Broiler sio kuku wa kula kabisa!!

Broiler sio kuku wa kula kabisa!!

Hawa kuku sio wa kuwala kabisa, leo nilijaribu kunywa supu yake kama ilivyo supu ya kuku wa kienyeji nilijaribu supu ya Broiler duuh yaani ni kinyaa wakuu

Bila kuwekwawekwa viungo kwa wale wapika chipsi hawa sio kuku kabisa

Kuku wasio na baba wala mama!!

Hawa kuku marufuku nyumbani kwangu!!
Kwa hiyo ukaagiza supu ya kabeji?
 
hii si kweli , kuna kipindi nilikuwa nafuga sana kuku miaka hiyo ya 2005 nikishauza broiler wakiachwa wachache wale waliodumaa kidogo nawatoa nawachanganya na kuku chotara enzi hizo kenbro, wanakaa humo hadi wili 12 au miezi 5 wanakomaa vizuri kabisa na wanakuwa wakubwa kg 3 na wanazoea hadi kuvuruga mabustanini huko
Broiler anavuraga bustani?
 
Hawa kuku sio wa kuwala kabisa, leo nilijaribu kunywa supu yake kama ilivyo supu ya kuku wa kienyeji nilijaribu supu ya Broiler duuh yaani ni kinyaa wakuu

Bila kuwekwawekwa viungo kwa wale wapika chipsi hawa sio kuku kabisa

Kuku wasio na baba wala mama!!

Hawa kuku marufuku nyumbani kwangu!!
Ulaya wanakula kuku kissing?
 
kabisa kama unao waache 5 hadi kumi wafuge kawaida kama kuku wa kienyeji halafu utaleta majibu hapa ndugu
Labda wale chotara. Broiler unawajua lakini boss? Wale kuku ni wazembe hata kutembea kwa kasi hawawezi.
 
Mnakosea sana wasomi kubwabwaja mambo bila udadavuzi.

Hao wanaotaga mayai ya kutotoleshea vifaranga, lazima "wagongwe' na jogoo ili yai liweze kutotolewa, vinginevyo haiwezekani.

Broiler wanachomkosea, hatokoswi supu ni kwa ajili ya kukaangwa tu, nyama yake ni teketeke mno.

Ukishamzoea hutataka kuku wengine.

Halafu watu wengi wanalishwa broiler kwa ajili ya brand ya jina 'kienyeji' lakini si wa kienyeji.

Kuku wengi Dar ni wa kisasa (chotara) huwezi jua kama siyo mfugaji, maana wanafanana sana sura na kuku wa kienyeji na wanaitwa wa kienyeji kwa ajili ya mahitaji ya soko.
Nilikuwa siamini mkuu kuna mtu hawezi kula kuku kienyeji kabisa anakwambia wananuka mavi na si utani halikabisa
 
Labda wale chotara. Broiler unawajua lakini boss? Wale kuku ni wazembe hata kutembea kwa kasi hawawezi.
kwenye hili nina hakika kabisa ndugu kma una hata rafiki yako mwambie awajaribu wachache muone , wakishakomaa waachie nje sema kwenye fence pole pole utashangaa wamekuwa kama chotara
 
Wakuuu, kuku wa kienyeji wa kuoka mzima pure kienyeji,, karibuni Sana unampata kuku kasoro manyoya na utumbo tuuu! Haha 😂
 
kwenye hili nina hakika kabisa ndugu kma una hata rafiki yako mwambie awajaribu wachache muone , wakishakomaa waachie nje sema kwenye fence pole pole utashangaa wamekuwa kama chotara
Ok mkuu, ngoja ntamwambia jamaa mmoja huwa anakua nao kama 10,000 hivi kila miezi miwili.
 
Nilikuwa siamini mkuu kuna mtu hawezi kula kuku kienyeji kabisa anakwambia wananuka mavi na si utani halikabisa
Mkuu mazoea huzaa tabia nadhani!

Mtu anathamini alichozoea kula, ingawa kwa wasiozoea huona tofauti.

Ona sasa, watu hukimbilia kula kuku kwa brand name 'kienyeji', mwingine kumbe hali!

Tuseme vyakula hivi huliwa kwa mazoea pamoja na tamaduni za watu.

Utaona Mchina karost mbwa ama punda akifakamia kwa furaha kabisa, usimbeze, ni vyakula vyao pendwa!
 
Hawa kuku sio wa kuwala kabisa, leo nilijaribu kunywa supu yake kama ilivyo supu ya kuku wa kienyeji nilijaribu supu ya Broiler duuh yaani ni kinyaa wakuu

Bila kuwekwawekwa viungo kwa wale wapika chipsi hawa sio kuku kabisa

Kuku wasio na baba wala mama!!

Hawa kuku marufuku nyumbani kwangu!!
Broiler hapikwi supu.Ni watamu sana wakipikwa vizuri
 
Back
Top Bottom