Breaking news: papic abwaga manyanga yanga

yahoo

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
3,527
1,405
Kocha wa yanga kostad papic amebwaga manyanga kuifundisha yanga.hii imetokana na uongozi wa yanga kumhoji kuhusu mahusiano yake na wachezaji kwani ilionekana anaendekeza chuki na baadhi ya wachezaji kiasi cha kuwapiga benchi ,hadi kusahaulika kama wanachezea yanga huku wachezaji hao wakipokea mishahara kama kawa.ndipo papic akaamua kususa na kurudi kwao.
Soarce: clouds a.k.a simba tv ,a.k.a kamati ya nidham ya tff.a.k.a tawi la simba ,
 
Hata mm nimeckia habari hyo yanga walichemsha kumfukuza sam timbe papic ni msumbufu sana
 
Tuondokane na kasumba ya kuegemea/kuamini sana makocha wa nje! Shehata kafanya makubwa sana kama kocha mzawa Misri, Yanga hawa mpango wa kumsomesha Chambua ukocha umefikia wapi? Hatupendi kuunda vya kwetu tunakimbilia vilivyoundwa
 
Kama ni kweli kajiuzuru hii itakuwa ni Habari njema sana kwangu.....

Papic hafai hata kidogo kuwa kocha wa Yanga......Anaendekeza makundi tu miongoni mwa wachezaji na kushusha viwango vya wachezaji.....

Na aondoke zake maana HANA JIPYA.......Namkumbuka sana mtaalamu SAM TIMBE aliyetuletea ubingwa wa VPL na CECAFA
 
Poleni! Naona kumbukumbu zetu kiduchu! Alipokuja aliikuta Yanga chini ya Sam Timbe iko relegation zone. Kaipandisha hadi sasa inachuana na Simba & Azam kileleni!
 
Kocha wa yanga kostad papic amebwaga manyanga kuifundisha yanga.hii imetokana na uongozi wa yanga kumhoji kuhusu mahusiano yake na wachezaji kwani ilionekana anaendekeza chuki na baadhi ya wachezaji kiasi cha kuwapiga benchi ,hadi kusahaulika kama wanachezea yanga huku wachezaji hao wakipokea mishahara kama kawa.ndipo papic akaamua kususa na kurudi kwao.
Soarce: clouds a.k.a simba tv ,a.k.a kamati ya nidham ya tff.a.k.a tawi la simba ,

Fitina hizo nakombe tutalibeba
 
Vipi hawaktmtandika bakora? Yanga wakimchoka kocha huwa hawakopeshi, tunangoja kusikia anadai mshahara wa miezi kadhaa na bili ya hoteli anakoishi.
 
eeehhh....kidedea...eehhh....kidedea....

Kashtuka, mnyama hakamatiki...lols
 
Papic hafai hata kidogo kuwa kocha wa Yanga......Anaendekeza makundi tu miongoni mwa wachezaji na kushusha viwango vya wachezaji.....

Hivi Stephano Mwasika na mabondia wenzake hawakuliona hili wakalishughulikia ipasavyo?
 
Yanga walimdanganya kuwa anakuja kufundisha soka badala yake alipofika akaambiwa afundishe ndondi akawaambia yeye amesomea kufundisha soka na si masubwi kaeni na timu yenu ya ndondi nitatafuta timu ya mpira hata kama ni daraja la nne..Hongera sana papic kwa uamzi huo huwezi kufundisha timu ya wahuni kuanzia wachezaji mpaka wazee wao
 
Kama ni kweli kajiuzuru hii itakuwa ni Habari njema sana kwangu.....

Papic hafai hata kidogo kuwa kocha wa Yanga......Anaendekeza makundi tu miongoni mwa wachezaji na kushusha viwango vya wachezaji.....

Na aondoke zake maana HANA JIPYA.......Namkumbuka sana mtaalamu SAM TIMBE aliyetuletea ubingwa wa VPL na CECAFA

Pole Mkuu, Yanga hawana noma, watamwajiri tena Timbe mara ya pili, mbona Papic aliondoka na akarudi tena?
 
Namlaumu Papic sijui kwa nini alirudi kuifundisha Yanga wakati anayajua matatizo ya uongozi wa timu,naamini hata Simba watafuata nyayo za Yanga Milovic naye atatimuliwa au ataondoka mwenyewe,tusubiri ligi iishe
 
mkuu unapaswa kutambua kitu kimoja kwa sasa simba ina watu wa mpira....halafu hawana njaa za kijinga hivyo kinachofata ni mafanikio
 
mkuu unapaswa kutambua kitu kimoja kwa sasa simba ina watu wa mpira....halafu hawana njaa za kijinga hivyo kinachofata ni mafanikio
Mtu wa mpira alikuwa Hassan Dallali,unakumbuka Simba walibeba ubingwa bila hata kupoteza mechi na wakati ule Yanga alikuwa mteja wa Simba.Tangu waje hao watu wa mpira (Rage na wenzie) wamefanya nini la maana baada ya kuona Yanga wamemuajiri Timbe na wao wakamuajiri Bassena .Yanga walivyomtimua Timbe na kurudisha Papic na wao wakamrudisha Milovan
 
Back
Top Bottom