Breaking News: Muhimbili Waharibu tena.!

Breaking News: Muhimbili Waharibu tena.!

yani utoe Maiti Dar "hospitali" hadi Tanga bila kumfunua?
kuna watu wanaogopa maiti wewe!!!
inawezekana wamechanganywa wakati wa kuchukua majeneza, labda walishakagua, wakatoa hela ya kusafisha na kuweka kwenye jeneza,

jamaa wakaja, wakaambiwa chukueni wakabeba kumbe tofauti. ina wezekana hawakuangalia kabisa.

Kumbuka kuangalia mwili uliowekwa kwenye jeneza ni mpaka umfunue ile nylon, then sand, ndo uhakiki! Watu wengi hawawezi kufanya hivyo!!
 
Pole zao sana!
Ina maana hawakufungua kujiridhisha kabla ya kuondoka?...waliochukua walikuwa watu wa mshahara nini?

Hata mimi nilitaka kusema hivyo, yaani upewe maiti uchukue mpaka nyumbani na kuanza kusafirisha haujaifungua!!!!! Ni jambo linalosababishwa na uoga uliopitiliza. Pole zao.
 
Lord Have Mercy!! Kwamba hakukuwa hata na mtu mmoja aliehakiki mwili kabla hawajauingiza kwenye jeneza...!! Kwamba majeneza yanafanana hence wakakosea na kuchukua lenye maiti ya mhindi?!! ?!!! Am just thinking aloud.....maswali mengi kuliko majibu!
 
Pole zao sana!
Ina maana hawakufungua kujiridhisha kabla ya kuondoka?...waliochukua walikuwa watu wa mshahara nini?



Mkuu!

Mi nafikiri waliochukuwa maiti hii ya kuelekea Mkoani walikuwa watu wa mshahara bila kukosea!
Sababu ya kunifanya kusema hivyo ni kwmb haiwezekani mkatoka Dar kuelekea Mkoa mwingine bila hata ya kumwomba mwenyenzi MUNGU mwingi wa rehema ktk hali ya kusafirisha marehemu.

Haiwezekani hata kidogo!!
 
Unapoenda mochwale zoezi la kutambua mwili wa marehemu ndo huwa la kwanza kabla jamaa hajaanza kuushughulikia kama kuuosha,kuupanga kwa geneza ,kuupiga pamba etc
So ndugu walaumiwe na si MNH

kama marehemu alikuwa akijipakaa ile dawa yetu wanaiitaje mweuzi kuwa mweupe
haata hivyo rip marehemu sukanachuse
 
Inaonesha hao waliokuja kuchukuwa maiti na wao walikuwa maiti. Hii kali ya mwaka!
 
Chanzo cha habari kikusaidie nini? Wewe rudi nyuma eti chanzo mnaniboa watu nyie sasa unataka sema katunga au. Phwuuuuu

[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: contentheading, width: 100%"]Muhimbili watoa mwili wa Muhindi kwa Waswahili [/TD]
[TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: contentpaneopen"]
[TR]
[TD="class: createdate"] Tuesday, 27 March 2012 19:24 [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] 0digg

Steven William, Muheza
WAFANYAKAZI wa chumba cha maiti katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar wametoa mpya baada ya kuwapa ndugu mwili wa marehemu ambaye sio ndugu yao.

Ndugu wa marehemu walibaini kuwa mwili waliouchukua si wa ndugu yao bali ni wa mtu mwenye asili ya kihindi, muda mfupi kabla ya kufanya maziko jana, baada ya kuufikisha kijijini kwao mkoani Tanga.

Juzi usiku, ndugu hao walikwenda katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuuchukua mwili wa ndugu yao aliyefahamika kwa jina la Luku Mwaopea ambaye ni mwenyekiti wa CCM kijiji cha Mkanyageni wilayani hapa.

Kwa mujibu wa ndugu hao, walikabidhiwa bila kuutizama majira ya saa mbili usiku na hatimaye kuupakia ndani ya gari aina ya Toyota ukiwa umehifadhiwa katika jeneza na kuanza safari kuelekea kijiji cha Mkanyageni wilayani Muheza kwa maziko.

Ndugu hao baada ya kukabidhiwa mwili wa marehemu, walianza safari kuelekea wilayani Muheza ambapo walifika katika kijiji cha Mkanyageni jana asubuhi majira ya saa tatu.

Wakati wa hatua za mwisho za maandalizi ya maziko, ndipo ndugu wa marehemu walipobaini kwamba mwili waliopewa si wa ndigu yao, walipoanza kuutizama kwa heshima ya mwisho.

Kwa msgangao, ndugu hao walibaini kuwa wamepewa mwili wa Muhindi badala ya ndugu yao, suala lililozua mshangao kwa kila aliyekuwepo msibani hapo.

Baada ya tukio hilo ndugu wa marehemu wafanya mawasiliano na wahudumu wa chumba cha maiti katika hospitali ya Muhimbili kuulizia mwili wao kama upo ambapo walijibiwa upo.

Hata hivyo safari ya kuurudisha mwili wa marehemu huyo mwenye asili ya Kihindi aliyefahamika jina moja la Lukumai ilianza tena kwa ndugu kulazimika kuurejesha Dar es Salaam ili wakamchukue ndugu yao kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika tena leo.

Mmoja wa ndugu wa marehemu huyo, Mwendo Abdallah alisema kuwa tukio hilo ni la kweli na kwamba lilitokana na makosa yaliyofanya wakati wa kukabidhiwa mwili huo huko Muhimbili.

Hata hivyo wafanyakazi wa chumba cha maiti Muhimbili walipoulizwa walisema kuwa marehemu hao wamefanana majina yao ambapo yule Muhindi anaitwa Lukumai na yule ndugu yao anaitwa Luku Mwaopea ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Mkanyageni kata ya Ngomeni wilayani Muheza.

Hata hivyo kwa sasa kaburi lililochimbwa lipo wazi kwa ajili ya mazishi ya kesho na kwamba viongozi wa chama na Serikali walihudhuria mazishi hayo na kushangazwa na hatua hiyo.


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Mbona kwenye pasi ya kusafiria tunanalazimishwa kuweka majina matatu, kwa na sehemu kama hizi nazo wasifanye hivyo ili kupunguza kama si kuondoa uwezekano wa kuchanganya majina?
 
Back
Top Bottom