bora ukimwi?

uzuri nimeshauguza mgonjwa wa ukimwi,NA WA KISUKARI!

kutoka moyoni nachelea kusema kwa sasa BORA UKIMWI!

Naomba kuuliza ndugu. Unaposema bora UKIMWI ni kwako kama muuguzi au kwa mgonjwa? Kwa maana inaweza ikawa unasema bora kumhudumia mtu wa UKIMWI ni rahisi kuliko kumuuguza wa kisukari. Swali ni in the retrospect of the one who would have the desease.
 
funny-picture-33.jpg


JE BOORA NI IPII????
 
Kuna vitu tunatakiwa tuelewe hapa, kwanza wote tunachoomba ni kuwa wazima bila ugonjwa wowote. Lakini maadamu sisi ni wamadamu basi hatuwezi kukosa magojwa. Mimi personally sioni bora kipi ila nitajaribu kutoa views zangu kati ya haya magonjwa mawil.
Kuwa na VVU haina maana una ukimwi, japo ukimwi ni end product ya VVU, cha ajabu, kisukari nacho huwa kinasababisha upungufu wa kinga mwilini especially uncontrolled one, ndo mana tunapata complication katika organs nyingi za mwili. Hapo hapo VVU navyo vinasababisha kisukari hasa unapopata viral pancreatitis huu ni ugonjwa wa kongosho unaosababishwa na VVU au hata bacteria. Lakini pia hata dawa za kupunguza makali ya VVU kama zile za second line mfano Protease Inhibitor huwa zinasababisha kisukari.

Tukija kwenye quality of life hapa inategemea position ya mgojwa economically na pia level ya uelewa lakini na readness kupambana na haya magonwa. Hivyo kusema kipi ni bora is so relative na pia si vyema.
 
Watanzania Milioni 1.5 waambukizwa virusi vyva ukimwi
2149722.jpg

Wednesday, June 03, 2009 9:26 AM
WATU Milioni 1.5 wameambukizwa virusi vya ukimwi kati ya watu Milioni 38 waishio nchini Tanzania kwa kipindi cha mwaka jana. Tathimini hiyo ilitolewa jana na Tume ya Ukimwi nchini [TACAIDS] iliyotolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa Tume hiyo Bi. Fatma Mrisho jijini Dar es Salaam jana.

Dk Mrisho alisema kuwa kati ya hao watu wazima kuanzia miaka 15 mpaka 49 wameambukizwa na kati ya hao wanawake ni asilimia 6.6 na asilimia 4.6 ni wanaume.

Amesema katika watu hao walioambukizwa ukimwi nchini asimilimia 10 ni watoto wadogo ambao wameambukizwa kutoka kwa wazazi wao.

Amesema mbali na maambukizi hayo pia amesema maambukizi ya ukimwi yameshuka kwa asilimia 7 kwa kipindi cha mwaka 2007 hadi 2008.

Pia amesema kuwa kwa makadirio yaliyofanyka imeonyesha kuwa elimu inaonyesha kuwa asilimia 46 ya watanzania wanaufahamu juu ya ukimwi na maambukizi lakini nusu ya watanzania hawaelewi kabisa juu ya virusi vya ukimvi.

Amesema shirika hilo wanaelekeza semina na elimu juu ya ugonjwa huo hasa kwa upande wa vijijini ambapo kumeonekana hawana ufahamu kabisa kuhusu ukimwi.
 
...Mziwanda umeleta hoja nzuri tu ambayo tunajifunza mengi toka kwa wachangiaji. Mchango wangu ni kama ifuatavyo; UKIMWI kwa maana ya UPUNGUFU WA KINGA MWILINI humlazimisha mgomnjwa kufuata masharti yafuatayo
1. Kuzingatia masharti ya unywaji wa dawa (adherence). Kwasa dawa zilizopo atakunywa asubuhi na jioni. Idadi ya vidonge itategemea yuko kwenye regimen ipi, mara nyingi ni 1x 2 au the current regimen ya AZT/3TC/EFV atameza 2x2. Bahati nzuri tayari hapa nchini ipo dawa ya ATRIPLA inapatikana kliniki ambapo mgonjwa humeza kidonge kimoja tu i.e 1x1

2. matumizi ya ARV ni lifelong
3. Pia mgonjwa atalazimika kunywa dawa kuzuia/au kutibu magonjwa nyemelezi.(when neccessary)
4. Atalazimika kuhudhuria klinic kwa ajili ya follow up care na refill ya dawa monthly.
5. Atashauriwa kula lishe bora na kujiepusha na vyakula/vinywaji vinavyodhoofisha afya yake (ulevi wa pombe,sigara nk)
6. Afanye mazoezi kuimarisha afya yake.
7. Ajikinge dhidi ya maambukizi mapya kwa kufanya ngono salama (condom)

Hayo ndio mambo ambayo BASICALLY anapaswa kuyafanya (yanaweza kuwepo mengine)

Kumekuwepo na upotoshaji unaotokana na kukosa taarifa sahihi juu ya ugonjwa wa Kisukari. Wengi wakiuhusisha na masharti mengi na side effects kibao! Dhana ya kizamani kuwa mgonjwa wa kisukari asile mlolongo wa vyakula imepitwa na wakati. Tiba ya kisasa inshauriwa mgonjwa wa kisukari kula kiasi kidogo but with an increased frequency. hapa essesnce ni ku mentain normal level ya sukari through out the day. Hivyo swala la kumfanya mgonjwa wa kisukari asile vyakula mbalimbali halipo! Kisuari huonekanabalaa pale kinapokuwa uncontrolled, ambapo mtu huanza kupata madhara kwenye mishipa ya damu na kuleta Impontence, impaired eyesight, Renal problems, skin problems, fungal infections,etc

Kwa mleta hoja nafikiri pengine suala hili linaweza kuwa gumu ukilitizama kwa kuangalia hali ya kiuchumi, literacy level kati ya wagonjwa hawa wawili na jamii inayowazunguka
manake stigma around HIV it is a disease of its own!

Kwasababu kwa jamii kwenye nchi zilizoendelea HIV/AIDS is just as chronic as any oter crhonic disease like hypertension, Diabetic mellitus, etc Life expectancy and quality ya HIV patients has significantly gone up

asante
 
Tunashukuru, kizikmazimkuu kwa uchambuzi huo mahiri. Kimantiki, magonjwa yote yanaumiza kwa vile inahitaji uangalifu katika kukabiliana nayo. Kwa mtu anayetumia dawa kwa upande wa ukimwi sijajua kama huwa anakuja tena kupatwa na ile hali ambayo huwa wanaipata wagonjwa wengi ambao kinga yao imeshuka sana. Mara nyingi nimesikia kuwa huwa wanaanguka ghafla na kufa. Kwa wale wa kisukari hata kama atatumia dawa inafika wakati hali inakuwa ngumu kuizuia-ndio unakuta impotency, mkojo kutoka, macho kuharibika, n.k. Ila "Dokta" hajatuambia yeye kasimamia wapi katika fadhaa hizi mbili
 
Back
Top Bottom