Bukoba: Mwalimu atakiwa kurejesha Mshahara aliolipwa kwa kufanya Udanganyifu kwa Mwajiri

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Novemba 22, 2023 katika Mahakama ya Bukoba imeamriwa kesi ya Jamhuri dhidi LYDIA KOKUSHOBOKA KAOO, ambaye ni alikuwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kashai- Manispaa ya Bukoba.

Imemtia hatiani kwa makosa mawili la kwanza matumizi ya nyaraka kumdanganya mwajiri kwa kuandika barua kwa mwajiri kujifanya hajamaliza masomo ya shahada ya kwanza ndani ya muda aliopewa na mwajiri wake ili aweze kuendelea na shahada ya pili.

Kosa la pili ni kuisababishia Serikali hasara kwa kuendelea kulipwa mishahara kwa kipindi cha udanganyifu asichokuwepo kazini.

Mshtakiwa ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 3 or fine ya 1 milioni kwa kosa la kwanza. Na kifungo cha miaka 3 bila fine kwa kosa la pili.

Pia imeamuliwa jumla ya sh. 22,252,134.73/= iliyopokelewa kama mishahara azirudishe kwa mwajiri wake.
 
Yaani hata digrii ya kwanza hakuwa nayo anaonyesha kufoji halafu kaomba ruksa akasome digrii ya Pili kumbe anaenda kulala nyumbani

Aweza kuwa form four failure huyo.sawa.ba wale waliofoji wakalipwa na serikali eti walitumikia taifa na kufoji mivyeti kwao

Serikali ikaamua kuwalipa
Mbona yule baba mlezi alithibitisha kuwa siye na aliendelea na kazi na sasa yupo kazini.
 
Yaani hata digrii ya kwanza hakuwa nayo anaonyesha kufoji halafu kaomba ruksa akasome digrii ya Pili kumbe anaenda kulala nyumbani

Aweza kuwa form four failure huyo.sawa.ba wale waliofoji wakalipwa na serikali eti walitumikia taifa na kufoji mivyeti kwao

Serikali ikaamua kuwalipa
Hawa ndio waliokuwa wakitetewa na chadema kipindi JPM akiwawajibisha
 
Yaani hata digrii ya kwanza hakuwa nayo anaonyesha kufoji halafu kaomba ruksa akasome digrii ya Pili kumbe anaenda kulala nyumbani

Aweza kuwa form four failure huyo.sawa.ba wale waliofoji wakalipwa na serikali eti walitumikia taifa na kufoji mivyeti kwao

Serikali ikaamua kuwalipa
Alimaliza digriiiiiii, akapata gepu la ada ndipo akaunganisha mastaz. Akaomba ruhusa Kwa kudanganya.

Itakuwa mmoja kati ya Hawa waliomba kupiga mti akawachomoa ndipo wakakinukisha DED , Deo, hr. Dso na dao
 
Novemba 22, 2023 katika Mahakama ya Bukoba imeamriwa kesi ya Jamhuri dhidi LYDIA KOKUSHOBOKA KAOO, ambaye ni alikuwa mwalimu wa Shule ya Msingi Kashai- Manispaa ya Bukoba.

Imemtia hatiani kwa makosa mawili la kwanza matumizi ya nyaraka kumdanganya mwajiri kwa kuandika barua kwa mwajiri kujifanya hajamaliza masomo ya shahada ya kwanza ndani ya muda aliopewa na mwajiri wake ili aweze kuendelea na shahada ya pili.

Kosa la pili ni kuisababishia Serikali hasara kwa kuendelea kulipwa mishahara kwa kipindi cha udanganyifu asichokuwepo kazini.

Mshtakiwa ametiwa hatiani na kupewa adhabu ya kifungo cha miaka 3 or fine ya 1 milioni kwa kosa la kwanza. Na kifungo cha miaka 3 bila fine kwa kosa la pili.

Pia imeamuliwa jumla ya sh. 22,252,134.73/= iliyopokelewa kama mishahara azirudishe kwa mwajiri wake.
Wanaoiba mabilioni mbona hamuwapeleki mahakamani
 
Yaani hata digrii ya kwanza hakuwa nayo anaonyesha kufoji halafu kaomba ruksa akasome digrii ya Pili kumbe anaenda kulala nyumbani

Aweza kuwa form four failure huyo.sawa.ba wale waliofoji wakalipwa na serikali eti walitumikia taifa na kufoji mivyeti kwao

Serikali ikaamua kuwalipa
Jifunze kusoma vizuri mkuu. Huyu mtumishi aliomba ruhusa akasome shahada ya kwanza,,baada ya kumaliza hyo shahada ya kwanza alitamani aendelee na shahada ya pili lakini ruhusa akawa hana maana ruhusa ambayo alipewa ni ya kusoma shahada ya kwanza ilikuwa imeisha.

Hivyo akalazimika kufanya udanganyifu wa kumuandikia muajiri wake barua kuwa hajamaliza shahada ya kwanza kwa sababu kadhaa(alifoji sababu) hivyo anaomba apewe ruhusa aweze kumalizia..malengo yake ni kwamba hyo ruhusa angepewa angeenda kusoma Shahada ya pili.

Umeelewa?
 
Yaani hata digrii ya kwanza hakuwa nayo anaonyesha kufoji halafu kaomba ruksa akasome digrii ya Pili kumbe anaenda kulala nyumbani

Aweza kuwa form four failure huyo.sawa.ba wale waliofoji wakalipwa na serikali eti walitumikia taifa na kufoji mivyeti kwao

Serikali ikaamua kuwalipa
Maelezo yanaonesha, alikuwa na ruhusa ya kusoma shahada.

Lakini alipomaliza shahada, akaandika kwa mwajiri kuwa hajamaliza hiyo shahada yake kwahiyo anahitaji muda zaidi (ili atumie huo muda kusoma, Masters).

Sasa inavyoonekana Kuna elements zenye Chuki, roho mbaya na kuchomeana zimehusika hapa.
 
Back
Top Bottom