Bukoba vs Moshi

Bukoba vs Moshi

Status
Not open for further replies.
Hapo tz tulikuwa tumeshapata uhuru?
Naam unaionaje stand inavyovutia? Hadi Leo Kuna wilayan Hakuna stand kama hii ya Moshi ya 1971 mfano bukoba
Cheki picha hapo chini ni stand ya bukoba ya leo
tapatalk_1548810355073.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tembea ht vijiji vya moshi.
Rombo
Kilema
Mwika
Marangu
Tarakea
Machame
Boma
Sanya
Sadala
Hizo vijiji huwezi fananisha na bukoba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Miaka ya 60 na 70 yalikuwepo mabasi makubwa aina ya Layland CD yakienda kwenye maeneo tajwa hapo na cha ajabu mengi yalikuwa yanamilikiwa na Umoja wa Akina Mama. Mfano ni UWT Kilema walikuwa na Layland iliyokuwa inatoka Kilema kwenda Moshi mjini kila siku.

Mwaka 1978 wakati wa vita basi hili lilichukuliwa na jeshi kupeleka askari Bukoba. Moshi ilirudi nyuma sana baada ya Uhuru.
 
*👆Malisa ampinga Polepole kwa fact*


Huyu dogo ameanza kuchanganyikiwa. Moshi ilianza kuendelea zamani za pontio pilato kabla ya ujio wa Dr.Livingstone na Gavana Edward Twining.

Mwaka 1902 barabara zinazounganisha mitaa mbalimbali ya Moshi zilikuwa na lami, enzi hizo CCM haijazaliwa, mama yake TANU wala bibi yake TAA.

Mwaka 1895 Ikulu ya kwanza ya kisasa ya Mangi mkuu wa wachagga ilijengwa eneo la KDC Moshi. Ikulu hiyo hadi sasa ndiyo inayotumika kama Ikulu ndogo ya Rais akija mkoani Kilimanjaro.

Mwaka 1917 dola ya wachagga ilikuwa na mfumo rasmi wa serikali na baraza la mawaziri, ikiwa ni pamoja na ofisi na magari kwa watendaji waandamizi wakiwemo mawaziri. Ofisi za mawaziri ndio zinatumika leo kama ofisi za halmashauri ya wilaya ya Moshi.

Miaka 100 iliyopita Moshi kulikuwa na viwanda mbalimbali kikiwemo kiwanda kikubwa zaidi cha kubangua kahawa eneo la Afrika Mashariki. Mwaka 1940 dola ya wachagga tayari ilikuwa na gazeti lake (Komkya), lililokuwa likisomwa maeneo yote ya wachagga kuanzia Siha hadi Rongai. Gazeti hilo liliandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
-
Kufikia mwaka 1950 karibu kila kata au tarafa ilikuwa na shule ya sekondari, zahanati au kituo cha afya pamoja na kanisa la kisasa, kuanzia Siha mpaka Tarakea. Sio zote lakini nyingi zilikuwa na shule zilizojengwa na wamisionari miaka mingi sana iliyopita.

Wakati chakubanga na babu yake wanatembea kilomita 50 kwenda kuchoma chanjo ya tetekuwanga, wazee wa kichagga walikua wakipata huduma za afya kwenye vituo vya afya vya mission vilivyopo kwenye kata/tarafa zao.

Leo mtu mmoja pengine kwa sababu ya kukosa chanjo ya pepopunda anaropoka kwamba maendeleo ya Moshi yameletwa na CCM? What a shame.!!
-
Kimsingi CCM na serikali yake zimezorotesha maradufu maendeleo ya Moshi kuliko wakati mwingine wowote katika historia. Moshi ya wakati ule (kama dola yenye mamlaka kamili), na Moshi ya leo (kama wilaya) ni vitu viwili tofauti. Moshi ingeachwa kuwa dola huru kama ilivyokuwa zamani, ingekuwa na maendeleo maradufu kuliko leo.

Halafu kama kweli CCM inaleta maendeleo, mbona kuna mikoa haijawahi kuchagua upinzani na bado haina maendeleo? Kwanini maendeleo hayo CCM isipeleke kwenye ngome zake? Next time mwambieni kabla hajabwatuka ajifunze historia kdg.!!!!!!!!!

Source instagram:Malisa_gj
 
Wakuu ili kudhibitisha mkoa wa Kilimanjaro ni ngome ya maendeleo tangu enzi na enzi,ninaomba kuwasilisha picha ya kituo Cha mabasi Moshi ya mwaka 1971
*NB* wale Wala senene waliokuwa wanafananisha Moshi na mji wao wajitafakari
Cc
instanbul
britanicca
Come27
Sky EclatView attachment 1011553

Sent using Jamii Forums mobile app
Exactly yaani hii ndiyo moshi kielelezo cha kwanza ni ile keria ya Leyland ilikuwa inaitwa mombasa rahaaa miaka ile jamani maisha ya zamani yalikuwa babukubwaa kinoma, kielelezo kingine ni theluji ya mlimani ilikuwa kibao tofauti na sasa hivi wanadai mambo ya tabia nchi ukipanda mlima hushuki hata na kibakuli ya barafu. yaani hiyo miaka ukiangalia hiyo manzari utafikiria ni asubuhi kumbe saa kumi na moja ya jioni wazee walitunza mazingira big up my young broda luambo makiadi kwa hisani ya maktaba yako.

Sent from my SM-E500H using JamiiForums mobile app
 
Miaka ya 60 na 70 yalikuwepo mabasi makubwa aina ya Layland CD yakienda kwenye maeneo tajwa hapo na cha ajabu mengi yalikuwa yanamilikiwa na Umoja wa Akina Mama. Mfano ni UWT Kilema walikuwa na Layland iliyokuwa inatoka Kilema kwenda Moshi mjini kila siku.

Mwaka 1978 wakati wa vita basi hili lilichukuliwa na jeshi kupeleka askari Bukoba. Moshi ilirudi nyuma sana baada ya Uhuru.
@instanbul imesikia história hiyo?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom