Brexit imegonga Mwamba, kiini macho cha Demokrasia!

Tangu useme eti airforce one ndio ndege kubwa kuliko zote duniani nilikudharau we mnyambi nikakuona kula kulala tuuu
 
Kama huyo Barbarosa kumiliki smartphone ya Itel anajiona kamaliza kutwa kushabikia mafisiemu
 
Elections in this day,anything can happen Jeremy Corbyn wa Labour was written off-magazeti karibu yote yakamgeuza punching bag-alichokubali kutoka kwa washauri ni kunyoa nywele,kuvaa tai na kununua suit mpya-mengine yote alikataa true to his communist values.Akawa target vijana na kuwateka. Leo hii ni shujaa wa Labour
 
We chizi kwani CCM huwa mnaitisha uchaguzi wa nn wakati mkijua wazi hamuwezi achia dola kwa karatasi na kalamu?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kura hata chizi anapiga ila linapokuja swala linalohusu maslai mapana ya nchi ambalo kueleweka kwake ni kugumu kwa watu wengi, kawaida wenye akili ndiyo huamua.

Dunia imeendelezwa na akili za wachache wakliojaliwa.
 
Tangu useme eti airforce one ndio ndege kubwa kuliko zote duniani nilikudharau we mnyambi nikakuona kula kulala tuuu
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Bora angesema zile Bombardier za Sizonje ndio nazani tungemuelewa
 
Usijifanye una uelewa mpana. Kura ya Brexit ilipigwa kwa ujinga wa Cameron na km ingekuwa ni nchi km US au Israel angekuwa shot toka anaanza kuwaza juu ya kuitisha kura.Mataifa yameundwa kwa akili kubwa za wachache.

Mambo ya msingi ya nchi yanaamuliwa na wachache ambao akili zao zimedhihirika kuwa ni kubwa sana sio kwa kura ambazo hata chizi anapiga.
 
Huyo mleta hiyo mada inaonyesha hajawahi kufika hats airport
 
Barbarosa, sometime ukichemka kubali tu kwamba umechemka!

Narudia, Brexit iko pale pale!!! Hata hiyo poster inadhihirisha!

Usije ukajichanganya hapo palipoandikwa HARD Brexit RIP ukadhani ndo basi tena! Kwa muda sasa kilichopo UK sio Brexit or non-Brexit bali but the question is HOW to exist! Hard or Soft Brexit!

Mama May was in favor of Hard Brexit wakati mbia wake, DUP alikuwa in favor of Soft Brexit!! Na ndio maana kwenye post yangu ya awali nilisema kutokana na May kukosa majority hivi sasa atalazimika kuweka mambo sawa ndani kwanza kabla ya kuingia kwenye EU Negotiation Table! Kwa mfano Unionists wanaweza kutoa condition kwamba, endapo unataka u-join force na sisi basi tunafanya Soft Brexit!

Remember, wenzetu kufanya serikali ya mseto isn't all about power but fulfilment of their interests. Katu Unionists hawawezi kushobokea serikali ya mseto simply because watapata nafasi serikalini bila kujali matakwa yao!!!
 
Na jinsi siku zinavyoenda itakuwa tabu kwa Conservative, Corbyn azidishe nguvu tu kwa vijana, adai EU-in, awasomeshe vijana wanachomisi au watakachomisi EU, kama kawaida ya Labour adai usawa na kodi kwa matajiri, atazikumba kura nyingi tu..Hawa vijana wa UK wa kisasa hawajali dini, rangi wala sex orientation, wao usawa na maendeleo, kujichanganya na dunia..Vijana wamechoka kuwaambia nini cha kufanya, kutishwa na ugaidi feki, kutishwa uhamiaji n.k. n.k.
 
Mtoa mada yupo sahihi Waziri Mkuu Theresa May aliitisha uchaguzi wa haraka ili apate mandate kubwa katika kujitoa EU. Lakini baada ya uchaguzi na chama cha conservative kupoteza wingi wa wabunge itabidii waziri mkuu aunde serikali ya mseto. Kunauwezekano mkubwa huyu mama asiendelee kuwa waziri mkuu. Itabidi serikali ya UK wa review katika masuala ya kujitoa EU
 
No! Umetoa angalizo zuri sana manake ni kweli wengi wanashindwa kutofautisha kati ya Ireland (Rep) and Northern Ireland kiasi kwamba hata mimi kuishia kusema Ireland, officially ni sawa na kusema Rep of Ireland ingawaje intention yangu ni Northern Ireland ya akina Arlene Foster!

Aidha ni kweli pia wapo wanaoshindwa kutofautisha kati ya UK, Great Britain & England! Tena kuweka kumbukumbu sawa hapo juu, pia kuna tofauti kidogo kati ya GB na UK kwa sababu Northern Ireland sio sehemu ya GB; au kwa maana nyingine UK - Northern Ireland = GB.

Thanks kwa angalizo... ni bahati mbaya sana nilichelewa kuiona hii post yako!!!!
 
Hivi una habari anachosema Barbarosa na wewe ni vitu tofauti?! Wakati wewe unadai May aliitisha uchaguzi wa haraka ili apate mandate ya kujitoa EU (na ndio ukweli wenyewe) mleta mada anadai Theresa May aliitisha uchaguzi wakati alifahamu fika kwamba angeshindwa na matokeo yake lengo la elites kutotaka Brexit limetimia and in turn, kuizika maoni ya Waingereza walio wengi waliotaka Brexit!!!

Kwavile Barbarosa sio mgeni kwangu hapa JF; lengo lake kwenye thread hii ni lile lile... WAZUNGU!!!! Hapa anajaribu kuonesha "unafiki" wa WAZUNGU linapokuja suala la demokrasia... kwamba, hao hao wanaoimba demokrasia leo hii wanataka kunyang'anya maoni ya walio wengi waliotaka Brexit!!

Sio kwamba Barbarosa is in favor of hao walio wengi bali tukikubaliana nae hatimae ile discredit yake kwa Wazungu itakuwa imetimia!!!!
 
Duh! Unaweza kuwa unajua kweli lakini kwa dharau hizi mh! Kuna ulazima kweli wa kumdharau mtu hivi? Kuna ubaya gani ukimwelewesha kwa ustaarabu tu?
 
Unaona sasa. Unamwelewesha kwa kina na kwa uzuri kabisa. Huu ndiyo ustaarabu. Hata mtu unapata raha ya kufuatilia mjadala na kujifunza. Niko na kidaftari hapa naandika pont zako. Endelea kumwaga nondo...
 
Nguruvi acha kupamba siasa za uingereza as if watu hawana uwezo wa kuzifuatilia...wewe unaleta uzamani...eti ili uwe msomi basi utembee na gazeti kuubwa la DailyNews ...hizo nyakati zimepitwa na wakati.

Mleta mada ameshapima hiko unachokiita kina kirefu na kuona wazi maamuzi ya wananchi hayatoheshimiwa...

Hata msimamo wa May katika Brexit ni wa mashaka sana...pengine ndio maana anayapeleka mambo kisanisanii...

Mleta mada anawaoesha kuwa huko mnapojidai kuiga siasa za kidemokrasia kuna unafiki mkubwa sana ...na tunaaswa kuacha kuiga unafiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…