Muhimbili watoa mwili wa Muhindi kwa Waswahili!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muhimbili watoa mwili wa Muhindi kwa Waswahili!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Matola, Mar 28, 2012.

 1. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #1
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Muhimbili watoa mwili wa Muhindi kwa Waswahili [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Tuesday, 27 March 2012 19:24 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Steven William, Muheza
  WAFANYAKAZI wa chumba cha maiti katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar wametoa mpya baada ya kuwapa ndugu mwili wa marehemu ambaye sio ndugu yao.

  Ndugu wa marehemu walibaini kuwa mwili waliouchukua si wa ndugu yao bali ni wa mtu mwenye asili ya kihindi, muda mfupi kabla ya kufanya maziko jana, baada ya kuufikisha kijijini kwao mkoani Tanga.

  Juzi usiku, ndugu hao walikwenda katika hospitali hiyo kwa ajili ya kuuchukua mwili wa ndugu yao aliyefahamika kwa jina la Luku Mwaopea ambaye ni mwenyekiti wa CCM kijiji cha Mkanyageni wilayani hapa.

  Kwa mujibu wa ndugu hao, walikabidhiwa bila kuutizama majira ya saa mbili usiku na hatimaye kuupakia ndani ya gari aina ya Toyota ukiwa umehifadhiwa katika jeneza na kuanza safari kuelekea kijiji cha Mkanyageni wilayani Muheza kwa maziko.

  Ndugu hao baada ya kukabidhiwa mwili wa marehemu, walianza safari kuelekea wilayani Muheza ambapo walifika katika kijiji cha Mkanyageni jana asubuhi majira ya saa tatu.

  Wakati wa hatua za mwisho za maandalizi ya maziko, ndipo ndugu wa marehemu walipobaini kwamba mwili waliopewa si wa ndigu yao, walipoanza kuutizama kwa heshima ya mwisho.

  Kwa msgangao, ndugu hao walibaini kuwa wamepewa mwili wa Muhindi badala ya ndugu yao, suala lililozua mshangao kwa kila aliyekuwepo msibani hapo.

  Baada ya tukio hilo ndugu wa marehemu wafanya mawasiliano na wahudumu wa chumba cha maiti katika hospitali ya Muhimbili kuulizia mwili wao kama upo ambapo walijibiwa upo.

  Hata hivyo safari ya kuurudisha mwili wa marehemu huyo mwenye asili ya Kihindi aliyefahamika jina moja la Lukumai ilianza tena kwa ndugu kulazimika kuurejesha Dar es Salaam ili wakamchukue ndugu yao kwa ajili ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika tena leo.

  Mmoja wa ndugu wa marehemu huyo, Mwendo Abdallah alisema kuwa tukio hilo ni la kweli na kwamba lilitokana na makosa yaliyofanya wakati wa kukabidhiwa mwili huo huko Muhimbili.

  Hata hivyo wafanyakazi wa chumba cha maiti Muhimbili walipoulizwa walisema kuwa marehemu hao wamefanana majina yao ambapo yule Muhindi anaitwa Lukumai na yule ndugu yao anaitwa Luku Mwaopea ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM kijiji cha Mkanyageni kata ya Ngomeni wilayani Muheza.

  Hata hivyo kwa sasa kaburi lililochimbwa lipo wazi kwa ajili ya mazishi ya kesho na kwamba viongozi wa chama na Serikali walihudhuria mazishi hayo na kushangazwa na hatua hiyo.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BIG X

  BIG X JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 4, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kaazi kweli kweli!!!
   
 3. sinafungu

  sinafungu JF-Expert Member

  #3
  Mar 28, 2012
  Joined: Feb 13, 2010
  Messages: 1,406
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Ndo shida ya kuogopa maiti, hivi wangeliungalia huo mwili pale pale kabla ya kuondoka hilo lingekuwepo..........?
   
 4. Mlitika

  Mlitika JF-Expert Member

  #4
  Mar 28, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 458
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hii habari tunayo jamvini tangu jana saa nane mchana. Soma kwanza post zilizohewani kabla ya kutupotezea muda.
   
 5. rushanju

  rushanju JF-Expert Member

  #5
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 2,342
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  Kurudia post kunakara bana. hii imeletwa jana watu tukachangia wewe bila kusoma unaamka na ya kwako
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Acha kuongea kama mlevi mimi hapa nimeleta reliable source ya habari, ni jukumu lako kama mwana Forum kuwajulisha moderators waziunganishe hizi thread badala ya kubwabwaja kama mla ugoro. wewe umeleta habari gani za kushare na wenzako!?
   
 7. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #7
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Muda wako unaupoteza wewe mwenyewe kama utaacha kufanya shughuri zako za msingi na kushinda kwenye mtandao, unachotakiwa kufanya ni kuwajulisha mods waziunganishe hizi thread na sio kuongea kama bata. wewe unaweza kupitia post zote humu JF? YAANI WATU WENGINE AKILI UKWAJU KWELI KWELI.
   
 8. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #8
  Mar 28, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  hiki kichwa cha habari hii kinaonyesha mwandishi alisoma shule ya kata.
  Kwani waswahili hawawezi kwenda kuchukua mwli wa marehemu ambaye ni muhindi/mzungu.cha kushangaza ni kipi hapa.
  Nijuavyo ukichukua mwili unaonyeshwa na kusaini.
   
 9. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #9
  Mar 28, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Mnashangaa nini hospitali ya Muhimbili? Je wale wagonjwa mmoja aliyefanyiwa operasheni ya mguu badala ya kichwa na mwingine operesheni ya kichwa badala ya mguu?
   
Loading...