Bora nikaoe Tanga

Hapo mikanjuni ulipotaja pana demu wangu anaitwa Khadija ni kungwi huyu wa kufundwa wari, sasa ole wako ukamchukue usije sema sikukukanya.
 
JIBU LA SHAHIRI..NIOE TANGA.
Na Wenyewe twajijua,siri ya mke wa pwani,
shanga zilizozagaa,mguni na kiunoni,
Hawahitaji chapaa, zitokazo mashineni,
Kaoe baba kaoe, Nyumbani tanga kunani!.

Siri ni ngoma ya ndani, siyo ya mkidigeni ,
hufunziwa kitandani, siyo yenu hadharani,
Huchoma ndani miyoni,kufurahisha machoni,
Kaoe baba kaoe,Nyumbani tanga kunani!.

Huzifunga zao shanga,kiuno bigili ndani,
huzivunja zao chaga, kwa ile shuhuri ndani,
kama mtoto mchanga,kilio cha dirishani,
Kaoe baba kaoe, Nyumbani tanga kunani! .

Waja leo ondoka leo,Ni msemo wa zamani,
waja leo wala leo, ufunuliwe vya ndani,
wala usinywe kileo,ili upate mwandani,
Kaoe baba kaoe,Nyumbani tanga kunani! .

Oa makorora sikoni, wala si wa mikanjuni,
si muheza si handeni, kote kumeja mapenzi,
wakuacha simuoni, vyote vya utamu ndani,
Kaoe baba kaoe, Nyumbani tanga kunani! .
 
Mkuu wewe ni mtunzi mzuri, endeleza kipaji chako
 
shairi zuri kweli lina vina na mizani, hongera
 
Hongera mkuu umetisha ila kuhusu kupanda milima siku hiz wote tunapanda mlima! wengine wanaruka hadi ukuta! afadhal hata anaepanda mliman labda atarud na kuni kuliko tunao tafuta kitu ambacho hatukioni wala kukipata!
 
Hongera mkuu umetisha ila kuhusu kupanda milima siku hiz wote tunapanda mlima! wengine wanaruka hadi ukuta! afadhal hata anaepanda mliman labda atarud na kuni kuliko tunao tafuta kitu ambacho hatukioni wala kukipata!
Ahsante mkuu, hahahahaha anaepanda mlima labda atarudi na kuni
 
Mabinti Wa Kitanga Wanasifika Sana Kwenye Mapenzi Na Mie Nijongee Nikatafute Wangu Wa Maishani
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…