BOT yawafukuza waliorejeshwa na mahakama

BOT yawafukuza waliorejeshwa na mahakama

Yule Mjita naye anajidai kujua mno, wacha wazuiliwe tuone watatokea wapi? Wanajidai kwenda kichwa kichwa bila ushauri wa kisheria? Eti mpaka vikakodi na mpicha piga wa mwananchi akawa anavipiga picha tangu vinatoka nyumbani mpaka vinaingia kwenye gate la BOT!!
 
Baada ya mahakama kuona they received unfair dismissal common sense would have been asking BoT iwalipe loss of income, paying other additional financial compensation for damages caused to ppl or families and a hefty government financial penalty to deter others from repeating similar actions.

Lakini kuamuru watu warudi kazini kama mwajiri awataki was just a pathetic ruling.
Hivi mwajiri anaweza kuamua tu kutoka usingizi na kuwakataa wafanyakazi fulani ?
 
Kwa mazingira ya sasa hawana uwezo wa kufanya kaz BOT. Mazingira yamebaditika sana.
Cha msingi wawasitaafishe wapewe chao kaz kwisha
 
Tatizo suala hili linawekewa siasa sana. Kimsingi, baada ya ile hukumu wale wafanyakazi hawakupaswa kurejea kazini kama walivyofanya. Walipaswa kuomba mahakamani utekelezwaji wa hukumu yao iliyotolewa. Kama wangeomba kuitekeleza kwa njia ya kurejea kazini na BOT kugoma, sheria ingechukua mkondo wake. Walikosea kisheria na kihalisia kwenda kuripoti kazini bila ya kuomba utekelezaji wa hukumu yao kimahakama.

Unadhani hawakulijua hilo? ila kitaa kumekuwa kugumu wameona waende hivyo hivyo kitajulikana mbele kwa mbele, chezea kufanya kazi BOT wewe
 
Wanasheria naombeni msaada na mm kwenye hili nifanyaje?
Mahakama imeamuru nirudishwe kazini ktk bank moja hapa mjini na kulipwa malimbikizo yangu yote ya mishahara tangia nifukuzwe kazi kama miaka minne hivi iliyo pita...
Je wakisha nilipa, nini kifanyike ili nirudi kazini? Niende tu mwenyewe au mpaka waniite?
 
Nilichogundua katika sakata hili ni kuwa walioshinda kesi wanatumia media kushikiniza wao kurudishwa kazini...
Hukumu ilisema kuwa walikuwa dismissed unfairly so walitakiwa wawe reinstated to their jobs so hawa jamaa wakaita waandishi wa habari na kuanza safari ya kwenda BOT this was technical mistake kwani walichotakiwa kufanya ni kuomba execution of court order ili mwajiri awarudishe kazini kisheria ingawa mwajiri ana haki ya kuwalipa maslahi yao na kumalizana nao bila kuwarudisha kazini...
So ishu ni siasa imeingia hapo
 
Wanasheria naombeni msaada na mm kwenye hili nifanyaje?
Mahakama imeamuru nirudishwe kazini ktk bank moja hapa mjini na kulipwa malimbikizo yangu yote ya mishahara tangia nifukuzwe kazi kama miaka minne hivi iliyo pita...
Je wakisha nilipa, nini kifanyike ili nirudi kazini? Niende tu mwenyewe au mpaka waniite?
Si lazima wakurudishe kazini wanaweza wakaomba mahakama iamue wakulipe haki zako ikiwa ni pamoja na mishahara ya miezi 12 na stahiki nyingine za kawaida biashara ikaishia hapo.
 
Tatizo suala hili linawekewa siasa sana. Kimsingi, baada ya ile hukumu wale wafanyakazi hawakupaswa kurejea kazini kama walivyofanya. Walipaswa kuomba mahakamani utekelezwaji wa hukumu yao iliyotolewa. Kama wangeomba kuitekeleza kwa njia ya kurejea kazini na BOT kugoma, sheria ingechukua mkondo wake. Walikosea kisheria na kihalisia kwenda kuripoti kazini bila ya kuomba utekelezaji wa hukumu yao kimahakama.
Mkuu sidhani kama Ushafanya Utafiti wowote ule hadi ujaze maneno humu na kuanza kukosoa hao wafanyakazi... kumbuka kama hujafanya research yeyote jitambue kuwa huna haki ya kuzungumzia kitu.... Hii nakupa tahadhari tu.... kwa leo na siku za baadae.... usichukue kitu juu juu tu
 
Mtu yupo tayari kuteseka miaka 40 akiwa ameajiriwa lakini hayupo tayari kuteseka miaka 3 akiwa anajiimarisha katika biashara yake. Ndiyo maana tukipata janga kazini kinachofuata ni stroke, ndoa kuvunjika na kujifia.
 
Hivi kweli kesi ya Labour (Kazi),inakaa mahakamani miaka 23? Ni criminal Case? Hivi mifumo ya mahakama IPO kuchelewesha kesi au kutenda haki; hata km caseload hapana hii imezidi.
 
Sababu iliyotajwa ni kuwa hawatambuliwi na BOT .

" BOT hawataki kutupokea , wametufukuza ka mbwa "

Taarifa zaidi zinadokeza kwamba jumla ya waliorejeshwa na mahakama walikuwa 31 , lakini 11 kati yao walishafariki dunia kutokana matatizo ya msongo wa mawazo uliosababishwa na kufukuzwa kazi .

Chanzo - MwanaHalisi.

Mungu wabariki wahanga hawa .
Hii ni Mwanahalisi ipi. ????? Wajameni. Mwanahalisi ile waliokuwa wakisema Lowasa ni fisadi papa. Hasafishiki na wala hafai kuwa rais wa Tanzania ? Mwanahalisi lile la Kubenea au ipi. Mzee wa elimu ya hapa na pale.
 
Back
Top Bottom