Kategele
JF-Expert Member
- Oct 7, 2017
- 971
- 2,233
Ni miaka imepita tangu nihitimu hii elimu ya makaratasi nimegundua kumbe ilikuwa mahususi kwa kuajiriwa na kunifanya niwe mtumwa wa kazi za wengine.
Serikali Mungu anawaona mumeandaa mtaala wa kutumia muda mwingi shuleni, jamii nayo ikaaminishwa kuwa kusoma na kupata vyeti ndiyo kufanikiwa kumbe mlitupofusha ili tusione fursa mtaani.
Haiwezekani Leo na elimu yangu nikiingia pale kariakoo naonekana Kama darasa la saba,wakati kuna watu hawana elimu ila ndo wamiliki wa machimbo yote ya biashara wanapiga pesa balaa.
Kuna watu walishituka mapema wakaingia mjini kufanya mishe wako mbali Leo nakutana nao ndo naanza kufanya training ya kujua machimbo ya biashara!
Ewe muhitimu mwenzagu nakupa ushauri shituka mapema usikalie kusambaza Cv tu Kuna fursa zipo mtaani sema elimu yetu haitusaidii zaidi ya kututoa kwenye ushamba nakutupeleka kwenye ujinga pia kutuacha hapo kwenye ujinga.
Elimu ya makaratasi kwaheli naanza kutumia akili yangu ya kuzaliwa.