Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,353
Aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza bwana Boris Johnson yuko kwenye mgogoro na chama chake cha Conservative kufuatia ujumbe wake kwenye gazeti kuhusu wanawake wavaa hijabu na baibui.
Mjadala wa kamati ya maadili ya Conservative unafikiria kumwajibisha bwana Johnson kwa kumtaka kuomba msamaha hadharani. Hata hivyo wanawake wavaa hijab wamepinga adhabu ya bwana Johnson kuomba msamaha hadharani wakidai kuwa adhabu hiyo ni ndogo sana. Wanawake hao wameweka shinikizo bwana Johnson avuliwe uwanachama.
Wengi wanasema kumvua bwana Johnson uwanachama kutaleta mgawanyiko mkubwa katika chama. Bwana Johnson ni chaguo la wengi ndani ya chama kuwa mrith wa Theresa May ambae ni waziri mkuu wa sasa.
Maneno aliyoandika bwana Johnson yaliyomletea matatizo ni kuwa wanawake wavaa hijab hufanana na masanduku ya kupostia barua au wezi wa benki “.