BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,015
Date::3/3/2009
BoT yabana wanaotorosha mabilioni ya fedha nje
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi
BoT yabana wanaotorosha mabilioni ya fedha nje
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi
BENKI Kuu Tanzania (BoT) imeanza utekelezaji wa taratibu mpya za uendeshaji Maduka ya Kubadilishia Fedha (Bureau de Change), ambazo pamoja na nyingine zinazuia uuzaji wa fedha za kigeni zenye kiwango cha zaidi sawa na dola 10,000 za Marekani, kwa wasafiri waendao nje ya nchi.
Taratibu hizo za BoT, ambazo zimo chini ya Sheria ya Kubadlisha Fedha za Kigeni ya mwaka 1992, zimekuja wakati serikali imekuwa ikipambana na ufisadi ikiwa na pamoja na kuanzisha Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu (Anti- Money Loundering) na Kitengo cha Kuangalia Mzunguuko wa Fedha (Financial Intelligency Unit-FIU), zote za mwaka 2007.
Kwa mujibu wa taratibu hizo, ambazo pia zilijadiliwa katika mkutano kati ya BoT na maofisa watendaji wakuu wa benki na taasisi za fedha hivi karibuni, zinasisitiza kwamba, wenye maduka hayo pia hawapaswi kuuza fedha za kigeni zenye thamani zaidi sawa na Dola 10,000 za Kimarekani (sawa na Sh13,1 milioni za Tanzania) kwa madhumuni yoyote yale.
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema uamuzi huo umeangalia maslahi ya taifa.
Kwa mujibu wa Gavana Ndulu, taratibu hizo ni nzuri kwani zimezingatia maoni ya wadau mbalimbali, vikiwemo vyombo vya habari.
Alisema kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka kwa wadau ambayo yalikuwa yakisisitiza umuhimu wa kuangalia udhibiti wa ubadilishaji fedha za kigeni.
"Ni uamuzi ambao umezingatia maoni ya wadau, ninyi wenyewe (waandishi) na wadau wengine... nafikiri hauna tatizo lolote lilile," alifafanua Profesa Ndulu.
Gavana huyo alisema BoT pia iliunda timu maalumu ya wataalamu kuangalia taratibu hizo.
"Lengo letu ni kuongeza ufanisi, si kufuta maduka ya fedha wala hakuna mpango huo," alisema.
Kifungu cha 18 cha sehemu ya tatu ya taratibu za sheria hiyo ya mwaka 1992, kinapiga marufuku uuzwaji fedha za kigeni zenye thamani inayozidi sawa na dola 10,000, kwa madhumuni yoyote yale.
Pia kifungu cha 22 (1) Sehemu ya Nne kinasisitiza marufuku ya maduka hayo kuuza hundi za kusafiria (Traveler's Cheques) au fedha taslimu za kigeni zinazozidi kiwango cha Dola 10,000 za Kimarekani.
Kifungu cha 21 kinazuia mtu asiye mkazi kuuziwa fedha za kigeni hadi itakapothibitika fedha hizo zilipatikana nchini kwa kuuza fedha za kigeni au zimepatikana kwa njia nyingine za kisheria zinazokubalika, wakati kifungu cha 22 (3) kinazuia uuzwaji wa fedha za kigeni kwa mtu asiye mkazi wa Tanzania na kuweka taratibu za kufuata kwa watu wa aina hiyo.
Katika Sehemu ya Tano ya kifungu cha 23, imeelezwa kuwa mzunguko wote wa fedha unapaswa kuwa siri.
Utaratibu huo unakwenda pamoja na ule ambao umekwishatangazwa na BoT, ambao unahusu mzunguko wa fedha za ndani hasa akaunti za Benki Kuu.
Katima utaratibu huo hundi zote ambazo zina thamani ya zaidi ya Sh10 milioni, hazitaruhusiwa kupita katika mfumo wa Ubadilishanaji Hundi (clearing house) ulio Benki Kuu Dar es Salaam pamoja na matawi yake yote nchini.
Katika utaratibu huo, malipo yoyote yanayozidi Sh10 milioni yatafanyika kwa kupitia mfumo wa malipo wa taifa uitwao Tanzania Interbank Settlement System (TISS).
Hata hivyo, hundi za serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh10 milioni, zitaendelea kupokelewa kama kawaida katika mabenki ya biashara na kupitishwa kwenye mfumo huo wa ubadilishanaji mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.
Uamuzi huo wa BoT kudhibiti biashara ya fedha za kigeni, umekosolewa na baadhi ya wenye maduka ya fedha wakisema umekuwa ukiwaathiri kibiashara.
'Wanafikiri sisi tunatumika kusafirisha fedha kuzificha nje, wakati mafisadi ni wao ambao baadhi yao wapo serikalini," alisema mmiliki mmoja kwa sharti la kutotajwa jina.
Katika siku za karibuni nchi imegubikwa na tuhuma nzito za ufisadi, ikiwemo baadhi ya watu kutorosha fedha nje na kwenda kuzificha nje.
Miongoni mwa tuhuma hizo ni dhidi ya baadhi ya makampuni tisa yanayotuhumiwa kuiba Sh42 bilioni na kuzisafirisha nje katika kashfa ya wizi wizi wa zaidi ya Sh133 bilioni zilizowekwa kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).