chuki
JF-Expert Member
- Mar 10, 2011
- 2,715
- 533
Taarifa iliyofikia Meza ya Habari muda huu Mbunge wa Bunda Vijijini anaemaliza muda wake amekamatwa na TAKUKURU ambao wamemkuta Mbunge huyo amekusanya Wajumbe akiwagawia Fedha Tsh. Elfu 50, kwa kila Mjumbe na akiwa amewachinjia kondoo wawili kama kitoweo.
Tukio hilo limetokea Kijiji cha Mugeta, Kata ya Mugeta ,Jimbo la Bunda (Maarufu kama Bunda Vijijini).
Pamoja na maonyo ya kila siku Toka kwa Mamlaka za Dola na Viongozi baadhi ya Watia NIA na wanaomaliza muda wao wameendelea kufanya vikao vya Siri na kugawa rushwa ya Fedha na Chakula.
Aidha taarifa zaidi zinasema Ndugu Boniphace Mwita Getere amejenga mazoea ya kutoa Fedha ili kushinda uchaguzi huku akiwa hakubaliki kwa Wananchi, Mwaka 2015 Ndugu huyo alitoa Fedha kwa wajumbe kwa udhamini wa Aliyekuwa Mgombea wa UKAWA Edward Lowasa na Mfanyabiashara Maarufu toka Musoma Mjini ambaye ana cheo cha Ubunge.
Mbunge huyo ameshindwa kutekeleza Ilani ya Chama na kushindwa kujenga Hoja jambo ambalo limekuwa chanzo cha kuchukiwa na WanaCCM pamoja na Wananchi.
Vyombo vya Dola vichukue Hatua bila Huruma kwa Wanaovunja Maadili kama hawa.