Boniface Jacob: MKUU AMETUAGIZA TUKUUE

Boniface Jacob: MKUU AMETUAGIZA TUKUUE

Ee Mungu damu hizi zinazodondoka aridhini kwa amri ya tuliwapa kutuongoza, zisiende bure. Ziwafutilie wao na vizazi vyao. AMEN.
 
Nanyie viongozi wao ni wanafiki mnajitokeza wakati matukio kama haya kutafuta kiki tuu lakini wanachama wenu wanapotukana matusi makubwa kwa viongozi wa nchi tena walio kama baba zao hamjitokezi kukemea mnafurahia tuu. Huyu jamaa vyovyote kilichompata iwe alifumaniwa aliiba alionewa nk amepata funzo la mdomo wake mchafu sana ! Nadhani amerudi atakua amekua sasa maana mdomo kila mtu anao lakini kwenye matumizi duuh noma.
Tatizo hawa vijana wa chadema hawana adabu hata kidogo ndo maana hata viongozi wao wa chama wanashindwa kuwashauri kwani hata wao watatukanwa ,jitahidini kujenga nidhamu ndani ya chama hasa kwa hao watoto limbukeni,mbona Mnyika ,hayuko kama wao ?
 
Na Boniface Jacob

LEO ikiwa ni siku ya tano tangu kijana Mdude Nyagali (Mdude Chadema) atoweke katika mazingira ya kutatanisha, hatimaye tunamshukuru Mungu amepatikana. Inauma kwa sababu amepatikana akiwa ameumizwa vibaya sana.

Pamoja na yote, ipo faraja. Ni kwamba haki inakuja na itatendeka kwa waovu. Watalipa gharama ya kumteka na kumshikilia Mdude siku nne na kumuumiza vibaya. Watalipa gharama ya kuwateka Ben Saanane, Simon Kanguye, Azory Gwanda na kadhalika. Watalipa gharama ya kumpiga risasi Tundu Lissu.

Wamemuumiza Mdude. Wamemuumiza sana. Kwa kujikumbusha tu, siku nne zilizopita magari mawili aina ya Nissan Patrol na Toyota Land Cruiser, yalivamia ofisi ya Mdude, Vwawa, Songwe, wakamchukua kimabavu na kutokomea naye kusikojulikana.

Tukio la Mdude limenifanya nikumbuke simulizi fulani kipindi cha uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Mzee wetu, marehemu Reginald Mengi, kipindi hicho alikuwa kwenye malumbano na mfanyabiashara mmoja mkubwa. Wakati wa malumbano hayo, mzee Mengi alilalamika ni kwa nini Rais Kikwete hakutia neno lolote.

Mzee Mengi alisimulia hadithi ambayo naileta hapa leo ili iongeze tafakuri kipindi hiki cha matukio ya utekaji.

Alisema: "Palikuwa na Mfalme huko sehemu za mbali. Zamani kidogo, Mfalme alikuwa katika ziara ya kutembelea vijiji vyake. Akawa na msafara uliojumuisha viongozi wa chini yake pamoja na vikosi vya ulinzi wa Mfalme.

"Walipofika katika kijiji kimoja cha njiani, Mfame akaamuru msafara usimame. Viongozi wa chini yake walishangaa kuona Mfalme anamuita mzee mmoja wa makamu aliye kuwa dhaifu, fukara na mchafu sana.

Mtu yule alipomsogea jirani, Mfalme ambaye alimuuliza ''hivi wewe mzee bado upo tu'', yule mzee akajibu 'ndiyo nipo Mfalme', Mfalme akatikisa kichwa na kumuaga kwa kumwambia 'sawa niache niendelee na safari yangu nimechelewa niendako,' kisha msafara ukaendelea."

Mzee Mengi aliendelea kusimulia: "Basi Mfalme baada ya kumaliza ziara na kurudi kwake, siku kadhaa zilipita, yule mzee alivamiwa na vikosi vya ulinzi vya Mfalme na kupelekwa msituni, lakini wakiwa wanamtesa mateso makali karibu kutoa uhai wake yule mzee alipata nafasi ya kuwauliza watesi wake.

"Aliwauliza 'mbona mnanifanyia hivi, nimemkosea nani nimuombe anisamehe?' Wale vijana wa vikosi vya ulinzi wa Mfalme wakamjibu *'mkuu ametutuma Tukuue'* . Kweli wakamuua. Kikapita kitambo, Mfalme akapata habari kuwa yule mzee uliye simama kumsalimia, ameuawa na mwili wake umetupwa msituni.

"Mfalme akastaajabu sana, bila kuchukua muda Mfalme akaita wakuu wake wote wa vyombo vya ulinzi na kuamuru wampe Majibu ni nani aliye muua mzee yule. Alitaka muuaji akipatikana aadhibiwe mbele ya wananchi.

"Mkuu wa ulinzi akanyoosha mkono. Akamjibu mfalme 'Mkuu ni sisi na vikosi vyetu vya siri ndiyo vimefanya hivyo'. Mfalme akashangaa akamuuliza Mkuu wa ulinzi sababu ya kumuua mzee ni ipi. Mkuu wa Ulinzi akajibu bila kusita 'tulikusikia ukishangaa mtu yule kuendelea kuwa hai, tukajua hastahili kuishi, isije siku nyingine ukamkuta mahala pale na kusononeka tena'. Mfalme akang'aka.

"Akasema kwa ukali, 'nilishangaa mtu yule kuwa hai sababu tunafahamiana siku nyingi tangu enzi za utoto. Sikuwahi kumuona wala kujua yupo wapi, maana wazee wa umri wake wengi walishafariki dunia kwa magonjwa na sababu mbalimbali, nikaona ajabu yeye kubakia na umri mkubwa kama ule. Nilikuwa nimeshapanga nimuite nimpatie msaada ajikwamue na umasikini'.

"Wakuu wa ulinzi wakabaki vichwa chini wakose cha kufanya wala kujibu. Lakini ukweli walichofanya walikuwa sahihi sababu ilikuwa ni sehemu ya majukumu yao kusikiliza na kutii kila neno litokalo kinywani kwa Mfalme."

Imepita miaka 11 tangu mzee Mengi atoe hadithi hii, lakini bado inaleta fundisho kuwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mara zote vipo kumfurahisha kiongozi wake. Hata hivyo, si mara zote vyombo hivyo vinapokuwa vimekiuka au kwenda kinyume na taratibu zao za kazi yanakuwa maagizo ya Mfalme.

Wapo watu katika vyombo hivyo huangalia kinywa cha Mkuu na kutafsiri kila neno litokalo kwake watakavyo ili tu wamfurahishe.

Mkuu anaweza asijue nyuma kinachoendelea kwa vyombo hivyo kuwa katika kumtafutia furaha vinaumiza kiasi gani wananchi wake anaopaswa kuwalinda muda wote.

Mfano hai ni hapa kwetu katika ziara ya Rais wetu John Magufuli akiwa mkoani mbeya Wilaya ya Mbarali, mtu mmoja alizidiwa na midadi (mizuka ) na kujikuta anapiga kelele kwa kuongea hovyo wakati mheshimiwa Rais anaongea, kitendo kile kilimkwaza sana Rais ambaye aliagiza ashughulikiwe ili ajifunze.

Nikasema Mungu wangu, amekwisha!
Sababu nilijua katika mafundisho aliyokuwa anaenda kupewa huko faragha wala hatujui atapewa na polisi, jeshi au walinzi wa Rais ambao ndiyo wana jukumu la kulinda usalama na utulivu wa ziara ya Rais.

Natamani hata leo Rais apige simu aulize mtu yule yupo wapi? Walimuachia au bado? Au RPC amemuweka korokoroni kusubiri maelekezo ya kumtoa? Je kama yupo salama, Najua hakuna askari wa chini anaweza kumtoa mtu yule arudi uraiani. Maana amri ya kumpeleka huko kwenye mafundisho imetolewa na Amiri Jeshi Kkuu.

Mbaya zaidi hukohuko Mbeya baada tu ya Rais kumaliza Ziara yake ghafla ikaja taarifa mbaya ya kutoweshwa kijana na mwanasiasa chipukizi Mkoa jirani.

Kwa hadithi hii pia tunajifunza kuwa Mkuu wa Nchi kinywa chake ni tiba. Kinaweza kumponya yeyote au kikawa sumu na kumuangamiza yeyote bila yeye kujua au kwakujua.

Binafsi kupitia hadithi hii nimejifunza kuwa si kweli kwamba mara zote kutoweka kwa watu kuna baraka za Mkuu wa Nchi(Rais) au Wakuu wa Vyombo Vya ulinzi(DGIS,IGP,CDF,CGP,au CGM). Baadhi ya watu wa chini yao kwa utashi wao wanapolenga kuwafurahisha mabosi zao, hutenda ukatili bila kujua ndiyo wanawatia Doa au kuwafanya wachukiwe.

Mara nyingine yaweza kuwa ni maadui wa nje ya nchi kwa dhumuni la kutufarakanisha tusipendane sisi kwa sisi ili tupoteze Umoja wete

Basi kwa dhana hizi zote mbili zinazomtenga Rais wetu na uovu huu, tunaomba japo Rais awe anatoka hadharani kukemea au kutoa msimamo wake kama Baba Mfariji, mlezi wa Taifa na Mlinzi namba 1 wa mali na uhai wa sisi watu wake na Roho zetu zitapona

Hii itasaidia sana kuwarudisha nyuma wote wenye nia ovu wa ndani au nje ya nchi. Kama alivyokuwa akifanya Rais Kikwete hata pale vyombo vyake vya Dola vilipotuhumiwa, bado yeye kama Mfariji Mkuu alikuwa wa kwanza kufika hospitali na kutoa pole kwa wahanga kama aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Madaktari, Dk Stephen Ulimboka, mwandishi wa habari mwandamizi, Absalom Kibanda na wengine wengi wa namna hiyo.

Tunamshukuru Mungu Mdude amepatikana. Tuendelee kupaza sauti ili na wengine ambao hawajapatikana wapatikane.
Tuungane kumuomba Rais wetu atoe neno iwe salama kwetu.

BONIFACE JACOB
MSTAHIKI MEYA UBUNGO
MEI 9, 2019
Mshauri Mdudu ache kutoa lugha za kuuzi na hili liwe fundisho kwake! Ila kama ataendelea hivyo Mungu atachoka kumpigania na wala si hawa wanasiasa uchwara wakina Jacob.
 
Kwani nilikwambia nina hiyo list, ushasema ya kupika, nilikwambia utapinga tu hata ukiletewa hapo.

Ulisema zimejengwa hospitali 67, nikakuambia kutaja ni rahisi hata na idadi ya uongo. Ili udhibitishe usemacho na sio kuwa kasuku kama wengine, weka list ya hizo hospitali 67. Naona huna jipya zaidi ya kuleta porojo. Ni vyema ukakaa kimya maana huna ujualo zaidi ya kupiga propaganda mfu hapa jukwaani.
 
Tulipofikia sasahivi ni pabaya saana...kiasi kwamba kuna watu tunaogopa hata kutoa maoni yetu kwenye mitandao ya kijamii kwa maana ukikosoa tu unaonekana ni mpinzani!.. Mitandao ya kijamii ipo lkn hakuna uhuru wa kuitumia!

Pole @MdudeChadema Tunakuombea upone & urudi katika majukumu yako ya kila siku..
 
Upinzani amueni leo kumtoa Rais ktk matusi yenu mpeni heshima yake alafu tuone Kama akisema leo KESHO NATAKA WALIOMPIGA RISASI LISSU NIWAONE TUONE KAMA HAWATOPATIKANA,nENO LA RAIS NI TIBA kama umelitambua hilo basi TUMUHESHIMUNI.[/QUOTE]

Mbona aliagiza majibu kuhusu kutekwa kwa Mo mpaka leo kimya
 
Mayor Jacob ameandika kwa akili ambayo sikuitegemea!!

Neno la Askofu Mkuu Kanisa la Morovian wakati wa kadhia ya Mdude litusaidie sote. Kama raia na taifà kwa ujumla ttakuwa salama tu pale tutakapokubali kwa dhati kuwa jambo kubwa kuliko yote katika siasa hizi ni Tanzania na amani yake kushinda. Kinyume chake ni mahangaiko tupu kwa pande zote; wanaohofia kutekwa, watekaji na hata wapambe wa utekaji!
 
Upinzani amueni leo kumtoa Rais ktk matusi yenu mpeni heshima yake alafu tuone Kama akisema leo KESHO NATAKA WALIOMPIGA RISASI LISSU NIWAONE TUONE KAMA HAWATOPATIKANA,nENO LA RAIS NI TIBA kama umelitambua hilo basi TUMUHESHIMUNI.

Mbona aliagiza majibu kuhusu kutekwa kwa Mo mpaka leo kimya
[/QUOTE]

Rubbish.
 
M

Meya
Umeandika vizuri sana yoyote anayeelewa utendaji wa serikali hawezi kumuhusisha mkuu wa nchi na uuwaji au utekaji nyara raia. Kuna vikosi vinavyolinda usalama wa nchi wao wana taratibu zao wala hawapewi maagizo na mkuu wa nchi bali wanatenda

Kweli vyombo vina utaratibu wao na zinasimamiwa pia kwa maadili. Vyombo hivi vimekuwepo tangu hata ukoloni na baada ya uhuru. Hatukuona mambo haya. Raia wanayo haki kujiuliza kwanini haya yashamiri kipindi hiki? Makosa gani makubwa yamefanywa na raia hawa kustahili kutekwa, kupotezwa na kuuawa? Nadhani kosa kubwa kuliko yote katika nchi ni uhaini. Lakini utamaduni wa nchi hii ni kwamba hata wahaini wamekuwa wakipelekwa mahakamani na kuhukumiwa. Baadhi ya wahaini tunao mtaani leo baada ya kutumikia adhabu zao. Tusikatae kuwa tunalo tatizo kubwa. Wakati wa awamu ya kwanza vyombo vilipokiuka taratibu kwa kutesa na kuua viliwajibishwa. Vyombo hivi having huru kiasi cha kuua watu kwa sababu tu ya kukosoa wanasiasa!
 
Hii story yako ya mzee na mfalme haina mfanano wowote...na hawa vijana waropokaji hovyoo..
Naona hawajifunzi kwa wenzao kama lema, sugu etc...

Ukileta siasa zakichochezii nikushughulikiwa tuu..sababu ni hadui mchafu kwenye umma
Kama nimekuelewa vizuri ni kwamba Mdude (sina hakika kama nimepatia spelling za jina lake) alitekwa na kuteswa na serikali? Is that what you mean?
 
Kwanza kwa nini Anaitwa mdude katika Jamii ya kistaarabu?
watakuwa wanamtuma kumtukana rais,kweli chama kimeshindwa kumuonya mwanachama wao kuacha kutumia matusi na kejeli dhidi ya rais?!

Kwani akikosa kutumia matusi na kejeli dhidi ya rais ujumbe haufiki? Boniface angeanza kumkanya mdude kwanza maana CDM kinaonekana kama chama cha wahuni kwa kuwalea watu wa aina ya MDUDE.
 
Jamani watanzania tunapoambwa kuwa tujiunge na JKT au hata mgambo tujitokeze .
Kwanza nidhamu itakua zaidi miongoni mwetu lakini pia watu watajua namna ya kuweza kuepuka mambo haya ya kutekwa tekwa na binadamu wenzao.

Yani watu wanawindwa kama swala kila kukicha na kakikundi kadogo kabisa ka wajinga wajinga wasiojulikana na wanatekwa bila hata kuonyesha jitihada za kujua ni akina nani na wanatoka wapi na wanakaa wapi wametumwa na nani na wanapata nini kwa matendo yao hayo maovu.
Kama wanapata Mali kwa matendo hayo dawa yao ni kudili nao moja kwa moja.

Waovu wakiachwa wakafaidi ujambazi wao matendo hayo hayataosha Leo wala kesho na wengi wataumia sana.

Inawezekana ni mpango wa kuwafurahisha watu fulani.
Au kuwakomoa watu Fulani au kuwachafua watu Fulani lakini yote kwa Yote ni kwa nini wananchi wanakua kama Kondoo wa Kafara wakati wanaofanya mambo hayo ni miongoni mwa jamii?

Mdude aliwaambia mpaka viongozi wake wa Chama kuwa anatishiwa lakini walibaki kumshauri akimbie badala ya kuweka mtego wa kuwanasa Wanaomtishia na kuwatia matairi wote na vibastola vyao vitegeshwe vijulikane nani atakua anavitafuta.
Akibainika naye ale tairi shingoni mpaka kizazi hicho kiovu kinacholichafua taifa letu na kuleta hofi kitakapoisha.

Mungu aliwaambia wana wa Israel kuwa watakapoingia Kaanani wasiwaache wale watu hata mtoto mdogo mana watakapowaacha watakua kama mchanga machoni pao.
Kumwacha adui atambe ni kumpa mafanikio na ujasiri mkubwa wa kufanya anayofanya.

Tuliona wale wa kibiti walivyokua wanatamba lakini Serikali ilipoamua kuwasaka kwa UDI na uvumba Leo Kibiti ni shwari kabisa.
Labda ni kwa sababu waliokua wanauawa ni CCM lakini pia jitihada za kupaza sauti kwa Makada wao zilisaidia Jeshi la Polisi kutokomeza mauaji Yale ambayo yalikua na madhara makubwa kwa Nchi yetu kuonekana kama nchi yenye Viashiria vya Ugaidi.

Sasa wale maharamia yamehamia kwa wapinzani na wanafanikiwa sana mana Vyombo vya dola havina habari ya kufuatilia vilio vya wapinzani.

Hii ni hatari sana. Ni lazima wakubwa waone kuwa wapinzani nao ni watanzania wanaohitaji ulinzi na usalama wa maisha yao. Hawa wanaofanya mauaji na utekaji wanaweza wakawa ni wale wale waliokua wanawaua watu kule kibiti kwa lengo la kuwatia hofu watu wa ndani na nje ya nchi kuona kuwa Tanzania ni sehemu ya kuogopwa.

Serikali kupitia mawaziri wake imekua ikiwakana kabisa watekaji.
Jeshi la Polisi limekua likiwakana watekaji. Kwa hiyo kilichobaki ni wananchi wenyewe kuwasaka na kudili nao popote walipo mana ni adui wakubwa wasiojulikana.
Watafutwe na kulaaniwa na watu wote.
Ikiwezekana hata kwa maombi kwa Mungu kwa wale wenye dini na hata wale wa jadi kwa njia za kijadi wapatikane na watokomezwe kabisa mana hawajulikani kwa njia ya kawaida.

Lakini pia Wale wapinzani wanaowindwa ni vema wajipange kiitelijensia kujua kuwa nini kinaendelea na nani anawafuata fuata.

Watanzania tusikubali kujengewa hofu wakati Mh . Rais ametuambia tutembee vifua Mbele bila kujali vyama.
 
Back
Top Bottom