Bulembo amejuaje mambo ya Hazina!?.Wewe mtoa hii mada unajua utaratibu wa Hazina kuwa na pesa?
Ngoja tusaidiane hapa kuondoa ujinga:
Kwa ufupi mmoja wa anayejua kuhusu pesa za Hazina na mwenye mamlaka ya kuzisemea ni kamishna wa bajeti wa wizara ya fedha.
Hazina ni wasimamizi wa mfuko mkuu wa serikali na akaunti yao ipo banki kuu. Banki kuu kila siku inapokea pesa kutoka TRA...maana wote tunajua kuwa TRA inafanya makusanyo ya kila siku.
Kutoka TRA pesa zinaingizwa Banki kuu kila siku. Na zikifikishwa Banki kuu, kila siku zinatoka kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya serikali. Utaratibu wa miaka yote huu.
Je, hoja kuwa Hazina ina pesa pungufu au kidogo imetoka wapi!? Je makusanyo yamepungua huko TRA? Au mlidhani pesa za serikali uwa zinatunzwa tu!?
Hoja za kujiuliza:
Kama Hazina haina kitu...mishahara ya mwezi huu tumelipwaje?
Kama Hazina haina kitu...bodi ya mikopo imepata wapi pesa ya kulipa wanafunzi wa elimu ya juu wa kuanzia mwaka wa 1 hadi wa 5 kwa vyuo vyote nchini?
Kama Hazina haina pesa...shughuli za serikazi zinajiendeshaje?
Ukijiuliza hayo maswali...utapata picha kuwa pesa zipo na zinaendelea kukusanywa kila siku, ila serikali ya awamu ya 5 imeamua kubana matumizi na kuongeza makusanyo zaidi ili ahadi za rais Dkt Magufuli zitekelezwe kwa wakatiikiwemo ya elimu BURE...tayari mashule yamepigwa MARUFUKU kukusanya michango ya aina yoyote kutoka kwa wanafunzi.
#HapaKaziTu