BoT yabana wanaotorosha mabilioni ya fedha nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BoT yabana wanaotorosha mabilioni ya fedha nje

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Mar 3, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Mar 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,461
  Likes Received: 81,711
  Trophy Points: 280
  Date::3/3/2009
  BoT yabana wanaotorosha mabilioni ya fedha nje

  Na Ramadhan Semtawa
  Mwananchi


  BENKI Kuu Tanzania (BoT) imeanza utekelezaji wa taratibu mpya za uendeshaji Maduka ya Kubadilishia Fedha (Bureau de Change), ambazo pamoja na nyingine zinazuia uuzaji wa fedha za kigeni zenye kiwango cha zaidi sawa na dola 10,000 za Marekani, kwa wasafiri waendao nje ya nchi.

  Taratibu hizo za BoT, ambazo zimo chini ya Sheria ya Kubadlisha Fedha za Kigeni ya mwaka 1992, zimekuja wakati serikali imekuwa ikipambana na ufisadi ikiwa na pamoja na kuanzisha Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu (Anti- Money Loundering) na Kitengo cha Kuangalia Mzunguuko wa Fedha (Financial Intelligency Unit-FIU), zote za mwaka 2007.

  Kwa mujibu wa taratibu hizo, ambazo pia zilijadiliwa katika mkutano kati ya BoT na maofisa watendaji wakuu wa benki na taasisi za fedha hivi karibuni, zinasisitiza kwamba, wenye maduka hayo pia hawapaswi kuuza fedha za kigeni zenye thamani zaidi sawa na Dola 10,000 za Kimarekani (sawa na Sh13,1 milioni za Tanzania) kwa madhumuni yoyote yale.

  Alipoulizwa kuhusu suala hilo, gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu alisema uamuzi huo umeangalia maslahi ya taifa.


  Kwa mujibu wa Gavana Ndulu, taratibu hizo ni nzuri kwani zimezingatia maoni ya wadau mbalimbali, vikiwemo vyombo vya habari.

  Alisema kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka kwa wadau ambayo yalikuwa yakisisitiza umuhimu wa kuangalia udhibiti wa ubadilishaji fedha za kigeni.

  "Ni uamuzi ambao umezingatia maoni ya wadau, ninyi wenyewe (waandishi) na wadau wengine... nafikiri hauna tatizo lolote lilile," alifafanua Profesa Ndulu.

  Gavana huyo alisema BoT pia iliunda timu maalumu ya wataalamu kuangalia taratibu hizo.

  "Lengo letu ni kuongeza ufanisi, si kufuta maduka ya fedha wala hakuna mpango huo," alisema.

  Kifungu cha 18 cha sehemu ya tatu ya taratibu za sheria hiyo ya mwaka 1992, kinapiga marufuku uuzwaji fedha za kigeni zenye thamani inayozidi sawa na dola 10,000, kwa madhumuni yoyote yale.

  Pia kifungu cha 22 (1) Sehemu ya Nne kinasisitiza marufuku ya maduka hayo kuuza hundi za kusafiria (Traveler's Cheques) au fedha taslimu za kigeni zinazozidi kiwango cha Dola 10,000 za Kimarekani.

  Kifungu cha 21 kinazuia mtu asiye mkazi kuuziwa fedha za kigeni hadi itakapothibitika fedha hizo zilipatikana nchini kwa kuuza fedha za kigeni au zimepatikana kwa njia nyingine za kisheria zinazokubalika, wakati kifungu cha 22 (3) kinazuia uuzwaji wa fedha za kigeni kwa mtu asiye mkazi wa Tanzania na kuweka taratibu za kufuata kwa watu wa aina hiyo.

  Katika Sehemu ya Tano ya kifungu cha 23, imeelezwa kuwa mzunguko wote wa fedha unapaswa kuwa siri.

  Utaratibu huo unakwenda pamoja na ule ambao umekwishatangazwa na BoT, ambao unahusu mzunguko wa fedha za ndani hasa akaunti za Benki Kuu.

  Katima utaratibu huo hundi zote ambazo zina thamani ya zaidi ya Sh10 milioni, hazitaruhusiwa kupita katika mfumo wa Ubadilishanaji Hundi (clearing house) ulio Benki Kuu Dar es Salaam pamoja na matawi yake yote nchini.

  Katika utaratibu huo, malipo yoyote yanayozidi Sh10 milioni yatafanyika kwa kupitia mfumo wa malipo wa taifa uitwao ‘Tanzania Interbank Settlement System (TISS)’.

  Hata hivyo, hundi za serikali zenye thamani ya zaidi ya Sh10 milioni, zitaendelea kupokelewa kama kawaida katika mabenki ya biashara na kupitishwa kwenye mfumo huo wa ubadilishanaji mpaka hapo itakapotangazwa vinginevyo.

  Uamuzi huo wa BoT kudhibiti biashara ya fedha za kigeni, umekosolewa na baadhi ya wenye maduka ya fedha wakisema umekuwa ukiwaathiri kibiashara.

  'Wanafikiri sisi tunatumika kusafirisha fedha kuzificha nje, wakati mafisadi ni wao ambao baadhi yao wapo serikalini," alisema mmiliki mmoja kwa sharti la kutotajwa jina.

  Katika siku za karibuni nchi imegubikwa na tuhuma nzito za ufisadi, ikiwemo baadhi ya watu kutorosha fedha nje na kwenda kuzificha nje.

  Miongoni mwa tuhuma hizo ni dhidi ya baadhi ya makampuni tisa yanayotuhumiwa kuiba Sh42 bilioni na kuzisafirisha nje katika kashfa ya wizi wizi wa zaidi ya Sh133 bilioni zilizowekwa kwenye Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA).
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  Mar 3, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huu ni ukiritimba mwengine ,dola 10,000/- ? ni aibu kubwa sana bora wasingetangaza,nini dola elfu kumi ,hebu watuambie 5* hotel hapa Tanzania kwa siku ni kiasi gani ?

  Huu ni udikteta katika sura au rangi nyingine ,ila nawapa hongera Utawala wa Sultani CCM maana upinzani unazidi kusafishiwa njia , wandugu natangaza moja kwa moja kuwa Upinzani ukichukua Nchi nakumuangusha Sultani CCM basi maduka ya fedha yataruhusiwa mara moja kubadilisha kiasi chochote cha fedha wanachotaka ,hakuna udhibiti ambao serikali utajishughulisha na maduka ya binafsi.

  Maana benki inauza na kununua na kujipangia viwango vya ununuzi hivyo wenye maduka wanarudi benki kununua au kuuza fedha zao hapo.

  Hii ni janja ya kuwarahisishia mafisadi wanufaike wao tu na fedha zilizoko benki ,maana wao ni ruhusa ,ukoo wa Kisulatni ukisafiri kwenda nje unachukua kiasi watakacho lakini mfanya biashara haruhusiwi maana gari second hand hujainunua huko japan na kuisafirisha wala hujailipia ushuru na gharama za bandari.

  Huku ni kuwabana wafanya biashara wadogowadogo ambao hutegemea kuondoka na dola zisizopungua 50000/- ili anunue mzigo wa kuleta Tanzania ,hii sheria sijui kama kule Nchini Zanzibar wataikubali ,ngoja tuone.

  Hawa Masultani wana choyo tu hawana jingine, watu wakishakuwa mafisadi basi watafisadi kila kitu.
   
 3. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2009
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,548
  Likes Received: 1,306
  Trophy Points: 280

  Mwiba taratibu ndugu yangu,

  Leo hii nenda US na zaidi ya 10,000 Cash uone utakavyosumbuliwa point of entry utajuta kwa nini umechukua kiasi kikubwa(kidogo) hivyo cha fedha.

  Kikubwa hapa ni taratibu za fedha, Je hizo 10,000plus ulikuwa nazo wapi siku zote?????? kama zilikua bank kwa nini usinunue hela za kigeni kwenye bank yako?????

  Kama unasafiri sio lazima uende na cash, unaweza kutumia travelers cheque, unaweza kufanya net banking, credit cards n.k.

  Kama umefanya booking ya hotel kule unakoenda unaweza kulipia kabla hujasafiri na ndio maana wanatoa details zote wakati unapofanya booking, so
  hakuna justification ya kutembea na maburungutu ya hela kwenye soksi na bag.

  wewe pia umekuwa ukilalamika Tsh kuyumba against dola, hatua zikichukuliwa unalalamika watanzania bwana........ ..... ndivyo walivyo
   
 4. ChaMtuMavi

  ChaMtuMavi JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 333
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mwiba usiniaibishe, wewe unazo hizo $10,000? au ni mwananchi gani anazo hizo dola kama siyo mafisadi ambao waliachiwa huru kucheza michezo michafu na pesa za walalahoi.
  BOT ku-control dola au pesa za kigeni kwa maslahi ya taifa ni vyema kabisa, cha msingi ni kujiuliza je BOT wamejiandaa kikamilifu na operation hii au ndo wataanza ukiritimba na ufisadi mwingine?

  Ni dhahiri nchi i-control pesa za kigeni ndani ya nchi. Mimi binafsi naiunga mkono hii operation. Kwani wanaomiliki hizo station za kuuza pesa ni nani? huenda ni mafisadi hao hao, wametumia pesa za walala hoi kendelea kujinufaisha na kusafirisha pesa zetu.
  BOT isafishwe na ufisadi wake kwanza, halafu iwe na taratibu muafaka wa manunuzi ya pesa za kigeni nchini.
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Mar 4, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mwiba ndiyo zake, Mnyamwezi wa Zanzibar.
  Nina rafiki yangu yuko BoT aliniambia kuwa hapo kwao BoT kimeanzishwa kitengo kipya kabisa kinachodeal na mambo haya. Kama sikosei wameanza mwezi wa 1 mwaka huu. Wamepewa pesa na vifaa na hata ufundi kutoka USA. Hivyo hiki kitu wala si cha Tanzania ila tumelazimishwa. Dunia hii sasa hivi USA wanalazimisha nchi nyingi kuwa na hii system. Labda kwetu itakuwa safi tu maana mafisadi walau hawataiba sana kwa kuogopa kunaswa mapema.
   
 6. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Ni Lazima ku control fedha za kigeni ktk nchi yako.

  Mfano South Africa, maduka yote ya kuuza na kubadilisha fedha za Kigeni yapo connected na Central Bank yao. Yaani Central Bank yao inaona kila cku Duka fulani wamebadilisha kiasi gani cha fedha za Kigeni na hivyo basi central bank yao wakati wowte ina Data kuwa kwa sasa tuna kiasi fulani cha USD au EURO au Yen zipo ktk nchi yetu,

  Hapa kwetu sasa Mungu tusaidie, hebu waulize BOT jana ni kiasi gani cha fedha za Kigeni kimeingia nchi au kimetoka ............Upumbavu mtupu na hivyo basi kuanzisha kitu kama hiki hapa TZ ni moja wapo ya ku control fedha za kigeni.
   
 7. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hiki kitengo kinaitwa FINANCIAL INTELLIGENCE UNIT ambacho kimeanzishwa chini ya UN Resolution katika kupambana na ugaidi. Hii inaendana pamoja na kupitishwa kwa sheria ya MONEY LAUNDARING ambayo serikali ilipitisha kwa shingo upande kutokana na pressure kubwa kutoka kwa Uncle Sam...

  All in all ingawa itakuwa kikwezo kwa baadhi ya watu lakini kwa ujumla ina manufaa makubwa kwa nchi yoyote ile kiuchumi na kiusalama...

  omarilyas
   
 8. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Hapa sijaelewa kidogo, inakuwaje ukienda badili katika makuka tofauti ya kubadilishia pesa?, Hata hivyo naunga mkono kutembea na pesa nyingi cash ni risk sana.
   
 9. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili mbona siyo jambo jipya? Tangu Serikali iruhusu matumiszi ya fedha za kigeni nchini, mwaka 1992. Bank of Tanzania ambayo yenye jumkumu la kusimamia shughuli za fedha ilitoa FOREING EXCHANGE REGULATIONS 1999 kwa Bureau De Change kuweza kufanya shughuli za Biashara na wakati huo ilikuwa ni ngumu zaidi kwa sababu kima cha mwisho kuweza kununua fedha ilikuwa si zaidi ya US$ 9,999 na mteja aambatanishe nakala za pasi ya kusafiria pamoja na ticket ili aweze kununua fedha za kigeni hii ni kwa Watanzania tu. Na ilikuwa mteja akitaka dola moja tu ya marekani ilibidi atoe hiyo nakala ya pasi ya kusafiria na ticket. Hivi sasa Bank of Tanzania wametoa FOREING EXCHANGE REGULATIONS 2008, kwa Bureau De Change na wametoa fursa zaidi za kuwezesha wateja kununua fedha za kigeni ambacho ni US$ 10,000 kwa mteja mmoja kwa mara moja akiwa na nakala za pasi ya kusafiria na ticket au documents nyengine kama invoice ya Hospital kama anakwenda kutibiwa nje au Invoice ya Shule kama anajilipia masomo nje. Lakini pia wameongeza kima cha chini cha kununua fedha bila ya kuwa na nyaraka zote hizo ambacho ni US$ 2,000 tu unachotakiwa hapo ni kuonyesha kitambulisho chako cha kazi au hata kadi ya kura inakubalika. Nafikiri kwa hili wamepiga hatua pengine huko tunakokwenda wanaweza siku moja ikawa mteja anaweza kujinunulia fedha mpaka US$ 10,000 kwa kutumia kitambulisho tu.
   
 10. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hili mbona siyo jambo jipya? Tangu Serikali iruhusu matumiszi ya fedha za kigeni nchini, mwaka 1992. Bank of Tanzania ambayo yenye jumkumu la kusimamia shughuli za fedha ilitoa FOREING EXCHANGE REGULATIONS 1999 kwa Bureau De Change kuweza kufanya shughuli za Biashara na wakati huo ilikuwa ni ngumu zaidi kwa sababu kima cha mwisho kuweza kununua fedha ilikuwa si zaidi ya US$ 9,999 na mteja aambatanishe nakala za pasi ya kusafiria pamoja na ticket ili aweze kununua fedha za kigeni hii ni kwa Watanzania tu. Na ilikuwa mteja akitaka dola moja tu ya marekani ilibidi atoe hiyo nakala ya pasi ya kusafiria na ticket. Hivi sasa Bank of Tanzania wametoa FOREING EXCHANGE REGULATIONS 2008, kwa Bureau De Change na wametoa fursa zaidi za kuwezesha wateja kununua fedha za kigeni ambacho si zaidi US$ 10,000 kwa mteja mmoja kwa mara moja akiwa na nakala za pasi ya kusafiria na ticket au documents nyengine kama invoice ya Hospital kama anakwenda kutibiwa nje au Invoice ya Shule kama anajilipia masomo nje. Lakini pia wameongeza kima cha chini cha kununua fedha bila ya kuwa na nyaraka zote hizo ambacho ni US$ 2,000 tu unachotakiwa hapo ni kuonyesha kitambulisho chako cha kazi au hata kadi ya kura inakubalika. Nafikiri kwa hili wamepiga hatua pengine huko tunakokwenda wanaweza siku moja ikawa mteja anaweza kujinunulia fedha mpaka US$ 10,000 kwa kutumia kitambulisho tu.
   
 11. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Swali zuri.
  Unless wana networked id system among all exchange bureaus (which,I'll bet,they don't) ili kuweza kudhibiti mtu mmoja kuchukua zaidi ya kiasi kilichotajwa,watakuwa wanatupotezea muda kusikiliza mikakati yao bomu.Na kama wanayo hiyo system,what will stop one from sending a friend second time round?

  Halafu hawajatuambia ni ndani ya muda gani mtu hataruhusiwa kutoa zaidi ya kiasi hicho.Is it within 24 hours?A week?A lifetime?
   
 12. M

  Mkodoleaji JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2009
  Joined: Apr 27, 2008
  Messages: 454
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hiki ni kichekesho kingine tena!!! Yaani baada ya kumaliza kufislisi nchi kwa njia mbalimbali na kukimbizia mihela nje ndipo wanakuja na visheria na vijikanuni uchwara?? Hivi wakati akina Lukaza et al wanahamisha hela bila kumsahau kubwa lao JEETU Patel hizo sheria zilikuwa hazipo??? Walikua wanafumba macho maana fika BOT walijua kila deal those times!!!!

  Na kwa Tz hii ni danganya toto tu ili umma uone kuwa kuna ka effort kanafanyika kuzuia hela haramu!!!! Wenye hela zao watapitisha tu. Money is power!!! Watabuni mbinu nyingine kama ambavyo vinara wa madawa ya kulevya wanafanya!!!! Yangu macho!!!

  Nchi inatawaliwa kifisadi na mambo yake ni ya kifisadi tu. Hakuna badiliko lolote la sheria au kanunu litakuwa effective kama the rotten system haijabadilika!!!!!! Wewe na mimi tuna wajibu wa kuibadilisha system hiyo. Poor the citizens of Tanzania.
   
 14. Kuhani

  Kuhani JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2009
  Joined: Apr 2, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Elusive,

  Unasema hili si jambo jipya lakini kilichoandikwa humo kwenye taarifa kwa kweli ni elusive sana kwangu.

  Wanasema:
  Sasa, bwana/bibi Elusive, hebu tusaidiane. Benki kuu imetangaza nini hapa, utekelezaji wa taratibu mpya au wanasema wataanza kutekeleza taratibu za zamani? Kama ni taratibu mpya basi gazeti limechemka maana limesema taratibu hizi zipo kwenye sheria ya 1992, na wakatoa vipengele.

  Lakini kama ni taratibu za zamani basi Ndullu ilibidi aeleze au aulizwe inakuwaje, utaanzaje leo kutekeleza sheria ya miaka kumi na saba vitabuni?

  Kwa hiyo somewhere between the mwandishi and the governor kuna mmoja hapa hajui anachokifanya au anajua lakini hajui anachokiongea, au hajui vyote viwili, anachokifanya wala anachokiongea au wote wawili hawajui yote mawili, wanayoyafanya wala wanayoyaongea.

  Gavana au kiongozi huwezi kuzinduka na kukurupuka kutoka usingizini katika utekelezaji wa sheria ukasema kuanzia leo tunaanza kufuatilia sheria fulani. Unless wewe ni "new sheriff in town." Only a new sheriff in town ndio anaweza kutangaza kwamba kuanzia leo ninaanza kutekeleza sheria ya kupiga marufuku wizi. An old dog sheriff akitangaza hivyo ataambiwa ulikuwa wapi siku zote, leo ndio umepata dini? Jiuzulu!
   
 15. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Suki hapa inaonekana kunatatizo kubwa. Ninahakika hawakonetworked wenye maduka ya kubadili pesa bongo. Hii sera inamapungufu nafikiri inahitaji maboresho.
   
 16. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa nini wengine huwa wanakuja kusoma na kuruka maelezo yaliyofuatwa?

  Nimesema nyuma kuwa "Rafiki yangu kaniambia kuwa wanafungua kitengo kipya kushughulikia haya mambo. Watakuwa chini ya BoT ila mambo yao yatakuwa hayana uhusiano wa karibu na BoT. Watakuwa na system zao, Server zao, email zao, www zao...... Nafikiri hii system itaunganishwa hadi sehemu zote zenye kuingiza fedha za kigeni. Hili limepewa gia na USA. Nafikiri hawa ndiyo wanatakuwa hata wanalipia".

  Kwa maana hiyo hata kama hii ilikuwepo, kwa sasa itaanza ikiwa coputerised. Lengo ni kuzuia kusafisha pesa chafu, ku-control kuingia na kutoka fedha za kigeni nk. Sidhani kama mafisadi wanafurahia hii kitu ila maadamu wameshikwa pabaya na hawana jinsi.
   
 17. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nina wasiwasi mwandishi hakuwa makini alipokuwa anamsikiliza Gavana, kwa sababu Gavana hawezi kuongelea nje ya mwongozo ambao Bank Kuu inautayarisha wenyewe. Sielewi mwandishi alimfahamu vipi lakini katika BUREAU DE CHANGE REGULATIONS, 2008 baadhi ya vipengele ni kama hivi.

  Regulation 15(d) which requires bureax de change to keep copies of valid identification and supporting documents for sales in excess of an amount that is equivalent to US$ 2,000.

  Regulation 19. A bureau de change shall not sell foreign currency, for any purpose in excess of an amount that is equivalent to US$ 10,000.

  Regulation 22(1) a bureau de change shall not sell foreign currency or Traveler's cheques in excess of an amount that is equivalent to ten thousand US dollars to a resident wishing to travel outside Tanzania at any one time for each trip.

  (2) A bureau de chante shall obtain and retain a copy of confirmed travel ticket and documentary proof of residence for every sale of foreign currency for travel allowance purposes where the amount sold is in excess of an amount that is equivalent to two thaousand US Dollars.

  Hamna kitu marufuku kama utafahamu hizo regulations. Kama ingekuwa kuna marufuku basi maduka ya fedha za kigeni yasingekuwepo.
   
 18. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Labda Ndullu alisahau kuongea na rafiki yako kabla ya kujibu maswali haya.You would think,maelezo kama haya yangetolewa na Gavana au kunukuliwa na kuchapishwa na waandishi wa habari kama wao ndio waliyaoverlook.

  Je?Hiki ndicho alichomaanisha Gavana aliposema ''...BOT pia iliunda timu maalum ya wataalamu kuangalia taratibu hizo''? Kwa sababu,if you ask me,hakuna mention of any US influence in the matter.Slip of the mind?

  Unajua,hata kama ni kucomputerize vitu,lazima kuwe na code of some kind.Now,by the look of things,hii ishu iko all over the place,making me think that only a BOT,magical computer system can execute such a louche strategy.
   
Loading...