KENYATTA: Nilikuwa tayari kuachia madaraka ya Urais ili kuepusha umwagikaji wa damu 2017

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,453
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema alikuwa tayari kuachia madaraka ya Urais baada ya Mahakama Kuu kuufuta ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2017, angefanya hivyo ili kuzuia umwagikaji wa damu lakini Naibu wake, William Ruto alimshawishi kutofanya hivyo.

Mahakama iliagiza kurudiwa kwa uchaguzo huo baada ya kesi kufunguliwa na Raila Odinga na muungano wake wa kisiasa wa NASA.

“Nilikuwa tayari kuweka maslahi ya nchi mbele na kuokoa nchi dhidi ya umwagikaji wa damu. Haya madaraka tuliyo nayo hayana thamani sana kushinda maisha ya watu. Ndio! Nilikuwa nimeamua kuachia madaraka na kuokoa nchi,” anasema.

Ametoa kauli hiyo baada ya sauti kusambaa mitandaoni Ruto akisikika akisema alitamani kumpiga kofi Kenyatta kwa kutaka kuchukua maamuzi hayo

“Iwapo wangenipiga kofi kwa sababu ya madaraka, ningewapa shavu la pili na wapige kofi lingine. Ndio, nilitaka kuachia madaraka na niende Ichaweri kwa sababu nisingeweza kulinganisha madaraka na umwagikagi wa damu.”

Ichaweri ni Kijijini kwao Uhuru Kenyatta, kipo eneo la Gatundu Kusini, Kaunti ya Kiambu, kilomita 50 kutoka Nairobi.

Source: tuko


----------------------

” I Almost Quit for the Sake of Peace” Uhuru Speaks On Ruto Alleged Slap Remarks

President Uhuru Kenyatta has responded to Ruto’s alleged slap remarks making it clear he was ready to let power go than lead the country into bloodshed. According to Uhuru, he was ready to ensure peace prevailed in the country and that’s why he said he was ready to handover power to Raila Odinga.

The president is clear he wouldn’t bother handing over power to Raila Odinga is that would have brought peace in the country. Uhuru Kenyatta is clear he is a leader who is not power angry rather he only wants peace for this country.

The president is clear that at the moment, he is ready to leave government and those who accused him of trying to extend power through BBI are now confusing themselves. According to Uhuru Kenyatta, he would have given the other chick had Ruto slapped him as alleged.

President Uhuru Kenyatta is clear he is a peace loving leader and he wouldn’t want to see the country degenerate into war just because of politics. Uhuru’s revelation has exposed Raila Odinga and William Ruto as power angry leaders who would not let power go.
 
Uongo mtupu,alimuua mpk yule boss wa IEBC kwa ajili ya Utamu wa urais afu Leo anajiongelesha upumbavu.
Msando yule jamaa wakati wanamzika walimzika kwa milae za kijaluo walimzika na mkuki yule. Wote waliohisika kuchukua maisha yake hawatabaki salama Uhuru na Ruto saivi ni chui na paka
 
Msando yule jamaa wakati wanamzika walimzika kwa milae za kijaluo walimzika na mkuki yule. Wote waliohisika kuchukua maisha yake hawatabaki salama Uhuru na Ruto saivi ni chui na paka
Sahihi kabisa mkuu,afu leo anazuga eti alikua tayari kuachia urais.
 
Uhuru ni muungwana sana. Hilo alilosema la uchaguzi wa 2017 si mara ya kwanza. Nakumbuka ulipokaribia uchaguzi wa 2012 kulipotokea mvuano wa nani agombee alisema wazi yeye hata akipewa ubalozi ni sawa tu, tena alisema angependa apewe ubalozi kuwakilisha Nchi Tanzania. Si hivyo tu, alifikia mpaka kufanya makubaliano tena ya maandishi na Musalia Mudavadi awe mgombea lakini wengi katika chama wakapinga sana ikabidi abebe kijiti
Sahihi kabisa mkuu,afu leo anazuga eti alikua tayari kuachia urais.
 
Eti amesemaje ?
images.jpeg
 
Back
Top Bottom