Bora kutumia akili ya kuzaliwa nayo kuliko Elimu ya makaratasi

Siku hizi kuna nyuzi nyingi zinafunguliwa na members kujaribu kuonyesha elimu ya darasani haina faida. Mtu ukifikia hatua ya kuona elimu uliyosoma darasani haikusadii na ulipoteza muda bure basi ujue ulienda shule kukariri ili ushinde mtihani na hukwenda kuelimika. Na hili liko sana kwenye shule nyingi za Tanzania.

Nadhani mfumo wetu wa elimu ni mbovu haswa ndiyo maana watu wanamaliza mpaka chuo kikuu lakini hawana tofauti na walipomaliza darasa la saba. Muda wote kuanzia sekondari mpaka chuo kikuu walikuwa wanakariri ili mtihani ukija wafaulu vizuri. Mimi nimemaliza degree na shughuli ninazofanya ni tofauti kabisa na vitu nilivyosoma lakini sijawahi hata siku moja kujuta ni kwanini nilisoma.
 
IMG-20200706-WA0013.jpg
 
Tafuta kazi ndugu yangu usikate tamaa, ni vibaya sana kuitukana elimu uliyoisotea zaidi ya miaka 16-17,maana hujui lini na wapi itakuokoa!
 
~ sisi tusiokuwa na helimu tunajuta kuikosa....wewe hauitaki binadamu ni mwingi wa tamaa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom