bora ukimwi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

bora ukimwi?

Discussion in 'JF Doctor' started by Raia Fulani, May 21, 2009.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ndio baadhi ya watu wanavyosema. Hata mimi nimewahi kuwaza hivyo kabla ya kusikia kwa watu. Hii dhana ni dhidi ya ugonjwa wa kisukari ambao una masharti magumu hasa kwa mtu wa kipato cha chini. Huu usemi unaweza kuwa sawa au nu upotoshaji tu?
   
 2. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Yaani Bora uumwe ukimwi kuliko Kisukari? sijakuelewa
   
 3. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,181
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 280
  Mkuu, sijakupata kabisa. Hebu fafanua kidogo ni masharti yapi hayo ambayo ni magumu kwa mlalahoi.
  1.Je umewahi kuwaza nini?
  2.Umesikia watu wakisema nini ?

  Sidhani kama kuna ugonjwa ambao tiba yake haina masharti. Ukimwi tiba yake bado ni msamiati na bado mgonjwa anapewa masharti lukuki!
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  yaani bora uumwe ukimwi kuliko kisukari maana ukimwi una madawa mengi ya kupunguza makali ila kisukari ni maumivu tu
   
 5. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  jamani... wenye kusema heri UKIMWI, mmeshawahi kuona mgonjwa wa UKIMWI au mmeona tu watu wenye VVU?
  Kisukari ukifuata masharti unakuwa kawaida tu.... na iko mifano mingi sana ya watu wenye kisukari na wanaishi nao kwa miaka mingi.
   
 6. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #6
  May 21, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,181
  Likes Received: 663
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hata kisukari unaweza ukapunguza makali yake kwa kufuata masharti.
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  May 21, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  sasa watu wanataka kuamini kuwa bora upate VVU tu na utumie hizo dozi. Nadhani wanasema hivyo kutokana na masharti yaliyopo kulinganisha na magonjwa hayo (hususan kwenye vyakula)
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  May 21, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Tusifikiri kuwa kila mwenye VVU basi anaweza kuponea kwenye ARV.Kuna wale ambao hawawezi kuhimili reactions za ARV.

  Halafu unapoanza kutumia ARV huwezi kuacha hadi mwisho wa maisha yako..na dawa zinaweza kuwa na effect/reaction mbaya..na siyo kidonge kimoja.ni cocktail iliyosheheni.In short its not easy kama wengine wanavyodhania.
  Unapokuwa unatumia ARV kuna masharti yake pia tena huenda mi magumu zaidi kutegemeana na mwathirika.
   
 9. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #9
  May 23, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Kama natakiwa kuchagua mi kwa furaha nachukua VVU. KISUKARI na UKIMWI yote ni magonjwa sugu yanayohitaji muathirika kunywa dawa for LIFE!, lakini KISUKARI ni complicated zaidi ya ukimwi. KISUKARI hata kama utafuata masharti vizuri lakini comlications lazima zikukute, km vile UPOFU, KUPOTEZA VIUNGO hasa miguu, KUPOTEZA NGUVU ZA KIUME, SHINIKIZO LA DAMU, KUHARIBIKA MISHIPA YA FAHAMU, KIHARUSI, KUHARIBIKA FIGO (leading cause of Renal failure), n.k, n.k, kwa ujumla quality ya life inakuwa severly compromised kuliko anayekula ARV, dawa za ARV zimezidi kuboreshwa... idadi ya vidonge inazidi kupungua, huduma ni bure, vituo vya tiba na wataalamu wako kila hospitali, lkn tiba ya kisukari ni duni na aghali sana.
   
 10. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #10
  May 23, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii ni "old thought" hasa kwa madaktari wa miaka ile! Sio kweli kuwa ukiwa na kisukari lazima uishie kwenye renal. eye, brain ama cardiovascular complications. NO. Evidence zaonyesha uki-control vizuri sukari yako (largely kwa lifestyle na partly kwa dawa) you should be OK.
  Na masharti wala sio magumu; ni hizi beliefs tu ndio zimepelekea kuwa na attittude kama hii.
  Visenti inabidi urudi shule kwani hili ni suala muhimu sana na unatakiwa uelimishe watu hapa; sorry!
  Kisukari una-control vizuri kwa lishe na mazoezi - vyakula ni hivi hivi vilivyopo magengeni, mchicha, matembele, maharage n.k na mazoezi ndio haya ya kutembea, kuna issue hapo - evening walk kila siku unafurahia mandhari na kujitibu.
  NB: kisukari kinachoongelewa hapa ni type 2 (ambacho kina-account for 90-95% ya kisukari patients).
  On the other hand, UKIMWI kibaya zaidi kuliko hata masharti ni STIGMA.
  Kunyanyapaana kukipungua kutasaidia sana kupunguza makali ya VVU.
   
 11. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #11
  May 23, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hao watu wanaosema bora Ukimwi hawaja upata bado, wana sema tu kwa sababu hawaja upata. Jamani dawa za VVU zina side affect mbaya sana na una takiwa unywe on time every time. Life style yako lazima pia ibadilike kutokana na ugonjwa. Watu msiji roge wenyewe hapa kusema bora Ukimwi kisha ukiupata huo Ukimwi wenyewe au VVU ndiyo uwe wakwanza kuombea bora ungekua na kisukari. Tatizo mtu asiye na ugonjwa fulani siko zote ataongelea huo ugonjwa kwa mzaha. Mbona nisha sikia watu wengi wakisema Ukimwi kama malaria tu lakini waambie wakapime uta shang'aa woga unavyo waingia.

  Jamani HIV/AIDS is very serious. ARV zenyewe zina side effects nyingi na kubwa sana na zina cause complications kubwa sana. Life style yako inakua controlled by the medications. Mkiwaona ambao wana tumia ARV msione ni kazi rahisi, ni kwa sababu hawa watu hawana alternative. Baada ya muda wana jifunza kukubali hali.

  Hili swali muulize mtu mwenye VVU kuwa akiambiwa sasa hivi awe na kisukari badala ya VVU ata kubali kubaki na VVU? Nyie mnaosema bora VVU ni obvious hamna uelewa wa ugonjwa wenyewe wala tiba zake. Tafitini tu hata kwenye mitandao mtajua kisha mrudi mseme tena bora VVU.

  VVU:
  1.Haina tiba
  2.Life expectancy tokea maambukizi 10-20 years na hiyo ina tegemeana mtu hadi mtu
  3.Dawa kunywa on time all the time
  4.Uki kosea tu muda wa dawa ume tia dosari tiba
  5.Side effects mbaya
  6.Uta develop tu Ukimwi mwishoni na hapo utaona mateso yake.
  7.VVU ikianza kudevelop kuwa Ukimwi dalili za nje ya mwili zinaonekana kitu ambacho kina encourage uyanyapa toka kwa watu wenye uelewa mdogo(which are a majority).
  8.Kuna mambo kama kuumwa mara kwa mara, kuharisha, mahoma ya mara kwa mara, jasho za njozi mbaya usiku etc.
  9.Kuna mengine mengi pia ambayo siyo lazima niorodheshe hapa if you are interested fanya utafiti ila hata common sense yako itakupa baadhi.

  Kisukari
  1.Mabadiliko ya maisha kama kula vizuri na mazoezi mambo ambayo kila mtu ana takiwa kufanya in the first place awe na kisukari au la.
  2.Life expectancy yako haiwi compromised as long as una fuata masharti yanayo takiwa
  3.Check ups the mara kwa mara which again kila binadamu ana takiwa ajijengee tabia hii au na kisukari au la.

  JAMANI MWENYE AKILI TIMAMU HAPO KWELI UTASEMA BORA VVU KULIKO KISUKARI?
   
 12. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #12
  May 23, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ukweli kuhusu ukimwi ni kwamba ukikubali unao utakuwa salama. Pia masharti yake ni kama maisha ya siku ya mtu, yaani kula diet, mazoezi, cheki afya mara kwa mara, usiwaze, n.k. Sasa kisukari kinaondoa nguvu za kiume, % 90 ya vyakula huli, n.k. Ukitaka kuishi na ukimwi kwa raha upime mapema na kufuata masharti
   
 13. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #13
  May 23, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ngoma pia yasababisha ngwengwe kutofanya kazi in the long run. Na sio kweli kuwa kisukari kitakufanya usile 90% ya vyakula.
   
 14. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #14
  May 23, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Ukweli ni kwamba, Ukimwi ni ungonjwa ambao umeoneka kuenea kwa kasi sana hapa Duniani hasa kusini mwa Jangwa la Sahara. Kwa hiyo nguvu nyingi sana imetumika ili kupambana na tatizo hili.

  Kutokana na kuwepo kwa madawa ya kupunguza makali ya virusi vya ukimwi (ARV) na kufuata masharti mgonjwa wa ukimwi anakuwa na nafuu zaidi ya mgonjwa wa kisukari.

  Barani afrika ni mtu gani mwenye maisha ya kawaida au ya hali ya chini anaweza kuishi bila ya kukutana na starch kwenye vyakula anavyokula kila siku???
   
 15. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #15
  May 23, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145

  so tufike conclusion tuseme angalau mgonjwa wa ukimwi ana nafuu zaidi kuliko wa kisukari
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  May 23, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  so tufike conclusion tuseme angalau mgonjwa wa ukimwi ana nafuu zaidi kuliko wa kisukari
   
 17. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #17
  May 24, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Outlier acha jazba, mi nipo shule siku zote, huo ni mchango wangu wewe elimisha kivyako bila degedege. Nimechangia hoja "UKIMWI vs KISUKARI" hasa kwa watu masikini walio wengi (remember the thread is Philosophical and so are my views).
   
 18. Visenti

  Visenti JF-Expert Member

  #18
  May 24, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 1,031
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 133
  Mziwanda, fungua www.worlddiabetesfoundation.org/composite-35.htm itakusaidia kujua ukali wa KISUKARI kwa mtu masikini, kisha linganisha na huduma za UKIMWI ilivyo sasa.
   
 19. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #19
  May 24, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,220
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  poa chief, nitafungua mda kidogo. Umetoa hoja hapo juu. Hatuombei mtu kuumwa kwa vyovyote ila magonjwa tumeumbiwa wanadam. Watu wanahofu na ukimwi kutokana na historia yake nchini. Kuna usemi usemao avumaye baharini papa. Kumbe wapo wengi. Hao wengi ndio kama kisukari, kansa, n.k. Angalau ukimwi ukiujulia una ahueni ila sijui ahueni ya kisukari iko wapi
   
 20. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hakuna degedege wala tantrum; hii ni about facts sio philosophy. views inabidi ziwe na evidence, na its wrong big time kusema kuwa ukiwa na kisukari lazima uishie na complications za figo, hert etc.
   
Loading...