Uchaguzi 2020 Bora CHADEMA mngesitisha uzinduzi wa kampeni kufuatilia hujuma za wagombea wenu kuenguliwa

...CDM na ACT endeleeni na kampeni za uchaguzi, chakula kimeshaiva kipo tayari kwa kupakuliwa, mkisusa wenzenu watakula.
 
Mkuu haya yalifahamika mapema kwamba yatatokea , kila kanda ina timu makini sana ya wanasheria wanasimamia jambo hili kwa ukamilifu kabisa
Chadema wanajua kuwa kwa tume hii haya yatatokea na hata mapingamizi ya jana Tundu Lissu alijua kuwa Tume hii haiwezi kuona haki kwa kiwango hicho, lakini akapinga tu ili wananchi waone uovu wa tume. Hata matokeo ya mwisho wanajua yatakavyotangazwa lakini kuingia kwenye uchaguzi ilikuwa uamuzi sahihi. Swali hapa ni kuwa nini kitakachofuatia? Baada ya haya watafanya nini? Watanyamaza? Watashitaki? Au nini hatimaye?
 
Very urgently waunde TASK FORCE ya kushughulkia suala hilo wakati mengine yakiendelea. A strong TASK force
 
Umeandika vizuri sna. Busara tupu. Sasa CDM na ACT???? (sina imani nao) wakutane to deliberate on What next! Mwanahabari Huru
 
Acha upimbi wee bwege, una ushahidi gn kuwa Kuna hela zimetoka nje ya nchi?? Kwn kuzidundua kampeni ndo mwisho wa kukata rufaa Tume au hata kwenda mahakamani?? Kote ambako hatujaenguliwa kampeni zimeanza ..usiandike Kama umebanwa na tumbo la kuhara
 
Aisee, wewe unanifanya nicheke kama vile haya mambo ni mazuri na ndugu yangu Mmawia kafanyiwa ndivyo sivyo.
 
Msituletee Mambo ya kijinga hapa..kwanini msiende tume wawaeleweshe mnatuelezea elezea Nini hapa
 
Napendekeza in two or three weeks kama Tume haijawarejesha wagombea kwa kuibeba tume basi shughuli ya kudai tume huru ianzie hapo na kumuondoa magufuli rasmi kwa nguvu ya umma
 
Ni ujinga wa kiwango gani kilichowafanya Chadema na wapinzani wengine kuingia kwenye uchaguzi wakiwa na tume isiyokuwa huru? N i maajabu gani wanategemea Tume hii kuwa tofauti na ile iliyosimamia uchaguzi wa serikali za mitaa ambao ulijaa vituko mwanzo mwisho?

Kwa sie wengine tunajionea kuwa kile kinachooendelea sasa ni haki yao wapinzani wote kwani wamejali njaa zao kuliko kujenga haki ya leo na siku zijazo bila kujali chama gani kipo madarakani au kitakuwa madarakani ktk siku zijazo
 
Bro wangu Mimi ni Katibu wa Jimbo Chadema huku ninakokaa

Wakati wa kurudisha fomu, Mgombea urais mh Tundu Lisu alisema, Wagombea wasindikizwe kupeleka fomu zao

Sasa kilichofanyika huku, ni walisindikizwa madiwani wote waliokuwa wameomba kugombea Kwa upande wa Chadema, alichoniambia Bro kuwa, waliondoka vizuri wakiwa kundi la watu wengi kurudisha fomu wakiwepo na wagombea Wao wote

Lakini Hadi wanafika ofisi ndogo za tume W. Wagombea Udiwani wawili hawakuwaona, walikuja fika saa 10 jioni, sasa sijui walikwenda wapi, muulizeni Bro na kivipi waliwatoroka muulizeni Bro

Bro Anasema, hata hivyo swala Hilo walilipekeka Takukuru

Kwa hiyo, ni kweli wagombea wengi Chadema huenda njaa zimesumbua wakauza haki zao,
 
Mkuu Lissu ukiwa na akili Kama za kwako au zangu kumuelewa Lissu inahitaji muda.Unakumbuka tulivyomnanga Lissu kwa kutokuhakiki wadhamini wake kule majimboni? Mwisho wasiku inaonekana Magufuli ndo hajui sheria ya uchaguzi inasemaje pamoja na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali na wazara ya katiba na sheria kuwa chini yake.Kwa hiyo hata hili tusubilie tu tutajua maana yake muda ukifika
 
Jamani nafasi za police zikitoka naomba mnishitue.nataka nijiunge police ili nijue huko moshi ccp na vituoni kwao wanapewa nini hadi wanageuka robots?yaani nahamu sana ya kujua hili
 
Habari wanajukwaa?

Leo kwa Mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka ofisi za CHADEMA
CHAMA kinazindua na kufunagua kampaini rasmi za uchaguzi 2020.

Wakati hili zoezi la ufunguzi likiendelea
Tayari kuna wingu zito limetanda kwa wagombea wa CHADEMA wa ngazi mbalimbali kuwenguliwa .

Idadi ya walioenguliwa ni kubwa ,katika hali na MANTIKI ya kawaida usingetegemea CHAMA kiwe busy zaidi na ufunguzi wa kampeni na kuwaacha hawa wawakilishi ambao kimsingi ndio kuna uwezekano mkubwa wa Ushindi lakini hali ni tofauti.

Kwa sasa hakuna muunganiko kabisa na mtiririko wa matukio kwa mgombea wa NGAZI ya Urais na wagombea wao wa nafasi za ubunge.
Nguvu kubwa imeelekezwa kwa mgombea Urais tu kungine kumesahaulika

Kwa maoni yangu zoezi la uzinduzi wa kampeni lilipaswa lisubili na nguvu kubwa ielekezwe kwenye kuhakikisha wagombewa walioenguliwa wanapiganiwa na kurudishwa ndipo zoezi la ufunguzi lifanywe.

Kuendelea na ufunguzi wa kampeni wakati jambo hilo halijapatiwa majibu ni USALITI KWA UMMA.

Karibuni
 
Kwenye uzinduzi huo tuaelezwa hila zilizopo na kwanini CCM isichukiwe. Usimuombee upinzani wako kwenye mechi apate ajali njiani anapokuja kwenye pambano, nawe utaukosa ushindi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…