British Airways yafunga virago Tanzania...

British Airways yafunga virago Tanzania...

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803
BA.jpg

​

BAADA YA KUWA TANZANIA KWA KIPINDI CHA MIAKA 82, TOKA ENZI ZA BOAC, SHIRIKA LA NDEGE LA UINGEREZA YAANI BRITISH AIRWAYS LIMEAMUA KUITOSA RASMI TANZANIA,GLOBU YA JAMII INAWEZA KUTHIBITISHA!



HABARI ZA UHAKIKA TOKA JIKONI ZINASEMA NDEGE YA MWISHO YA BRITISH AIRWAYS KUTUA TANZANIA ITAKUWA MACHI 29, 2013 WAKATI BOEING 767 YA SHIRIKA HILO AMBAYO NI KIJEBA (ZINAZOKUJA HUKU ZINA UMRI ZAIDI YA MIAKA 20) ITATUA KWA MARA YA MWISHO.


NA KWA HUZUNI KUBWA KWA WADAU WAKE, OFISI ZA BRITISH AIRWAYS PALE SERENA INN JIJINI DAR ES SALAAM ZITAPIGWA KUFULI RASMI MACHI 31, 2013
​
 
Wameona mdau wao mkubwa sultani kikwete Karibu muda wake uishe kwahiyo biashara itashuka sana
 
Huzuni mwe...........kibarua cha watu kimeota nyasi naona wametyme watu wameshalipa ada...........nadhani uchache wa abiria au classic ya huduma yao inakua ngumu kwa ukanda huu kumudu
 
Tatizo ni nini? Hamna Soko au kampuni inafulia?
 
Wapi MOD hii haiwezi kuwa Breaking News pls, hizi habari ziko long time kwenye mitandao
 

Kenya BRITISH AIRWAYS inakwenda mara 7 yaani kila siku

Uganda inakwenda Mara 3

Hizo zimeongezwa Mwaka JANA hawakuongeza TANZANIA walisema wanapeleka NDEGE NDOGO

Hata VISA watanzania wanaipatia KENYA... SISI wabaya au wanaona kuna MACHAFUKO???
 
Wapi MOD hii haiwezi kuwa Breaking News pls, hizi habari ziko long time kwenye mitandao

kwako sio ... kwangu mimi it is sababu nimeiona sasa hivi...
 
Nililiona hilo tatizo lao ni kudharau waafrika hasa watanzania na kuleta ndege za ajabu, wanaofuatia ni klm kwani nao watu wanaikacha sasa hivi
Ni bora upande emirets kwenda amsterdam mpaka dubai then ukachukua flight ya dubai to amsterdam utapanda ndege nzuri

Ila ukisema upande klm toka hapa kwenda amsterdam utalia

Utashangaa unakutana na mende....

Wanashindwa na waarabu katika soko la ndege waarabu bwana ndege wanazoleta huku ni nzuri...
BA inayokatosha atlantic ni msala sasa sijui tatizo huku kwetu ni nini?
 
What is wrong with this British people? ,stated with BP now British Airways.
 
Duh, hii bongo bwana, wenzetu wanaenda mbele sisi tunarudi nyuma! Kaazi kweli kweli!
 
Jana nilinunua online ticket ya Dar - London mwezi wa 5. Wataturudishia fedha? Mbona mpaka sasa bado ticket zinauzwa za mpaka november? Itakuwaje?
 
Si shangai uhusiano wa tanganyika na uingereza ullikufa tangu enzi za nyerere....waende tu!
 
Back
Top Bottom