Afisa Mtendaji afungwa kifungo cha nje na kutakiwa kurejesha Tsh. Milioni 2 alizoiba

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Hukumu hiyo imetolewa na Mahakama ya Wilaya ya Mbozi, mkoani Songwe ikihusisha kesi ya Jinai No. 38/2023 dhidi ya Nassim Mbazu ambaye ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ipapa, Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi.

Kwa mujibu wa Waendesha Mashtaka, Mshtakiwa alikutwa na kosa la Wizi huku akiwa Mtumishi wa Umma, kinyume na Kifungu cha 258 (1) na 270 cha Kanuni ya Adhabu Sura ya 16 Marejeo ya mwaka 2022.

Mshtakiwa alikiri kosa na kutiwa hatiani ambapo Mahakama imeamuru atumikie Adhabu ya kifungo cha nje cha mwaka mmoja (Conditional Discharge), ikienda sambamba na kurejesha kwa Mwajiri wake fedha alizoiba ambazo tayari amezirejesha.
 
Back
Top Bottom