Ferruccio Lamborghini
JF-Expert Member
- Apr 15, 2020
- 1,667
- 2,631
JOHN Magufuli hayupo duniani. Ila nguvu yake bado inaishi ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Magufuli alitengeneza wabunge wake. Wanaitwa “loyal to a fault" – “watiifu wasioambiwa chochote". Wanaendelea kumtii hadi leo akiwa kaburini, kuliko kukitii chama chao, CCM.
Ukarabati ndani ya CCM ambao Magufuli aliufanya kati ya mwaka 2016 hadi Uchaguzi Mkuu 2020, ni matunda ya sasa.
Biashara kubwa ya wabunge ilifanyika, wapinzani wakajiuzulu ubunge na kujivua uanachama, kisha kujiunga na CCM kwa jina la “kuunga mkono juhudi za Magufuli".
Wahamiaji wakalindwa wasipingwe ndani ya chama na kurudishwa bungeni kwa leseni ya dezo ya Chama Cha Mapinduzi.
Tukafika 2020, mchakato wa kupata wagombea ubunge CCM. Walioshindwa ndio wakapitishwa. Na kwenye uchaguzi, wakatangazwa washindi hata wakiwa hawajui walishindaje.
Hali ya wageni kupewa mbeleko kwenye chama, wenyeji wakajiona hawapo salama. Ghafla ukaibuka mkumbo wa kumsifu Magufuli kwa bidii kubwa. Wasiosifu walionekana wapo nje ya “fasheni" mpya ya kisiasa. Wakapewa kisogo.
Uchaguzi Mkuu 2020, ukahitimisha kilichoanzishwa mwaka 2016. Waliopewa nafasi ya kugombea ubunge kupitia CCM hadi kutangazwa kwao kuwa washindi na kuapishwa, shukurani zao zote ni kwa Magufuli.
Hivyo, Bunge la Tanzania hivi sasa ni matokeo ya nusu muongo, ambao Magufuli aliutumia kujiimarisha binafsi kuliko chama. Wabunge wengi wanajiona wana deni kubwa kwa Magufuli kuliko Chama Cha Mapinduzi.
Kwamba bila Magufuli wala wasingekuwa wabunge. Wanapojitathmini hawajioni ni wabunge wa wananchi wala chama. Walipewa na mtu.
Livingstone Lusinde ‘Kibajaji', alipata kuwashushua wabunge wenzake bungeni kuwa bila Magufuli wasingeupata ubunge. Bila shaka aliwakumbusha kulipa fadhila angalau ya utii kwa aliyewapa ubunge.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana, Aprili Mosi, mwaka huu, aliuambia Mkutano Mkuu wa chama hicho kuhusu makosa yaliyopita ya kumsifu na kumtukuza mtu mmoja.
Hivyo, kwa hoja nyingi na vielelezo visivyoacha shaka yoyote, jumlisha “mpasho” wa Kibajaji na makosa yaliyosemwa na Kinana, tunakubaliana kuwa Bunge la sasa lina “U-Magufuli” mwingi kuliko “U-CCM".
Hii ndio sababu, hoja yoyote hasi kumhusu Magufuli ikizungumzwa hata mitandaoni na watoa maoni wa kawaida, kuna wabunge wanakuwa wakali. Bunge linawaka moto.
Hawataki Magufuli asemwe kwa aliyotenda. Wanasema “mtu akifa na kitabu chake kinafungwa". Hata tukio la Tundu Lissu kupigwa risasi nyingi Septemba 7, 2017, kisha polisi, Serikali na hata Bunge kupotezea, lisizungumzwe. Lissu ni mlemavu leo.
Mwandishi wa habari Azory Gwanda alipotea Novemba 2017, mwanaharakati Ben Saanane, alitoweka kwenye uso wa jamii Novemba 2016. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kibondo, Simon Kanguye, hajulikani alipo tangu Julai 2017. Wapo wapi? Nani aliwapoteza?
Ongeza mamia waliouawa Mkuranga, Kibiti na Rufiji (Mkiru). Uchaguzi ulioharibiwa mwaka 2020. Utitiri wa kesi za uhujumu uchumi na watu kulipa fedha kwenye akaunti za watu binafsi badala ya Serikali.
Pamoja na vyombo vya Serikali, Bunge ni chombo chenye wajibu mkubwa wa kusawazisha masuala yenye utata kwa umma. Badala ya Bunge kuomba kuundwa Kamati maalum ya kiuchunguzi juu ya masuala yanayoacha viulizo vingi kipindi cha uongozi wa Rais Magufuli, ndio kwanza wanasema “mtu akifa kitabu chake kinafungwa".
Alikuwepo Cyprian Musiba. Alikuwa na nguvu za ajabu sana. Alimchafua yeyote amtakaye na hakuna aliyethubutu kumgusa. Bunge linapaswa kuchunguza nyuma ya Musiba alikuwepo nani? Alilindwaje na alikuwa analipwa nini na nani?
Lengai Ole Sabaya alipata kusema mahakamani kuwa baadhi ya mambo aliyohukumiwa kuyatenda, alitumwa na Magufuli. Je, Sabaya anamsingizia? Bunge halioni wajibu wake wa kuondoa utata? Eti, mtu akifa na kitabu chake kinafungwa!
Paul Makonda ana tuhuma nyingi. Serikali ya Marekani ilishatoa taarifa ya kumpiga marufuku kukanyaga ardhi yao kwa makosa kadhaa, moja wapo likiwa kudhulumu haki za watu za kuishi. Bunge linatakiwa liisaidie nchi, akina nani walidhulumiwa maisha yao na Makonda? Uvamizi wa Clouds Media Group na bunduki upoje?
Kuna tuhuma kubwa kuhusu kikosi kazi kilichoundwa kukusanya madeni ya kodi na mapato mengine kuwa watu wengi walibambikiwa malimbikizo na kushurutishwa kulipa fedha kwenye akaunti binafsi badala ya Serikali. Bunge halioni hii ni agenda ya kufanyia kazi?
Bunge halitaki kutuliza ubongo kujiuliza kwa nini benki 11 zilifungwa wakati wa Magufuli? Kwa nini wafanyabiashara wa kubadilisha sarafu za kigeni (bureau de change) walifilisiwa mitaji yao kwa mtutu wa bunduki? Fedha zao zilikwenda wapi?
Mdororo wa kiuchumi wakati wa Magufuli ulisababishwa na nini? Kwa nini biashara nyingi zilifungwa? Ilikuwaje kipindi cha Magufuli ndio vyombo vingi vya habari viliingia ICU na vingine kufa kabisa? Yote hayo yaachwe kwa usemi dhaifu wa mtu akifa kitabu chake kinafungwa?
Hivi leo, ripoti za mapato ya Serikali kuongezeka wala hazilishitui Bunge, kuona kuwa kuna namna mambo yalikuwa yanakosewa na sasa yamerekebishwa.
Ripoti ya Mapitio ya Kiuchumi kila mwezi ya Benki Kuu, iliyotoka Januari mwaka huu, sio tu kwamba inaonesha kuimarika kwa mapato ya Serikali, bali pia hivi sasa Tanzania imepunguza kuagiza na imeongeza kusafirisha bidhaa nje ya nchi kwa kiasi kizuri.
Mambo haya yangetokea wakati Rais Magufuli yupo madarakani, angesifiwa na kupambwa kwa kila aina ya ngonjera. Hivi sasa Bunge lipo kimya. Kwa nini?
Jibu ni rahisi; wabunge wengi ni watiifu wa Magufuli hadi leo kutokana na jinsi walivyoingizwa bungeni dezodezo. Wana mahaba makubwa na Magufuli kwa ubunge walioupata kwa kujiokotea.
Februari mwaka huu, bungeni, Waziri wa Nishati, January Makamba, alilazimika kutoa takwimu za mapato kwa miezi miwili ya wakati wa Magufuli na miwili nchi ikiongozwa na Samia.
January alisema, Novemba 2020, Magufuli akiwa Rais, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), ilikusanya Sh1.3 trilioni. Novemba 2021, Samia akiwa kwenye usukani, mapato yalikuwa Sh1.7 trilioni. Desemba 2020 TRA walipata Sh2 trilioni na Desemba 2021 makusanyo yalikuwa Sh2.4 trilioni.
Hivi karibuni, nilikuwa nazungumza na mmoja wa vigogo wa TRA, akasema “huyu mama (Samia) sijui ana miujiza gani, sasa hivi tunakusanya mapato mpaka tunashangaa.”
Ukweli ni kuwa hakuna miujiza. Mazingira yamebadilishwa. Watu wana amani leo ya kibiashara. Biashara zinafunguliwa kwa wingi na wafanyabiashara waliokuwa wanajibana hivi sasa wanajitanua. Foleni benki zimerudi. Mzunguko wa fedha unaendelea kustawi.
Miaka ya nyuma kila mbunge akisimama, anatumia robo tatu ya muda aliopewa bungeni kwa ajili ya kumsifu Magufuli. Hivi sasa kimya. Utadhani Samia hafanyi chochote.
Rais amejitoa kurekodi makala ya Royal Tour ili kutangaza vivutio vya nchi, kuvutia watalii wengi, kuongeza mapato ya kigeni na kukuza uchumi wa nchi. Bungeni kimya, utadhani Rais hajafanya kitu.
Yanatokea hayo kipindi ambacho Bunge kwa asilimia 95 linaundwa na CCM. Samia ndiye Mwenyekiti wa CCM. Hata hivyo, wabunge hao kwa sababu hawana utii kwa chama, pia hawamtii Mwenyekiti wao.
Rais Samia mwenyewe amewahi kuwaambia wabunge “wanademka", kwa jinsi wanavyochukua maneno mitandaoni na kutaka kutengeneza ufa kati yake na Magufuli.
Ni kwa sababu wabunge wengi, kwa vile wametokana na yale ambayo Magufuli analalamikiwa kuyatekeleza kipindi akiwa Rais, hawataki aguswe. Kwao Magufuli ni malaika. Ila Samia, Mwenyekiti wa chama chao, hata akisemwa kwa uzushi ni sawa tu. Hawajali.
Kipindi cha Magufuli wabunge walikuwa tayari kusifu hadi upuuzi. Mathalan, utani dhidi ya maambukizi ya Covid-19. Kuna wabunge walipiga kelele kama mazuzu, eti Magufuli ameitokomeza Corona.
Dunia nzima watu walikuwa makini kupambana na Covid-19, Tanzania tukaleta ushirikina. Mara nyungu, tukapuuza barakoa, hatukujali misongamano. Rais Samia amesema alitofautiana na Magufuli, wanamshambulia.
Ni zuzu peke yake anayeishi gizani katika ulimwengu wa sayansi ndiye angemuunga mkono Magufuli kwa namna alivyokuwa anaipeleka nchi katikati ya janga la Covid-19.
Wabunge hao “loyal to a fault” kwa Magufuli, wanamtazama Rais Samia kwa jicho la kutoridhika kwa kila anachofanya. Hata mawaziri aliowateua ambao Magufuli aliwafungia vioo hawawataki. Wamewanunia.
Zipo taarifa kuwa kuna mipango ya wabunge kukwamisha bajeti za baadhi ya wizara sio tu kuwakomoa mawaziri wenye kijiba nao cha roho, bali pia kutuma ujumbe wa uasi wao kwa Rais Samia.
Hawafanyi hivyo kwa masilahi ya nchi. Bali kwa kijicho na chuki. Hawaitii CCM si kwa sababu chama kinaongozwa vibaya ni kwa kuwa hawataki kumkubali anayekiongoza na wasaidizi wake. Vivyo hivyo hawavutiwi na Serikali sio kwa utendaji mbaya, hawawapendi walioshika mpini. Hiyo ndio hali halisi. Wabunge wa CCM na Samia.
CreditL; uqman MALOTO