Bora nikaoe Tanga

Ndugu usioe Tanga,Mimi ninakuambia,
Hao watu wanaringa, Kisa tu kuwasifia,
Sio kwamba nakupinga, ukweli nakuambia,
Bora uje kwetu Njombe,kuna Wanawake wema,

Uje uoe mkinga,mpangwa au Mbena,
Maisha mtayapanga,na kufanikiwa sana,
Uchumi mtaujenga, tena pasipo hiana,
Heko Mabinti wa Njombe,Kwa tabia yenu njema,
 
Noma sana kweli ushairi wa kiswahili utaishi milele
 
Mkuu upo vizuri, Dada zako wakibena nawaelewa sana, wanajua kupenda.
 
Karibu Tanga...
 
Watamu hao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…