Bora nikaoe Tanga

Kama umetunga mwenyewe basi big up sana mzee wa Tanga kwa njeka.
Ahsante mkuu,
nikipaji kutoka kwa maulana,
nashukuru sikuanza juzi wala jana
 



MPWA WANGU
Imeshapita miaka,toka liposhika peni
Lile jambo solitaka,naona lipo mezani
mtunzi atiririka,kwa beti ziso kifani
kijana mwana wa kaka,tanga wenda fata nini?

yanishangaza barua,ndefu uliyoandika
akili ukazuzua,kwa misemo kusikika
tanga bahari ya nzoa,kwa huba yasifika
bure utajisumbua,nenda oa lipotoka

limekudatisha pishi,au kanga za mwilini
wajuvi tushirikishi,mpwa wangu watakani
ni viuno tetemeshi,wawapo huko ngomani
au memfata mishi,mwanangwa wa chumbageni

wataka kwenda korogwe,ukatafute mwandani
akili ikavurugwe,umletapo mjini
mchuzi kutiwa ngogwe,si utamu wa chumbani
kwa mganga ukarogwe,hayo ndo mapenzi gani

siku hizi si wa stara,wake wa tanga mjini
wanayabana madera,wakivaa na vimini
midomo wanaifura,ati watoto wa pwani
utajapata hasara,ututie lawamani

naona mesema mengi,na wino menishia
ila jambo la msingi,fata nilokuusia
ata maji yana rangi,ila huwezi ijua
kaka yangu majimengi,salam tampatia
 
MPWA WANGU
Imeshapita miaka,toka liposhika peni
Lile jambo solitaka,naona lipo mezani
mtunzi atiririka,kwa beti ziso kifani
Hahahahahahaha ahsante sana naona shairi limetulia πŸ™‚πŸ™‚πŸ™‚
 
Kaoe tanga ujute, na kilio cha hudhuni
Nyingi Pesa utafute, zinaishia ugangani
limbwata uje upate, akuingie akilini
Familia uifute, usahau kwenu nyumbani
Tanga kuzuli kuoa ila ujipanga mawazoni
 
Tanga mkoa pekee, kwa warembo tashtiti
Kwengine sikosee, moyo taupiga kibiriti
Iwe wachaga wahehe, au wale wamang'ati
Ugomvi kangojee, kikosa pesa ya vyapati
Na ukiwa pedeshee, takunyonga kwa shati
Ila Tanga utastarehe, hata kama riziki hupati
Taitwa bwanshee, mapajani tawekwa kati
Kwa mahaba akulee, kwa huba ya dhati
Na heshima akuletee, hata kwenye umati
Maji akutengee, yanukia mahanjumati
Chooni akupelekee, kuonyesha mahabati
Na ukitoka akupokee, sabuni na mswaki
Kisha dozi akugee, mpaka utetemeke magoti
Kwenu usirejee, na wala hukuoti.
 
Tanga Mjini ,,ingia Tairi Tatu,magaoni,na kwanjeka ,,duuuh Yan Kuna watoto wa KiswahiLi wazuri Mfano hakuna
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…