Botswana:Wageni waanza kufungasha virago

Delegate

JF-Expert Member
Jan 4, 2012
331
201
Wakuu
hali imebadilika na sasa hapa Botswana wageni hasa wafanya biashara wenye makampuni na wafanya kazi wanaofanya serikalini na makampuni binafsi wameanza kufungasha virago baada ya mambo kubadilika ghafla,serikali ya hapa imeleta sera mpya inayobana wageni kiasi kwamba ukiwa mgini huwezi kabisa kufanya biashara,hilo limewafanya wengi washindwe kuishi hapa baada ya kuonekana serikali inaleta standard ya Europe,
baada ya kuwanyima wageni wengi permit za kuishi na kufanya kazi sasa wameanza kulazimisha makampuni ya wageni kutopewa kazi na tunakoelekea sasa hivi ni kufungasha
tulifikiri wamelenga wakenya peke yao kwani kila mkenya aliyeomba permit alitolewa nje,sasa wamegeuza kibao na kuandama wageni wote ijapokuwa kwa watanzania wanalegeza kamba kidogo
ndugu zangu tunarudi nyumbani tujenge taifa letu,hayo maneno nimewaambia waswana na kuwahakikishia kuwa watakuja juta kwani hawa watu bado ni immature
tunarejea nyumbani tukiamini mtatupokea baada ya kuishi nje ya nchi yetu kwa miaka ming,mimi binafsi nimeishi botswana miaka 12 sasa
tunaamini siasa za tanzania hazitatuvunja moyo kwani tunakuja ku share skill na life education kwa ujumla tuliyoipata huko nje
tunaamini serikali itagundua uwezo mkubwa tulio nao na kututumia tuweze kuendeleza nchi yetu
 
hatujaua kwetu mkuu,no place like home,japokuwa siasa za nyumbani zinakatisha tamaa lakini hakuna jinsi

Ndo mje tuungane kubadilisha hali ya kisiasa nchini mwetu! waachieni nchi yao hao Makirikiri!
 
Wakuu
hali imebadilika na sasa hapa Botswana wageni hasa wafanya biashara wenye makampuni na wafanya kazi wanaofanya serikalini na makampuni binafsi wameanza kufungasha virago baada ya mambo kubadilika ghafla,serikali ya hapa imeleta sera mpya inayobana wageni kiasi kwamba ukiwa mgini huwezi kabisa kufanya biashara,hilo limewafanya wengi washindwe kuishi hapa baada ya kuonekana serikali inaleta standard ya Europe,
baada ya kuwanyima wageni wengi permit za kuishi na kufanya kazi sasa wameanza kulazimisha makampuni ya wageni kutopewa kazi na tunakoelekea sasa hivi ni kufungasha
tulifikiri wamelenga wakenya peke yao kwani kila mkenya aliyeomba permit alitolewa nje,sasa wamegeuza kibao na kuandama wageni wote ijapokuwa kwa watanzania wanalegeza kamba kidogo
ndugu zangu tunarudi nyumbani tujenge taifa letu,hayo maneno nimewaambia waswana na kuwahakikishia kuwa watakuja juta kwani hawa watu bado ni immature
tunarejea nyumbani tukiamini mtatupokea baada ya kuishi nje ya nchi yetu kwa miaka ming,mimi binafsi nimeishi botswana miaka 12 sasa
tunaamini siasa za tanzania hazitatuvunja moyo kwani tunakuja ku share skill na life education kwa ujumla tuliyoipata huko nje
tunaamini serikali itagundua uwezo mkubwa tulio nao na kututumia tuweze kuendeleza nchi yetu

Karibu sana nyumbani uka-impart ujuzi wako kwa wenzio, nimefurahi kusikia Botswana bado ina i-respect sana TANZANIA.
 
Hatuwataki tumesha jaa,Nendeni Sudan kuna taifa jipya kule linataka Greener Pastures kama nyie,wa tswana wame wa drain sasa mmekuwa useless.Serikali yenu ilijibana kuwasomesha matokeo yake mkapeleka skills kwengine.
 
tulifikiri wamelenga wakenya peke yao kwani kila mkenya aliyeomba permit alitolewa nje,sasa wamegeuza kibao na kuandama wageni wote ijapokuwa kwa watanzania wanalegeza kamba kidogo
ndugu zangu tunarudi nyumbani tujenge taifa letu,hayo maneno nimewaambia waswana na kuwahakikishia kuwa watakuja juta kwani hawa watu bado ni immature

Lol ingekuwa ni waKenya pekee hamna neno.
 
Tunawachukua kama wasaliti kwani mlikimbia kujenga nchi yenu kutaka fedha kirahisi. Kumbukeni hata sisi tunazo elimu kama zenu lakini we decided to serve our motherland regardless of the situation that prevailed! Tanzania ni mama yetu hata kama ni mchawi ndiye mzazi hatuwezi kumkimbia. Home is best!
 
msije mkawa wale madakitari waliogoma walipofukuzwa mkaona mkimbilie huko sasa nako mmekuta mambo magumu
 
sasa madaktari wetu wataenda wapi, manake wengi walitegemea wangeenda botwana...jamani mbona madili ya watu yanavurugika hivi?
 
...........tunakuja ku share skill na life education kwa ujumla tuliyoipata huko nje
tunaamini serikali itagundua uwezo mkubwa tulio nao na kututumia tuweze kuendeleza nchi yetu
Hayo mekundu sijui!!
Labda serikali nyingine si hii ya Kikwete na CCM.
Serikali iliwashauri wataalam kutafuta mwajiri mbadala the last time I checked.
 
njooni tu wakuu ila kazi kubwa apa bongo ni kuondoa siasa za kibadhilifu tulizonazo ambazo ndizo zinaleta umaskini wa nchi,hatuna kazi ingine hapa zaidi ya kupambana na wanasiasa hawa adi kileweke laa sivo mengine ayo yenu hayatafanikiwa

welcome home
 
usije home ukitegemea serikali hii inatambua hata chembe ya mchango wako kwa taifa hili...

njoo na ujanjaujanja maana hii nchi wajanjawajanja ndio wanaoila na kuifaidi kwa rahaaa na sio nyie mnaojiita wasomi..maana sikuhizi mmekuwa wengi hadi mnashindanishwa na watoto wa madrasa..wasomi wa qoran...

Kwani wewe mwenzetu ni msomi wa nini???...mengine mliyosomea huku hata hatuyahitaji..usijekuwa msomi wa nuclear physics ukija hapa huna chako na madini tushauza so 4get ur nuclear power reactors n blahblah... Utaishia kunywa whisky, wines mara unafulia kisha unaanza bia konyagi na viroba..kisha unaamia banana nzela na mwishoni gongo na chibuku kisha tunakuzika..
Pole
sana msomi unayetaka kurudi nyumbani ambako hakuna hada dalili ya kuthaminiwa.
 
Wakuu hali imebadilika na sasa hapa Botswana wageni hasa wafanya biashara wenye makampuni na wafanya kazi wanaofanya serikalini na makampuni binafsi wameanza kufungasha virago baada ya mambo kubadilika ghafla,serikali ya hapa imeleta sera mpya inayobana wageni kiasi kwamba ukiwa mgini huwezi kabisa kufanya biashara,hilo limewafanya wengi washindwe kuishi hapa baada ya kuonekana serikali inaleta standard ya Europe, baada ya kuwanyima wageni wengi permit za kuishi na kufanya kazi sasa wameanza kulazimisha makampuni ya wageni kutopewa kazi na tunakoelekea sasa hivi ni kufungasha tulifikiri wamelenga wakenya peke yao kwani kila mkenya aliyeomba permit alitolewa nje,sasa wamegeuza kibao na kuandama wageni wote ijapokuwa kwa watanzania wanalegeza kamba kidogo ndugu zangu tunarudi nyumbani tujenge taifa letu,hayo maneno nimewaambia waswana na kuwahakikishia kuwa watakuja juta kwani hawa watu bado ni immature tunarejea nyumbani tukiamini mtatupokea baada ya kuishi nje ya nchi yetu kwa miaka ming,mimi binafsi nimeishi botswana miaka 12 sasa tunaamini siasa za tanzania hazitatuvunja moyo kwani tunakuja ku share skill na life education kwa ujumla tuliyoipata huko nje tunaamini serikali itagundua uwezo mkubwa tulio nao na kututumia tuweze kuendeleza nchi yetu
Ninavyoijua Tswana,ujuzi wa kutuletea TZ huna,hata biashara tofauti na zilizoko TZ ua ya kipekee hauna,hata fedha hauna,ukija huku utaanza moja bora ujaribu huko South Sudan unaweza kutoka kwani wanahitaji watu kama nyie mnaopenda kuwatumikia wengine zaidi ya ulikotoka.huku TZ nina uhakika utachanganyikiwa tu ukiona kinachoendelea huku watu hawategemei mishahara 100%,supermarket kama Tswana kila mtu anakajisehemu kake ka kumuongezea maisha,hiyo miaka 12 uliyopoteza huko bondeni utaijutia maishani kwako.
 
Muieleze ukweli serikali yenu ya Tanzania waache tabia ya kukumbatia wageni na waanze kuwajali wazawa kwani kama nyie huko nje hawawajali iweje sisi tuwakumbatie?
 
Surely hao jamaa waatajuta kuwafanyia wageni fitina. kwa ufahamu wangu, ninajua ni wageni waliowafikisha hapo walipo! University of Botswana kwa kipindi fulani karibia kila Head of Department alikua mgeni, specifically Mtanzania. Najua mpaka sasa hawajajipanga vizuri sana katika sekta mbalimbali kujiongoza, na wageni wakiondoka watawakumbuka!
 
Back
Top Bottom