The Assassin
JF-Expert Member
- Oct 30, 2018
- 4,355
- 17,321
Nina brother wangu, tunachangia mzee ila kila mtu yuko na mama yake. Brother ananizidi kama miaka 6.
Miaka ile nakuja kusoma chuo kikuu, nilifikia kwa brother kwa sababu yeye tayari alikua anafanya kazi hapa Dar ila immediately baada ya mimi kuja akahamishiwa mkoa mwingine hivyo akaniacha na mke wake nyumbani kwake.
Kwa miaka yote ile nasoma nilikua naishi kwa brother, tuseme nyumbani kwetu. Jamaa alikua akija Dar once in a while.
Sasa baada ya kumaliza masomo tu hata kabla ya graduation shemeji akamshawishi brother anitimiue nyumbani kwake, yaani sina hili wala lile, nikaomba muda kidogo nijipange lakini ikashindikana, nikatimuliwa.
Nikahamia kwa brother mwingine mtoto wa baba mdogo, yeye alikua well off zaidi kuliko brother wangu. Nikakaa pale kama mwezi, kisha nikaunganishiwa kazi moja mkoani nikaenda huko baadae nikarudi Dar hadi leo.
Sasa, shemeji yetu bwana yeye hakutaka kabisa mahusiano yangu na brother, alihakikisha anatufarakanisha, alifanikiwa mwanzoni ila nadhani baadae bro akili zikamrudia akaona alifanya ujinga, tukaendelea vizuri ila sio kama zamani.
Sasa kwa kua shemeji alishalikoroga kwa ndugu zake na mume wake, mambo yalipoanza kumuendea kombo kwa mumewe akakosa msaada.
Hivi karibuni bro kaongeza mke wa pili, actually alifanya ndoa ya kimila kwani tayari alishakua amemzalisha huyo mwanamke watoto 3, sisi tundu tunajua long time, mke mkubwa kajua jana, amechanganyikiwa, presha imepanda amelazwa, hana wa kumpa faraja kwa upande wa mume. Mimi nasema atulie dawa imuingie.
Mimi binafsi nimefurahi sana. Sasa hivi mimi shemeji mdogo ndio mshikaji wangu, yule kimeo namuangalia tu.
Wanawake msijisahau sana, unaweza kufanikiwa kufarakanisha ndugu ila hutaweza kufuta undugu wao.
Ni hayo tu wakuu.