Mfiaukweli
JF-Expert Member
- Aug 30, 2018
- 5,636
- 8,774
Wandugu;
Nipo kwenye mizunguko yangu ya kutafuta shekeli kwenye mji mmoja hapa nchini. Sasa hivi nipo kwenye daladala - wanaita mzunguko hapa - na nimemsikia jamaa mmoja akiongea na mwenzake kwa simu. Kwa kawaida sina mazoea ya kusikiliza mazungumzo ya watu, ila attention yangu kwenye mazungumzo ya huyu ndugu yametokana na yeye kulalamikia huduma mbovu za dawati la msaada la BRELA. Kwa kifupi huyu ndugu anasema simu zao ama hazipatikani au hazipokelewi.
Nilidhani ni mimi peke yangu ndie huwa nakumbana na hili tatizo; namba wanazozinadi kuwa ukipiga utapata msaada zaidi ni hizi:
0735 331001, 0735 000003 na/au 0735 331004.
Binafsi SIJAWAHI kupiga namba yeyote kati ya hizo na ikapokelewa. BRELA; kama hamtaki kupigiwa kuna sababu gani ya kuzitangaza hizo namba?
Halafu kuna watu wanatuambia kuwa awamu hii nidhamu ya kazi imepanda na uzembe hakuna!