Bora kufa kuliko kuwa CCM, sitokaa niipende kamwe

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Kuliko kuwa mwanaCCM bora kufa tu.

Nilishawahi kujitahidi kujaribu kuwapenda lakini wapi lakini nashindwa

Wametutalawa kama mifugo kwa miaka 60 huku wakijiona wao wapo juu ya dola na wakilitumia jeshi la polisi kututawala kimabavu

Ccm bila polisi na Idara ya Usalama wa Taifa hawawezi kusurvive

Nakichukia hicho chama na sitokaa nije kuwa mwanaCCM sio mimi tu hata familia yangu, ni bora watoto wangu wasijihusishe na siasa kabisa na kutofungamana na chama chochote kuliko kuwa ccm.

Bora nife kuliko kuwa CCM
 
Mkuu ulishawahi Kufa? maumivu yake hayasimuliki enewei ngoja nishuke kwenye boda boda nichangiepo na mimi
 
Bora .....
Mimi sikubali ufe Hata kidogo. Tuna kazi hatujaimaliza ya Kurudisha walimwengu kwenye ustaarabu wa kuheshimiana kati ya nchi na nchi na kati ya binadamu mmoja na mwingine!!!

Ufe suala la Ukraine unamuachia nani ?

Ufe suala la kuhakikisha mwanaume anayezaliwa mwanaume Anaendelea kuwa mwanaume unamuachia nani?

Ufe suala la kuhakikisha mwanamke anayezaliwa mwanamke Anaendelea kuwa mwanamke unamuachia nani?

Nasema sikubali ufe

Ufe halafu vita aliyoianzisha Putin kuikomboa dunia kutoka kwa wadhalimu unamuachia nani?

CCM ni chama kinachoongoza serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano Tanzania. Kimeshida uchaguzi Mkuu uliopita kipo madarakani kwa mujibu wa Katiba. Uendeshaji wa uchaguzi uliopita kama chaguzi nyingine zilizopita unajadilika.

Mkuu nasema hufi mpaka utimize wajibu wako hapa Duniani. Ebu rejea kauli ya Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Dr Bashiru(PhD) kuwa CCM ni chama dola! Hivyo, hakiwezi kuachia Dola maana lengo la uwepo wake ni kutetea maslahi ya wakulima na wafanyakazi na makundi mengine kwa mujibu wa katiba na kanuni ya Chama hicho.

Sasa Mkuu, unakimbiaje Dola yako? Ili ulinde Dola yako ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lazima uwe Karibu na Dola. Njia Rahisi ya kuwa Karibu na Dola ni kujiunga na CCM! Ndiyo, ujiunge na CCM lengo uweze kupata nyenzo za kuweka mikakati ya kuwezeshwa Wananchi Wana nufaika na rasilimali za nchi hii.

Binafsi, naamini Ungekuwa ndani ya CCM huu "mtanzuko" wa DPWorld tungeusikia kwenye bomba! Usicheke, Mkuu uwezo huo unao.

Mkuu una kazi mbele yako ambayo umetumwa Duniani kusaidia walimwengu wakae salama!!! Mkuu haufi, jiunge CCM mara Moja!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom