Brela namba mlizoweka kama msaada hazina maana

Brela namba mlizoweka kama msaada hazina maana

queen of the jungle

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2017
Posts
228
Reaction score
430
Kuna namba ziko Brela kama technical support kwa ambaye umekwama sehemu unaposajili kampuni imekuwa kero hazipokelewi, nimejaribu kupiga zaidi ya mara 40 toka jumatatu hakuna anayepokea namba yangu na nahitaji msaada ili niweze kujaza form online, kiukweli nimejikuta napata hasira kwa nini wameziweka hizo namba kama msaada wakati hakuna wa kuzipokea namba hizo ni 0735331000 na 0735331001
kama wanaona wanazidiwa na mzigo wa kazi kuna vijana kadhaa wako na vyeti ukimpa hata kazi ya kupokea simu utamsaidia saana kuliko kuchelewesha usajili ambao unalenga kuongeza pato la taifa
Nawasilisha
Queen of the jungle kutoka Mara
 
Kama hutajali unaweza kueleza shida yako hapa au PM tukakusaidia vilevile kwa utaalamu wetu mdogo tuliona katika maswala hayo. Naona wamezidiwa update sasa zinachukua miezi miwili na sababu nyingine za kukataa hazina mashiko
 
Back
Top Bottom