Kwa kasi hii ya Azam Wachina wa StarTimes wajiandae kufungasha virago?

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,013
17,925
Kwa kasi hii ya Azam wachina wa Startimes wajiandae kufungasha virago?

Naona Azam media wanazidi kuja kwa kasi leo hii wamezindua minara ya bilioni 50 mikoa 21

Baada ya Dish wamekuja na vya Antenna, hawa jamaa wapo vizuri sana naona kwa sasa Wachina wa Startimes wajiandae kisaikolojia tu maana sidhani kama kuna mtu timamu atatumia vile vidubwashwa vyao.

Kongole Azam media sasa huku kwa vya Antenna ndo mnaenda kusepa na nyomi ya kijiji.
 
Ukitoa DSTV king'amuzi kinachofuata kwa ubora ni startimes, kwa upande wa football wako vizuri, series za kizungu, kihindi kichina, kikorea na kituruki wako vizuri kwa upande wa Tamthilia zilizotafsiriwa ingawa mimi sio mpenzi nazo ila The Brothers hainipiti, kwa upande wa michuano ya kimataifa star times inaonyesha ligi nyingi zaidi ya Azam huku mpaka Ronaldo anaonekana,kwa upande wa soka la Africa, wanaonyesha michuano yote inayosimamiwa na caf, Tunaangalia ligi ya kenya, tunaangalia ligi ya Uganda na kwa upande wa Tanzania wameanza na champioshp,
 
Kwa kasi hii ya Azam wachina wa Startimes wajiandae kufungasha virago?

Naona Azam media wanazidi kuja kwa kasi leo hii wamezindua minara ya bilioni 50 mikoa 21

Baada ya Dish wamekuja na vya Antenna hawa jamaa wapo vizuri sana naona kwa sasa Wachina wa Startimes wajiandae kisaikolojia tu maana sidhani kama kuna mtu timamu atatumia vile vidubwashwa vyao

Kongole Azam media sasa huku kwa vya Antenna ndo mnaenda kusepa na nyomi ya kijiji
Tusaidie kuielewa hiyo teknolojia mpya na faida zake
 
Jamii forums ni sehemu ndogo sana ya maisha yetu. Hiko kisimbuzi cha Star times mnavyokisakama kila siku humu mpaka juzi nikaona takwimu ndio kinachoongoza kwa mbali sana kuwa na watumiaji wengi Tanzania.
Mi mwenyewe natumia Startimes ukitoa mambo ya ligi ya bongo sioni cha maana Azam.

Bundesiliga, CAFCL na CAFCC huwa nacheki kwa matangazo ya kiingereza na picha za HD kabisa.

Japo kila king'amuzi na ubora wake na mapungufu yake.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Jamiiforums ni sehemu ndogo sana ya maisha yetu. Hiko kisimbuzi cha Star times mnavyokisakama kila siku humu mpaka juzi nikaona takwimu ndio kinachoongoza kwa mbali sana kuwa na watumiaji wengi Tanzania.
Kilichowabeba ni minara ya tbc wanayotumia pia kuhama analog to digital walipewa tenda wao
 
Ukitoa DSTV king'amuzi kinachofuata kwa ubora ni startimes, kwa upande wa football wako vizuri, series za kizungu, kihindi kichina, kikorea na kituruki wako vizuri kwa upande wa Tamthilia zilizotafsiriwa ingawa mimi sio mpenzi nazo ila The Brothers hainipiti, kwa upande wa michuano ya kimataifa star times inaonyesha ligi nyingi zaidi ya Azam huku mpaka Ronaldo anaonekana,kwa upande wa soka la Africa, wanaonyesha michuano yote inayosimamiwa na caf, Tunaangalia ligi ya kenya, tunaangalia ligi ya Uganda na kwa upande wa Tanzania wameanza na champioshp,
Hamna kitu pale
 
Bilioni 50 kusambaza antena? Badala ya kulipia EPL??

Azam bado sana...hawana channels za maana kabisa ...hata channels za South Africa Tu hawana hata moja
Azam ni levo nyingine kiongozi
 
Usifananishe Startimes Na Vitu Vya Hovyo Hovyo Tshs 15000/= Unaona Mwezi Mzima
Kifurushi Kikiisha Local Channels Zote Bure, Sasa Azam Hakuna Ikiisha Wanazima
Azam local ni bure bado channel kama 30 za dini ni bure
 
Back
Top Bottom