Bundi CHADEMA na Wakati wa Malipo - Lowassa Huyu Huyu?

Bundi CHADEMA na Wakati wa Malipo - Lowassa Huyu Huyu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
34,253
Reaction score
44,595
1.jpg
(Picha na Ikulu)

Katika jambo ambalo limetafsiriwa na baadhi ya watu kama kuuchanganya upinzani leo Waziri Mkuu wa zamani Bw. Edward Lowassa amekutana na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar-es-Salaam kwa mazungumzo. Kufuatia mazungumzo hayo Lowassa alizungumza na waandishi wa habari na alimmwagia sifa Rais Magufuli na serikali yake kwa kazi nzuri inayofanywa. Maelezo yake hayakuelezea kama katika mazungumzo na Rais Magufuli kama Lowassa alizungumzia masuala ya haki za kiraia, masuala ya usalama na masuala mbalimbali ya kidemokrasia ambayo chama chake kimekuwa kikizungumzia sana siku za karibuni.

Kutokana na hilo baadhi ya viongozi wa Chadema na hata wanachama wa kawaida wameanza mara moja kumshangaa Lowassa kwa uamuzi wake wa kukutana na Magufuli na kummwagia sifa kama alivyofanya. Miongoni mwa viongozi walioonesha mwitikio wa kutofurahishwa na jambo hilo ni Mbunge wa Arusha Mjini Bw. Godbless Lema. Lema akiandika katika ukurasa wake wa Twitter alisema hivi “Mh Lowassa umeikosea Tanzania kwa kauli baada ya kutoka Ikulu. Mema yapi umeyaona katika Serikali hii? Wakati Mbunge Lissu bado anauguza majeraha ya risasi, maiti zinaokotwa, Uchumi unaanguka, Benki zinafungwa, Demokrasia imekufa Bungeni/Nje ya Bunge na Sioi mkwe wako bado yuko Magereza”

Mwenyekiti wa CHADEMA naye Bw. Freeman Mbowe ambaye alifanya juhudi kubwa kumleta Lowassa ndani ya Chadema na hatimaye kutengeneza njia ya kumfanya kuwa mgombea wa Urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka 2015 ameonesha kushangazwa na kauli hiyo ya Lowassa. Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Ujerumani (DW Idhaa ya Kiswahili) Bw. Mbowe amesema kuwa kauli za Lowassa Ikulu ni zake binafsi na hazikuwa zinawakilisha msimamo wa chama.

Wakati huo huo baada ya mkutano wake na Magufuli jioni hii taarifa zimekuja zinazoelezea kuwa Mzee Lowassa anatarajiwa kuzungumza na vyombo vya habari kesho katika hoteli ya Serena. Haijajulikana anataka kuzungumzia nini hasa lakini kwa kuangalia wimbo wa kuhama Chadema unaoendelea sasa hivi na jinsi alivyogeuka na kuisifia Serikali ya Magufuli na kuacha kutetea misimamo ya Chadema wala ajenda zake hadharani hapo jana, ni wazi kuna uwezekano wa Lowassa kuamua kufanya mambo makubwa mawili.

Kuna uwezekano wa yeye kutangaza kustaafu siasa rasmi na hivyo kuamua kujivua nafasi zote za uongozi katika Chadema. Anaweza kufanya hivyo ili kutoa nafasi kwa wanasiasa vijana na wengine kuendelea kuijenga Chadema kuelekea chaguzi za 2019 na zile za 2020. Jambo jingine analoweza kulifanya atakapozungumza na waandishi wa habari ni kutangaza kukirudia chama chake cha awali cha CCM ambacho alichokulia na kukitumia kwa muda mrefu na ambacho kilimpa nafasi mbalimbali za juu uongozi nchini.

Endapo Lowassa ataamua kufanya hilo la kwanza ni wazi hilo la pili halitokuwa mbali; lakini kama ataamua kufanya hilo la pili ni wazi kuwa Lowassa atakuwa ameona kuwa hawezi kuendelea na siasa za upinzani kwani gharama ya kuwa upinzani ni kubwa sana na hakuwa tayari kuendelea kuilipa.

Kwa baadhi yetu ambao tumekuwa tunafuatilia siasa za upinzani hasa kufuatia Chadema kujivuruga kwa kumkumbatia Lowassa na kumtupa Dkt. Slaa kwa kejeli na dharau namna ile kuna somo ambalo viongozi wa Chadema watapaswa kuulizwa. Ni matumaini yetu endapo lolote litatokea kufuatia Lowassa kuamua ama kustaafu siasa au kujiondoa Chadema, wanachama na mashabiki wa Chadema watakasirishwa na uongozi wao na kutaka viongozi wote wa juu kuwajibika kwa kukivuruga chama.

Wakati umefika kwa wanachama wa kweli na wapinzani wa kweli ndani ya Chadema kuoneshwa kukasirishwa na uongozi wa chama cha kuanza kuoneshwa kukasirishwa na kutaka watu wawajibike kuanzia Mwenyekiti na Kamati Kuu nzima. Wasipoonesha hasira zao kwa viongozi wao na badala yake wakiendelea kumlalamikia Magufuli kwa kuvugura upinzani wataendelea kuwa kama mbuni aliyeficha kichwa chake mchangani na kama wale ambao wanazungumzia matatizo yote yaliyokuwemo ndani isipokuwa yule tembo aliyesimama pembeni!

Ni wakati wa malipo. Na alipo wataendelea kuwepo?

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
 
Mkuu Mwanakijiji,

Mimi nimekuwa siku zote nikiwaambia baadhi ya wana JF hapa kwamba Edward Lowasa hakwenda Chadema kwa nia ya kufanya upinzani bali kwa nia ya kukiangamiza.

Wale wakuu wote kama Nzi, G Sam na co waje hapa kuekezea kuhusu hli la leo la Edward Lowasa kwenda Ikulu kumsalimia raisi John Magufuli na kukiri kwamba nchi sasa imenyooka.

Je, nini maana ya hiki kitendo?
 
Umetoka pangoni kwa raha leo ..lini na wewe unatangaza nia kujiunga na ccm ?

Siasa ni upumbavu fulani hivi wachache sana ndio wanasimamia wanacho kiamini

Viva Tundu Lisu na wachache wengine kama wewe bila kumsahau Mbowe na ngozi ngumu yake pamoja na mikiki yote
 
Ngoja nikuulize swali, hivi unaamini kabisa Mbowe hakujua chochote kuhusu uamuzi wa Lowasa kwenda Ikulu? Jaribu kuunganisha matukio, Raisi alikwenda kumjulia hali Mzee Kingunge na Mzee Kingunge akatamka yake siku iliyofwata Lowasa na Mbowe wakaonekana kwa Mzee Kingunge, leo hii Lowasa katia timu Ikulu, je unaamini kabisa Mbowe hakufahamu hili hadi aje akane kwamba siyo msimamo wa Chama?

Binafsi naamini kabisa kilichomkimbiza Lowasa chadema ni tabia mbaya na ujeuri wa Tundu Lisu, hasa kitendo chake cha kuisema nchi yetu na Raisi wetu tena nchi ya kigeni na vyombo vya habari vya kigeni ni kitendo cha kifedhuri na dharau dhidi ya Raisi wetu na nchi yetu, na kuna Watanzania wengi sana kama vile Lowasa ambao wamechukizwa sana na kitendo kile hata wale ambao walikuwa wanamhurumia Tundu Lisu!

Na amini msiamini anayeiua chadema ni siyo Mbowe bali ni Tundu Lisu, hili nililiamini siku zote na limetimia, Tundu Lisu siyo intelligent man na ndiyo maana anaingiza jazba kwenye Siasa bila yakutambua kwamba huwezi kuanzisha Vita dhidi ya Raisi wa JMTZ na ukashinda, siyo kwa mfumo wetu huu, hivyo na bado muda utaongea wengi watamgeuka Tundu Lisu na atabakia mwenyewe labda na baadhi ya watu facebook!
 
Mkuu Mwanakijiji,

Mimi nimekuwa siku zote nikiwaambia baadhi ya wana JF hapa kwamba Edward Lowasa hakwenda Chadema kwa nia ya kufanya upinzani bali kwa nia ya kukiangamiza.

Wale wakuu wote kama Nzi, G Sam na co waje hapa kuekezea kuhusu hli la leo la Edward Lowasa kwenda Ikulu kumsalimia raisi John Magufuli na kukiri kwamba nchi sasa imenyooka.

Je, nini maana ya hiki kitendo?
Kwanza mkuu mimi siyo nzi.

Pili naomba niungane na Mbowe kwamba Lowassa kaenda ikulu kwa issues zake binafsi. Ila unaanzaje kumueleza rais wa kiafrika matatizo yako bila kisifia kidogo? Hivi Lowassa kaongea mambo mangapi? Kaongea dakika ngapi? Kasema reli, umeme wa striglers na elimu bure? Mimi ningepata shida sana kama angesema Magfuli ametengeneza ajira kila sekta ila kasema ukitengeneza reli unaajiri vibarua hilo nalo tujadili? Kasifia kuhusu demokrasia? Emb acheni. Tatizo ni watu wanakuuuza eti Lowassa amesifia?Wapi?Vingapi? Mbona hamsemi na Magufuli kamsifia Lowassa?
 
Mwanakijiji mzee wa kufunga siku 40 ili tupate wapiga risasi kwenye miili ya watu, naamini una furaha sana baada ya Lissu kupigwa risasi

Funga siku Mia ili na sisi wengine tupigwe pia
 
Umeshau kuwa kwenda kwake Ikulu pia huenda ilikuwa ni mbinu muhimu ya kisiasa kwake kuendelea kuwateka wafuasi wake waliopo CCM...
 
Matumizi sahihi ya akili humfanya mwanadamu aondokane na utumwa wa hisia na kufanya maamuzi sahihi

Watu wenye kutumia akili zao vyema walijua kuwa Lowasa si mpinzani wa Kweli na hajawahi kuwa mpinzani wa kweli....hili lilikuwa ni jambo jepesi sana kuling’amua kama ukijiweka kando na mihemko......

Daima Mungu hajawahi kumficha mnafiki.....
 
Ngoja nikuulize swali, hivi unaamini kabisa Mbowe hakujua chochote kuhusu uamuzi wa Lowasa kwenda Ikulu? Jaribu kuunganisha matukio, Raisi alikwenda kumjulia hali Mzee Kingunge na Mzee Kingunge akatamka yake siku iliyofwata Lowasa na Mbowe wakaonekana kwa Mzee Kingunge, leo hii Lowasa katia timu Ikulu, je unaamini kabisa Mbowe hakufahamu hili hadi aje akane kwamba siyo msimamo wa Chama?

Binafsi naamini kabisa kilichomkimbiza Lowasa chadema ni tabia mbaya na ujeuri wa Tundu Lisu, hasa kitendo chake cha kuisema nchi yetu na Raisi wetu tena nchi ya kigeni na vyombo vya habari vya kigeni ni kitendo cha kifedhuri na dharau dhidi ya Raisi wetu na nchi yetu, na kuna Watanzania wengi sana kama vile Lowasa ambao wamechukizwa sana na kitendo kile hata wale ambao walikuwa wanamhurumia Tundu Lisu!

Na amini msiamini anayeiua chadema ni siyo Mbowe bali ni Tundu Lisu, hili nililiamini siku zote na limetimia, Tundu Lisu siyo intelligent man na ndiyo maana anaingiza jazba kwenye Siasa bila yakutambua kwamba huwezi kuanzisha Vita dhidi ya Raisi wa JMTZ na ukashinda, siyo kwa mfumo wetu huu, hivyo na bado muda utaongea wengi watamgeuka Tundu Lisu na atabakia mwenyewe labda na baadhi ya watu facebook!
nani wa kumgeuka shujaa LISSU,labda sampuli yako tu!
 
Kwanza mkuu mimi siyo nzi.

Pili naomba niungane na Mbowe kwamba Lowassa kaenda ikulu kwa issues zake binafsi. Ila unaanzaje kumueleza rais wa kiafrika matatizo yako bila kisifia kidogo? Hivi Lowassa kaongea mambo mangapi? Kaongea dakika ngapi? Kasema reli, umeme wa striglers na elimu bure? Mimi ningepata shida sana kama angesema Magfuli ametengeneza ajira kila sekta ila kasema ukitengeneza reli unaajiri vibarua hilo nalo tujadili? Kasifia kuhusu demokrasia? Emb acheni. Tatizo ni watu wanakuuuza eti Lowassa amesifia?Wapi?Vingapi? Mbona hamsemi na Magufuli kamsifia Lowassa?

Kwanza nimesema wanachama wenzangu nimemtaja Nzi na wewe halafu nikasema na wengine, hivyo naomba hapo unielewe.

Pili, Lowasa amekwenda Ikulu kukiri kwamba kweli raisi John Magufuli anachapa kazi na yale anayoyafanya yanaonekana na pengine hata yeye (Lowasa) ameanza kuathirika na utekelezaji wa sera zake.

Mwisho, raisi Magufuli amemsifia Lowasa kwa kufanya siasa za kistaarabu.

Sasa niambie hili tukio la leo la Edward Lowasa kwenda kumtembelea raisi John Magufuli Ikulu, hata kama ni lake binafsi bwana Lowasa, lakini linamaanisha nini khasa?
 
Back
Top Bottom