Bora niombe .........

Bora niombe .........

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
1. Natunukia wenzangu, nilonacho sikhiyana
Katika fikira zangu, kutoa nikupeana
Lakini bahati yangu, kutunukiwa hakuna
Bora niombe

2. Natunukia wenzangu, nilichonacho hutowa
Kiwe ni saizi yangu, japo kidogo hugawa
Lakini bahati yangu, situnukiwi hapewa
Bora niombe

3. Natoa kauli yangu, kuomba nnachoomba
Hata majirani zangu, ni wengi wameninyima
Baadhi ya walimwengu, ukiwaomba hununa
Nami nipewe

4. Mwisho wa beiti yangu, kaditama nnatowa
Natunuku jasho langu, lengo na makusudiwa
Maneno ya walimwengu, kupeana ni kikowa
Nami nipewe
 
Back
Top Bottom