Boniface Jacob: Zijue sababu za UKAWA kukataa fedha za kuuzwa kwa UDA

Kuna dalili kuwa serikali kuu chini ya mtukufu Rais wanataka kulazimisha "nyama" haramu iwe halali kwa vile "kitoweo" kinahitajika.
Hapo ndio tutajua uthabiti wa imani kuhusu kupinga "haramu" ukoje. Jee ni wa kweli au ni maneno ya blabla?
Mkuu wameisha kula haramu mpaka wameshindwa kujua upi halali na ip ni haramu.Mwili wa mfukua makaburi tunao huku duniani, ila roho ya mfukua makaburi iko kwenye nakaburi yaliyozuhiliwa kufukuliwa. Ni muda rangi ya mkuu itaonekana
 
Chadema tokea msafishe fisadi Lowasa hamna atakayewamini tena.


Kila kitu mnataka mchakato ili kuchelewesha maendeleo ya wananchi makusudi.
Mnapinga kila kitu hadi maendeleo ya wananchi!!!
Unautaka wauze shirika nje ya sharia zinavyotaka? Baba yenu kawafundisha kukanyaga katiba na sheria naona na nyie mmeiga. Hiyo ni jatamu msile
 
Arguement kuhusu kuuzwa kwa hisa za UDA kwa wakati huu sijui kama zina mashiko tena. Kwa kauli za waziri ni kwamba asilimia 51 ya iliyokuwa UDA tayari imechukuliwa na Simon Group na fedha zimelipwa. Simoni Group kupitia kampuni yake tanzu ya UDART wanaendesha mradi wa mabasi ya mwendo kasi. Kuendelea na malumbano ya uuzwaji wa hisa za UDA ina maana sasa kila kitu kisimame pamoja na mradi wa UDART.

Ilikusonga mbele na kuepuka makosa ambayo inawezekana yalishafanyika huku nyuma ni serikali kama mwanahisa wa UDART (49%) kuhakikisha kwamba kampuni inaendeshwa kwa ufanisi na Return on Investiment inaonekana. Jiji la Dar es Salaama wawekeze hizo fedha za malipo ya hisa zake kwenye miradi kama stendi, shule, ujenzi wa barabara n.k
Kisena ni msukauma tutabariki tu huu mchezo kwa kuwa ni musukuma mwenzetu
 
Chadema tokea msafishe fisadi Lowasa hamna atakayewamini tena.


Kila kitu mnataka mchakato ili kuchelewesha maendeleo ya wananchi makusudi.
Mnapinga kila kitu hadi maendeleo ya wananchi!!!
Wewe kwa akili yako kukibali hizo hela ni maendeleo kwa wanachi,!! Shem on you!!
 
Hili ni tatizo kubwa la upinzani wa nchi yetu. Ufisadi upo katika nchi yetu na suala la UDA ni miongoni mwake. Ukawa hamuwezi huo mchakamchaka. Kuna vita mnapoteza muda tu. Hivi hao wananchi hayo ni kipaumbele? Ukawa ya sasa hivi si ya ufisadi. Pambaneni na immediate needs za wananchi. Ajira, njaa, gharama za maisha na Uhuru wa habari. Mengine, hamna uwezo wa kupaza sauti.
Pole kwa mawazo yako, ukijiona huwezi hata sababu ya kuishi huna. Pole sana mshindwa!!
 
Jukumu la upinzani ni lipi?. Hawa ndio wanatakiwa wawe na Sera mbadala bahati mbaya ni afadhali ya jana. Hivi outcome ya hilo wanalotaka watapata? Pesa zitapangiwa matumizi.
Potelea mbali zipangiwe matumizi na wanaofaidika na uuzaji huu wa shirika kubwa la UDA.
 
Chadema tokea msafishe fisadi Lowasa hamna atakayewamini tena.


Kila kitu mnataka mchakato ili kuchelewesha maendeleo ya wananchi makusudi.
Mnapinga kila kitu hadi maendeleo ya wananchi!!!
Huna lolote Lumumba boy.
Tumienia mabavu kuiba muwafukuze CDM nje ya ukumbi na mapolisi kama ilivyo kawaida yenu!!
 
Kiukweli kubariki ubadhirifu wa Mali za umma zilizogawiwa kifisadi ni jambo linalokera na litakaloendelea kuwakera wengi. Nilitarajia kuwa angemtumbua huyo mnunuzi na wote waliohusika. Kinyume chake kawaremba na kuwapulizia manukato! Najiuliza, vita yake juu ya kulinda mali za umma imeegemea upande upi?
Nauona ukabila na makandokando nengine mengi katika hili la uda pekee na bado la iptl asikokugeuzia japo uso tu apaone panavyoumiza taifa. Na hata mikataba ya madini, gesi na vitalu vya uwindaji sidhani kama yanamsumbua.
Binafsi najisikia vibaya kuendelea kuitazama sinema hii ya ufisadi isiyoonyesha kuwa na mwisho.
Sheria za manunuzi ya umma zihusike hapa kikamilifu na si kufanya mambo kwa kuwakomoa wasiofanana nawe rangi. Hakuna lingine zaidi ya kukomoana tu!
Au hakuna tofauti ya bei na taratibu za manunuzi yaani tenda kati ya zile nyumba za umma na uda? Mbona kama kunashabihiana hivi?
 
Baada ya kukataa fedha wanataka iweje?
Mchakato na taratibu za sheria za manunuzi ya umma yaonekane kufanya kazi. Yaani tenda itangazwe ili mimi na wewe kama tuna uwezo tushindane katika uwanja ulio sawa..
 
Uchambuzi mzuri na asante kwa kutuambia kuwa madiwani wa ccm bado wanataka kupiga dili juu ya dili.

Samahani unaweza kufafanua kidogo kuhusiana na hiyo bajeti ya b.34 hiyo stand ingekuwa na ukubwa gani pamoja na vitu gani. Na je katika pitia pitia yenu vitu alivyopewa simon vilistahili kuwa kiasi gani
We ni shidaaa
 
Kama tunavyomjua rais wetu hatakubali kituo hicho cha mabasi kijengwe kwa tsh bilioni 31 kama alivyokataa hospitali ya Simiyu kujengwa kwa bilioni 46. Sasa hivi hospitali ya Simiyu inajengwa kwa bilion 10 na TBA na wale wote waliosanifu ujenzi kwa bilioni 46 wameshatumbuliwa.

Hako ka stand ka mabasi hapo Mbezi katajengwa kwa bilioni 5 na TBA. Hivyo hizo bilioni 5.8 za Kisena zitatosha na chenji itabaki ya kununua mabasi 4 mapya ya mwendokasi toka China. Hao waliotaka ijengwe kwa bilioni 31 wakiwamo hao madiwani wa ukawa watatumbuliwa. Haiwezekani na wala haiingii kichwani stand ya basi ijengwe kwa bilioni 31. Huu ni ufisadi tunaoutafuta kuutumbua kila sehemu ulipo. Yaani mpaka madiwani wanapigana na wako tahari kuuana ili wasipokonywe deal hilo la 31 bilion?
 
Back
Top Bottom