Boniface Jacob: MKUU AMETUAGIZA TUKUUE

Boniface Jacob: MKUU AMETUAGIZA TUKUUE

Jikusanyeni mujitoe faham, alafu ndio mtajua kwa nini kuku hakojoi.

Lete Ile list ya hospital 67, naona unarukia mambo mepesi. Nilijua tu kwa hiyo list sio rahisi ulete taarifa za kupika. Saa hii umebaki kuleta mipasho tu hapa
 
Naiona Tanzania ya Amani na Mshikamano ileeeeee inakuja. Tutaheshimiana tu. Huu mdundo unaelekea tunaweza kuucheza wote
 
Kwa hadithi hii pia tunajifunza kuwa Mkuu wa Nchi kinywa chake ni tiba. Kinaweza kumponya yeyote au kikawa sumu na kumuangamiza yeyote bila yeye kujua au kwakujua.
Ninaposoma hadithi ndefu hizi zinazowafanya wakuu wa nchi kuwa kama ma'robot' hivi ambayo yakishawekewa 'software' hayawezi kutambua lingine lolote liwalo, huwa zinanichosha sana!

Hawa wafalme wa aina hii huwa mnawaokota wapi, au ni nyinyi ndio wajenga hizo 'software' zinazowaendesha?

Boniface 'meya', hata sijui kama hiyo stori aliitoa kweli marehemu Mengi, na kama maana yake uliielewa vizuri.
 
Why mdude...afikwe na haya!? Mmejaribu kutafuta because ya swali hili....!?
===
Ninachosema ...mwenye makosa aadhibiwe hadharani. Pia katika suala hili tuwaachie wanausalama wachunguze nini kilitokea na watenda kosa wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Hata hivyo...watanzania tuache kufanya provocation....ili maadui zetu wasipate upenyo wa kutuchonganisha.
 
Ndio Siku ya kwanza nasikia upinzani uki mtaja Rais kwa heshima bila background ya kejeli,na laiti mngekua mnajua Rais anatakiwa kutritiwa tofaut na viongozi wengine..kama Hadithi isimuliavyo basi nadhani nchi yetu ingekua salama lakini nyie mmekua mkimkejeli Rais na kumtamkia maneno mabaya mabaya yasio hata vumilika,ndio mana hata yeye anashindwa tamka maneno mazuri na Walinzi wake wanazunguka nae muda wote wanamsikia hata akilalamika kuhusu vyombo vya ulinzi vinaposhindwa fanya majukumu yao,ndio mana kama hadithi isimuliavyo Hutokea mambo kama hayo.

Tukumbuke huyu ni Rais hata kama mnamkosoa tumieni lugha laini maana kwa kufanya hivyo mtaokoa wengi lakini kwa kuendelea kuropoka na kumuudhi Rais bado walinzi na vyombo vya usalama havitakubali kuskia Rais akisononeka,yatafanywa ya kwenye hadithi,jambo ambalo si zuri ktk nchi yetu.

Nina uhakika upinzani wa nchi hiii ndio source ya wasiojulikana, Mmejigawa na Rais as if mna Rais wenu mnamkumbuka Rais kwenye matatizo tu ila yakipita mnamuanzia tena jambo ambalo nafikiri Mjitafakari na ifike mahali mpambane wenyewe na mawaziri na wabunge Rais ni wa wote,kumu attack RAIS ndio mnasababisha Rais asononeke na walinzi wakimuona Mshua anasikitika lazima waFanye Yao maana vyombo vyenyewe vya usalama ndio hivyo majukumu vinafanya mpk viambiwe.

Boniphace leo umeongea vizuri,hata Rais akisoma ataona YES hapa nisaidie hiii kitu,ila siku zingine zoteee mnaongea Kejeli,mnaongea Dharau yani mnachanganya kila kitu kwenye sentensi MOJA,siku mtakayogundua UMUHIMU WA rais NCHI ITAKUA salama...wakati mwingine Rais anaona yanayotokea ila anamua kuwaaacha maana kazi yenu kulalamika uCHUNGUZI WA KIMATAIFA sijui upelelezi utoke wapi,Rais anawaangalia TU

Mnajifanya mnajua sana basi anawaacha awaone hao wachunguzi wataletwa na nani na watapitia wapi,wakati ilikua ni simple TU kuwa wapole na kumuomba RAIS ATUSAIDIE HILI JANGA LA WASIOJULIKANA ni akina nani,tatizo tunamdharau rais na kumuona hana solution mplk watu wa nnje waje ndio walete solution,wataingia nchi ipi??

Upinzani amueni leo kumtoa Rais ktk matusi yenu mpeni heshima yake alafu tuone Kama akisema leo KESHO NATAKA WALIOMPIGA RISASI LISSU NIWAONE TUONE KAMA HAWATOPATIKANA,nENO LA RAIS NI TIBA kama umelitambua hilo basi TUMUHESHIMUNI.
Wewe NYAU ebu ficha upumbavu wako.
 
Mo alimkejeli nani??
 
Kumbe! Asante sana samwel mdodo, bila shaka ushauri wako huu ukizingatiwa hata Ben Saanane anaweza kupatikana! Umeondoa utata wote kuhusu kutekwa, kuteswa na kuuwawa kwa Watanzania, kumbe tiba ipo.
 
Why mdude...afikwe na haya!? Mmejaribu kutafuta because ya swali hili....!?
===
Ninachosema ...mwenye makosa aadhibiwe hadharani. Pia katika suala hili tuwaachie wanausalama wachunguze nini kilitokea na watenda kosa wafikishwe kwenye vyombo vya sheria. Hata hivyo...watanzania tuache kufanya provocation....ili maadui zetu wasipate upenyo wa kutuchonganisha.
Ki msingi tuupinge utekaji, msifocus kwenye siasa tu. ...mo na Zakaria wali mprevoke nani hadi wakatekwa??. You are not safe I'm not safe we are all not safe. Tuupinge udhalimu huu.
 
Na Boniface Jacob

LEO ikiwa ni siku ya tano tangu kijana Mdude Nyagali (Mdude Chadema) atoweke katika mazingira ya kutatanisha, hatimaye tunamshukuru Mungu amepatikana. Inauma kwa sababu amepatikana akiwa ameumizwa vibaya sana.

Pamoja na yote, ipo faraja. Ni kwamba haki inakuja na itatendeka kwa waovu. Watalipa gharama ya kumteka na kumshikilia Mdude siku nne na kumuumiza vibaya. Watalipa gharama ya kuwateka Ben Saanane, Simon Kanguye, Azory Gwanda na kadhalika. Watalipa gharama ya kumpiga risasi Tundu Lissu.

Wamemuumiza Mdude. Wamemuumiza sana. Kwa kujikumbusha tu, siku nne zilizopita magari mawili aina ya Nissan Patrol na Toyota Land Cruiser, yalivamia ofisi ya Mdude, Vwawa, Songwe, wakamchukua kimabavu na kutokomea naye kusikojulikana.

Tukio la Mdude limenifanya nikumbuke simulizi fulani kipindi cha uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Mzee wetu, marehemu Reginald Mengi, kipindi hicho alikuwa kwenye malumbano na mfanyabiashara mmoja mkubwa. Wakati wa malumbano hayo, mzee Mengi alilalamika ni kwa nini Rais Kikwete hakutia neno lolote.

Mzee Mengi alisimulia hadithi ambayo naileta hapa leo ili iongeze tafakuri kipindi hiki cha matukio ya utekaji.

Alisema: "Palikuwa na Mfalme huko sehemu za mbali. Zamani kidogo, Mfalme alikuwa katika ziara ya kutembelea vijiji vyake. Akawa na msafara uliojumuisha viongozi wa chini yake pamoja na vikosi vya ulinzi wa Mfalme.

"Walipofika katika kijiji kimoja cha njiani, Mfame akaamuru msafara usimame. Viongozi wa chini yake walishangaa kuona Mfalme anamuita mzee mmoja wa makamu aliye kuwa dhaifu, fukara na mchafu sana.

Mtu yule alipomsogea jirani, Mfalme ambaye alimuuliza ''hivi wewe mzee bado upo tu'', yule mzee akajibu 'ndiyo nipo Mfalme', Mfalme akatikisa kichwa na kumuaga kwa kumwambia 'sawa niache niendelee na safari yangu nimechelewa niendako,' kisha msafara ukaendelea."

Mzee Mengi aliendelea kusimulia: "Basi Mfalme baada ya kumaliza ziara na kurudi kwake, siku kadhaa zilipita, yule mzee alivamiwa na vikosi vya ulinzi vya Mfalme na kupelekwa msituni, lakini wakiwa wanamtesa mateso makali karibu kutoa uhai wake yule mzee alipata nafasi ya kuwauliza watesi wake.

"Aliwauliza 'mbona mnanifanyia hivi, nimemkosea nani nimuombe anisamehe?' Wale vijana wa vikosi vya ulinzi wa Mfalme wakamjibu *'mkuu ametutuma Tukuue'* . Kweli wakamuua. Kikapita kitambo, Mfalme akapata habari kuwa yule mzee uliye simama kumsalimia, ameuawa na mwili wake umetupwa msituni.

"Mfalme akastaajabu sana, bila kuchukua muda Mfalme akaita wakuu wake wote wa vyombo vya ulinzi na kuamuru wampe Majibu ni nani aliye muua mzee yule. Alitaka muuaji akipatikana aadhibiwe mbele ya wananchi.

"Mkuu wa ulinzi akanyoosha mkono. Akamjibu mfalme 'Mkuu ni sisi na vikosi vyetu vya siri ndiyo vimefanya hivyo'. Mfalme akashangaa akamuuliza Mkuu wa ulinzi sababu ya kumuua mzee ni ipi. Mkuu wa Ulinzi akajibu bila kusita 'tulikusikia ukishangaa mtu yule kuendelea kuwa hai, tukajua hastahili kuishi, isije siku nyingine ukamkuta mahala pale na kusononeka tena'. Mfalme akang'aka.

"Akasema kwa ukali, 'nilishangaa mtu yule kuwa hai sababu tunafahamiana siku nyingi tangu enzi za utoto. Sikuwahi kumuona wala kujua yupo wapi, maana wazee wa umri wake wengi walishafariki dunia kwa magonjwa na sababu mbalimbali, nikaona ajabu yeye kubakia na umri mkubwa kama ule. Nilikuwa nimeshapanga nimuite nimpatie msaada ajikwamue na umasikini'.

"Wakuu wa ulinzi wakabaki vichwa chini wakose cha kufanya wala kujibu. Lakini ukweli walichofanya walikuwa sahihi sababu ilikuwa ni sehemu ya majukumu yao kusikiliza na kutii kila neno litokalo kinywani kwa Mfalme."

Imepita miaka 11 tangu mzee Mengi atoe hadithi hii, lakini bado inaleta fundisho kuwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mara zote vipo kumfurahisha kiongozi wake. Hata hivyo, si mara zote vyombo hivyo vinapokuwa vimekiuka au kwenda kinyume na taratibu zao za kazi yanakuwa maagizo ya Mfalme.

Wapo watu katika vyombo hivyo huangalia kinywa cha Mkuu na kutafsiri kila neno litokalo kwake watakavyo ili tu wamfurahishe.

Mkuu anaweza asijue nyuma kinachoendelea kwa vyombo hivyo kuwa katika kumtafutia furaha vinaumiza kiasi gani wananchi wake anaopaswa kuwalinda muda wote.

Mfano hai ni hapa kwetu katika ziara ya Rais wetu John Magufuli akiwa mkoani mbeya Wilaya ya Mbarali, mtu mmoja alizidiwa na midadi (mizuka ) na kujikuta anapiga kelele kwa kuongea hovyo wakati mheshimiwa Rais anaongea, kitendo kile kilimkwaza sana Rais ambaye aliagiza ashughulikiwe ili ajifunze.

Nikasema Mungu wangu, amekwisha!
Sababu nilijua katika mafundisho aliyokuwa anaenda kupewa huko faragha wala hatujui atapewa na polisi, jeshi au walinzi wa Rais ambao ndiyo wana jukumu la kulinda usalama na utulivu wa ziara ya Rais.

Natamani hata leo Rais apige simu aulize mtu yule yupo wapi? Walimuachia au bado? Au RPC amemuweka korokoroni kusubiri maelekezo ya kumtoa? Je kama yupo salama, Najua hakuna askari wa chini anaweza kumtoa mtu yule arudi uraiani. Maana amri ya kumpeleka huko kwenye mafundisho imetolewa na Amiri Jeshi Kkuu.

Mbaya zaidi hukohuko Mbeya baada tu ya Rais kumaliza Ziara yake ghafla ikaja taarifa mbaya ya kutoweshwa kijana na mwanasiasa chipukizi Mkoa jirani.

Kwa hadithi hii pia tunajifunza kuwa Mkuu wa Nchi kinywa chake ni tiba. Kinaweza kumponya yeyote au kikawa sumu na kumuangamiza yeyote bila yeye kujua au kwakujua.

Binafsi kupitia hadithi hii nimejifunza kuwa si kweli kwamba mara zote kutoweka kwa watu kuna baraka za Mkuu wa Nchi(Rais) au Wakuu wa Vyombo Vya ulinzi(DGIS,IGP,CDF,CGP,au CGM). Baadhi ya watu wa chini yao kwa utashi wao wanapolenga kuwafurahisha mabosi zao, hutenda ukatili bila kujua ndiyo wanawatia Doa au kuwafanya wachukiwe.

Mara nyingine yaweza kuwa ni maadui wa nje ya nchi kwa dhumuni la kutufarakanisha tusipendane sisi kwa sisi ili tupoteze Umoja wete

Basi kwa dhana hizi zote mbili zinazomtenga Rais wetu na uovu huu, tunaomba japo Rais awe anatoka hadharani kukemea au kutoa msimamo wake kama Baba Mfariji, mlezi wa Taifa na Mlinzi namba 1 wa mali na uhai wa sisi watu wake na Roho zetu zitapona

Hii itasaidia sana kuwarudisha nyuma wote wenye nia ovu wa ndani au nje ya nchi. Kama alivyokuwa akifanya Rais Kikwete hata pale vyombo vyake vya Dola vilipotuhumiwa, bado yeye kama Mfariji Mkuu alikuwa wa kwanza kufika hospitali na kutoa pole kwa wahanga kama aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Madaktari, Dk Stephen Ulimboka, mwandishi wa habari mwandamizi, Absalom Kibanda na wengine wengi wa namna hiyo.

Tunamshukuru Mungu Mdude amepatikana. Tuendelee kupaza sauti ili na wengine ambao hawajapatikana wapatikane.
Tuungane kumuomba Rais wetu atoe neno iwe salama kwetu.

BONIFACE JACOB
MSTAHIKI MEYA UBUNGO
MEI 9, 2019
Hekima nzito kwelikweli..
 
Nanyie viongozi wao ni wanafiki mnajitokeza wakati matukio kama haya kutafuta kiki tuu lakini wanachama wenu wanapotukana matusi makubwa kwa viongozi wa nchi tena walio kama baba zao hamjitokezi kukemea mnafurahia tuu. Huyu jamaa vyovyote kilichompata iwe alifumaniwa aliiba alionewa nk amepata funzo la mdomo wake mchafu sana ! Nadhani amerudi atakua amekua sasa maana mdomo kila mtu anao lakini kwenye matumizi duuh noma.
 
Bashite akitoka madarakani hivi vitendo havitakwepo
 
Lete Ile list ya hospital 67, naona unarukia mambo mepesi. Nilijua tu kwa hiyo list sio rahisi ulete taarifa za kupika. Saa hii umebaki kuleta mipasho tu hapa
Kwani nilikwambia nina hiyo list, ushasema ya kupika, nilikwambia utapinga tu hata ukiletewa hapo.
 
Boni kwa mara ya kwanza umeandika Point.. Umeweka siasa pembeni... Hongera
 
Muumba atusamehe, tuache kiburi cha madaraka. Malipo ni hapahapa duniani.Tuikanyage kwa adabu ardhi ya muumba.
 
Back
Top Bottom