Boss wako akikuudhi unamfanyaje?

Mimi bwana namsafiria pande za Mlingotini au Pemba/Unguja mitaa ya Mchambawima.
 
Maprosoo,
hiyo kubwa naitolea palepale mezani kwake au niende nayo kwenye rambo nikaibwage ofsn kwake?

change habiT
Haina haja ya kubeba kwenye rambo,wewe asubuhi kabla ya kwenda ofisini unapiga chai na kiporo cha kande nazi mixer parachichi,embe na papai unashushia koka baridiiiii .........
 
Last edited by a moderator:
change habiT
Haina haja ya kubeba kwenye rambo,wewe asubuhi kabla ya kwenda ofisini unapiga chai na kiporo cha kande nazi mixer parachichi,embe na papai unashushia koka baridiiiii .........


hahahahahah lazima nichafue si meza tu ila chumba kizima loh
 
Last edited by a moderator:
Kama boss ni kidume na "usafiri" wako unauamini, mvalie ki skin tight halaf jipitishe halaf mwambie kwa lafudhi ya kitanga "Si wajifanya mnoko weye, wallahi usafiri wangu utauona hivi hivi, wataula wengine ela kwa weye ng'o"

hahahhahaa hapo lazima alegee........
 
mie kuna siku aliniboa sasa bahati nzuri ile natoka nje lunch nikakuta kunguru kagongwa na gari kavunjia bawa hawezi kuruka;nikamtia kwenye rambo then nikaenda kumfunga kwenye kiti chake kisha nikachukua waybill ya mzigo uliokuwa umetoka dubai nikakopi yale maandishi kwa red pen nikmfunga yule kunguru mguuni:::: alivyoingia tuu ofisini kusogeza kiti kunguru akaanza kupaparika....weee!hakukaa tena ofisini na alichukua likizo ya wiki!! Wakuu nilisali maanake sikujua alikokwenda ila baada ya kurudi heshima ilikuwepo
 
By Preta "Tafuta movie inaitwa.....Terrible Bosses......utafurahi.."

Me niliwahi kuona movie moja inaitwa " Horrible Bosses" sijui kama ndo ze same au tittle za kichina?

ndio hiyo hiyo....thx....lugha za watu ujue....
 
Kuna bosi yangu moja ilikuwa inatesa sana mimi. Nikaona hii dawa yake ndogo. Nikaanza kupiga mzigo wa hatari. Waki introduce systems mpya mimi ndio kimbelembele nishajua fasta. Hadi bosi kazi zake namsaidia nafanya mimi. Jamaa alikuwa ana blackberry ana relax sometimes haji job mapema yupo kwake anatumiwa e-mails na mabosi wake ananifowardia mimi wakati yupo home tu ame chill. Nilipoona nimeshakamata kila kitu vizuri nafanya mimi nikampiga Notice ya masaa 24. Ndio siku hiyo eti ananiuliza mshahara wangu ulikuwa sh ngapi ili aongee na HR waniongezee. Nikachomoa nikamwambia siondoki sababu ya pesa. Kwa hasira akakimbilia kwa HR akasema wasiniruhusu kuondoka hadi niwape mshahara wa mwezi mmoja!

Siku ya pili nakuja job morning nimsaidie japo nifanye ka smooth handover alivyo kilaza akawafahamisha watu wa IT waondoe profile yangu. Na log in nakuta nimekuwa disabled kwenye system. Kwakuwa nilitoa notice jana yake mchana nikaenda kuzurura posta mjini kuzunguka kushangaa magari na wapita njia ilipofika mida ile nikaenda kubeba kila kilicho changu nikasepa hata sikumkabidhi vitu vilivyokuwa kwenye profile yangu.

Next day nikawaingizia mshahara wa mwezi mmoja nikasepa coz vijihela vyenyewe vilikuwa peanut!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom