Botswana imemuomba Rais wa DR Congo, Joseph Kabila kuachia madaraka haraka ili kuepusha kumwaga damu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Botswana imemuomba Rais wa DR Congo, Joseph Kabila kuachia madaraka haraka ili kuepusha kumwaga damu

Serikali hiyo imejitosa kumshawishi Rais Kabila aachie ngazi ili kuheshimu Katiba na zaidi sana, kukubaliana na matakwa ya wananchi wengi. Taarifa ya serikali hiyo imeeleza kuwepo kwa kila dalili kuwa Congo itatumbukia katika machafuko na vita vitakavyosababisha vifo vya raia wasiokuwa na hatia

Kabila alichukua urais mwaka 2001 baadaya mauaji ya baba yake na alitarajiwa kuachia madaraka mwaka 2016 baada ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi kuisha. Hata hivyo, amekuwa akitoa changamoto mbalimbali ambazo zimezuia Shirika la Uchaguzi kufanya uchaguzi wa rais mwingine

Tarehe mpya ya Desemba 23, 2018 imewekwa kwa ajili ya Uchaguzi lakini wafuasi wa upinzani wanataka Kabila kutangaza kuwa hatatafuta kubadili Katiba ya nchi ili kumfanya aendelee kukaa madarakani.

index.jpeg

index.jpeg

DRC ni mwanachama wa SADC. Kwa nini wanaruhusu mwanachama wao kwa makusudi kuendelea kuvunja Katiba ya nchi yake na haki za wananchi wake? Ni kama wanamtia moyo kuendeleza hayo! SADC inapaswa kusimamia misingi yake.
 
Botswana imemuomba Rais wa DR Congo, Joseph Kabila kuachia madaraka haraka ili kuepusha kumwaga damu

Serikali hiyo imejitosa kumshawishi Rais Kabila aachie ngazi ili kuheshimu Katiba na zaidi sana, kukubaliana na matakwa ya wananchi wengi. Taarifa ya serikali hiyo imeeleza kuwepo kwa kila dalili kuwa Congo itatumbukia katika machafuko na vita vitakavyosababisha vifo vya raia wasiokuwa na hatia

Kabila alichukua urais mwaka 2001 baadaya mauaji ya baba yake na alitarajiwa kuachia madaraka mwaka 2016 baada ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi kuisha. Hata hivyo, amekuwa akitoa changamoto mbalimbali ambazo zimezuia Shirika la Uchaguzi kufanya uchaguzi wa rais mwingine

Tarehe mpya ya Desemba 23, 2018 imewekwa kwa ajili ya Uchaguzi lakini wafuasi wa upinzani wanataka Kabila kutangaza kuwa hatatafuta kubadili Katiba ya nchi ili kumfanya aendelee kukaa madarakani.
View attachment 701969

View attachment 701970
Yaani kaliungia madarakani hakana mavuzi, kamekaa hadi kameota na mvi kakiwa huko madarakani lakini bado kanataka katembelee fimbo na kwenda kaburini kakiwa madarakani.
 
Back
Top Bottom