waendelee na utaratibu wa KUJISAILI na KUJIPANGA UPYA baada ya kushindwa 2015.

..Pande zote zinatakiwa kuonyesha USTAARABU na UVUMILIVU wakati wa zoezi la kufikisha tamati mashirikiano yao.

Umeongea jambo la msingi sana.

Over to you G Sam.
 
Kuna mwanajamii forum alisema magufuli unaweza kumsema vibaya vyovyote ukiwa mbali ila ukibahatika kukutana naye utajikuta unapata upako wa kumkubali na kunsifia kama alivyofanya lowassa Leo.
 
Ngoja nikuulize swali, hivi unaamini kabisa Mbowe hakujua chochote kuhusu uamuzi wa Lowasa kwenda Ikulu? Jaribu kuunganisha matukio, Raisi alikwenda kumjulia hali Mzee Kingunge na Mzee Kingunge akatamka yake siku iliyofwata Lowasa na Mbowe wakaonekana kwa Mzee Kingunge, leo hii Lowasa katia timu Ikulu, je unaamini kabisa Mbowe hakufahamu hili hadi aje akane kwamba siyo msimamo wa Chama?

Binafsi naamini kabisa kilichomkimbiza Lowasa chadema ni tabia mbaya na ujeuri wa Tundu Lisu, hasa kitendo chake cha kuisema nchi yetu na Raisi wetu tena nchi ya kigeni na vyombo vya habari vya kigeni ni kitendo cha kifedhuri na dharau dhidi ya Raisi wetu na nchi yetu, na kuna Watanzania wengi sana kama vile Lowasa ambao wamechukizwa sana na kitendo kile hata wale ambao walikuwa wanamhurumia Tundu Lisu!

Na amini msiamini anayeiua chadema ni siyo Mbowe bali ni Tundu Lisu, hili nililiamini siku zote na limetimia, Tundu Lisu siyo intelligent man na ndiyo maana anaingiza jazba kwenye Siasa bila yakutambua kwamba huwezi kuanzisha Vita dhidi ya Raisi wa JMTZ na ukashinda, siyo kwa mfumo wetu huu, hivyo na bado muda utaongea wengi watamgeuka Tundu Lisu na atabakia mwenyewe labda na baadhi ya watu facebook!
Ulichokiongea ni ukweli mtupu lisu jazba zake ndo tatizo hasa japo ni msomi mzuri mjenga hoja vizuri ila uwasilishaji wake ndo umekaa kijeurijeuri
 
Mzee Mwanakijiji

Kitambo niliwaonya CHADEMA kwamba tabia yao ya kuchukua watu wa CCM na kuwapa nafasi za kugombea katika chaguzi, kuanzia ubunge mpaka urais, bila hata kupikwa na kuchunguzwa katika chama, zitawatokea puani.

Huo ulikuwa ni wakati wanamchukua Shibuda. Shibuda akawapa tabu sana kama nilivyotabiri.

Sasa, haijulikani Lowassa atasema nini licha ya wengi kubashiri anaweza kurudi CCM. Inawezekana harudi kabisa, anarudi kidogo tu katika kujipanga kufanya kazi kidiplomasia zaidi na rais Magufuli huku akiwa CHADEMA. Inawezekana anarudi kabisa CCM.

Lakini kwa vyovyote vile, kuna mtafaruku ndani ya CHADEMA kutokana na mwenendo huu. Lowassa anawasumbua CHADEMA wanaotaka kumpinga Magufuli bila kusitasita.

Hata katika kanisa, mtu hajiungi na kanisa siku moja, na kupewa nafasi ya kuwa Papa siku ya pili.

Inabidi apitie mfumo wa kanisa, kupata kipaimara, kuwekwa wakfu, kufikia mpaka u kardinali kanisani, halafu ndiyo anapewa nafasi ya kuwa Papa.

CHADEMA uroho wao wa kutaka watu wenye majina makubwa wanaoweza kushinda chaguzi bila kuangalia muendano kiitikadi na kupikwa katika chama utawatokea puani.
 
Back
Top Bottom