Brigedia adam mwakanjuki amefariki dunia (simulizi la kifo chake)

Tugutuke

JF-Expert Member
Apr 21, 2011
501
165
Brigedia Jenerali mstaafu Adam Mwakanjuki aripotiwa kufariki dunia mapema hii leo.
May his soul R.I.P
 
Brigedia Jenerali mstaafu Adam Mwakanjuki aripotiwa kufariki dunia mapema hii leo.
May his soul R.I.P

Mungu ailaze roho ya Mzee Mwakyanjuki mahala pema poponi! Kawa kiongozi mkubwa kwa miaka mingi katika SMZ
 

Attachments

  • p+046.jpg
    p+046.jpg
    9.5 KB · Views: 162
Wanabodi, nimepokea taarifa ya msiba wa Brigedia Generali Adam Mwakanjuki amefariki dunia leo mchana baada ya kuugua ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu. Msiba uko nyumbani kwake Mbezi Beach karibu na Club Oasis. Kwa wasiomfahamu, marehemu alikuwa waziri wa sheria wa SMZ na baadae kuhamishiwa Kilimo baada ya mtafaruku wa kumteua Kadhi Mkuu wa Zanzibar ili hali ni Mkiristu!. RIP Brig. Gen. Mwakanjuki.
 
Ni Mtanzania ni baba wa mtu pia. Amelitumikia taifa kwa miaka mingi katika Jeshi la Wananchi Tanzania. Jamani sisi kama WaTanzania tunayo mila na desturi ya kuweka tofauti zetu pembeni endapo mmoja wetu anapoteza maisha sidhani kumlable mtu kwa mtindo huu ni ustaarabu. Tuwe na huruma kidogo leo kwake kesho kwako. Mungu awajaze nguvu wale wote waliofikwa na msiba huu.
 
Wanabodi, nimepokea taarifa ya msiba wa Brigedia Generali Isaack Mwakanjuki amefariki dunia leo mchana baada ya kuugua ugonjwa wa kiharusi kwa muda mrefu. Msiba uko nyumbani kwake Mbezi Beach karibu na Club Oasis. Kwa wasiomfahamu, marehemu alikuwa waziri wa sheria wa SMZ na baadae kuhamishiwa Kilimo baada ya mtafaruku wa kumteua Kadhi Mkuu wa Zanzibar ili hali ni Mkiristu!. RIP Brig. Gen. Mwakanjuki.
nadhani ni adam mwakanjuki sio issac
 
Generali Adam mwakanjuki alikuwa kamanda wetu pale Makutopora tulipokuwa National service operation yetu ikiitwa TUMAINI!! R.I.P afande.
 
Aliyekuwa Waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Brigedia Jenerali, Adam clement Mwakanjuki amefariki dunia katika hospitali ya Lugalo Jijini Dar es Salaam. Marehemu Mwakanjuki amefariki duani jana Alaasiri baada ya kuugua kwa mfupi. Hata hivyo haikuelezwa alikuwa akisumbuliwa na kitu gani lakini alifikishwa hospitalini mapema wiki hii.
[FONT=Georgia,"Times New Roman",serif][/FONT]




Brigedia Jenerali Mwakanjuki ni miongoni miongoni mwa wanasiasa wakongwe hapa nchini ambaye alianza kazi ya siasa kabla ya mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12, 1964 katika chama cha Afro shirazi (ASP) na baadae Chama Cha Mapinduzi (CCM).

FULL STORY>>>>>>>>>>>>


 
Back
Top Bottom