Boniface Jacob: MKUU AMETUAGIZA TUKUUE

Boniface Jacob: MKUU AMETUAGIZA TUKUUE

Ndio Siku ya kwanza nasikia upinzani uki mtaja Rais kwa heshima bila background ya kejeli,na laiti mngekua mnajua Rais anatakiwa kutritiwa tofaut na viongozi wengine..kama Hadithi isimuliavyo basi nadhani nchi yetu ingekua salama lakini nyie mmekua mkimkejeli Rais na kumtamkia maneno mabaya mabaya yasio hata vumilika,ndio mana hata yeye anashindwa tamka maneno mazuri na Walinzi wake wanazunguka nae muda wote wanamsikia hata akilalamika kuhusu vyombo vya ulinzi vinaposhindwa fanya majukumu yao,ndio mana kama hadithi isimuliavyo Hutokea mambo kama hayo.

Tukumbuke huyu ni Rais hata kama mnamkosoa tumieni lugha laini maana kwa kufanya hivyo mtaokoa wengi lakini kwa kuendelea kuropoka na kumuudhi Rais bado walinzi na vyombo vya usalama havitakubali kuskia Rais akisononeka,yatafanywa ya kwenye hadithi,jambo ambalo si zuri ktk nchi yetu.

Nina uhakika upinzani wa nchi hiii ndio source ya wasiojulikana, Mmejigawa na Rais as if mna Rais wenu mnamkumbuka Rais kwenye matatizo tu ila yakipita mnamuanzia tena jambo ambalo nafikiri Mjitafakari na ifike mahali mpambane wenyewe na mawaziri na wabunge Rais ni wa wote,kumu attack RAIS ndio mnasababisha Rais asononeke na walinzi wakimuona Mshua anasikitika lazima waFanye Yao maana vyombo vyenyewe vya usalama ndio hivyo majukumu vinafanya mpk viambiwe.

Boniphace leo umeongea vizuri,hata Rais akisoma ataona YES hapa nisaidie hiii kitu,ila siku zingine zoteee mnaongea Kejeli,mnaongea Dharau yani mnachanganya kila kitu kwenye sentensi MOJA,siku mtakayogundua UMUHIMU WA rais NCHI ITAKUA salama...wakati mwingine Rais anaona yanayotokea ila anamua kuwaaacha maana kazi yenu kulalamika uCHUNGUZI WA KIMATAIFA sijui upelelezi utoke wapi,Rais anawaangalia TU

Mnajifanya mnajua sana basi anawaacha awaone hao wachunguzi wataletwa na nani na watapitia wapi,wakati ilikua ni simple TU kuwa wapole na kumuomba RAIS ATUSAIDIE HILI JANGA LA WASIOJULIKANA ni akina nani,tatizo tunamdharau rais na kumuona hana solution mplk watu wa nnje waje ndio walete solution,wataingia nchi ipi??

Upinzani amueni leo kumtoa Rais ktk matusi yenu mpeni heshima yake alafu tuone Kama akisema leo KESHO NATAKA WALIOMPIGA RISASI LISSU NIWAONE TUONE KAMA HAWATOPATIKANA,nENO LA RAIS NI TIBA kama umelitambua hilo basi TUMUHESHIMUNI.
Umeongea vizuri sana,wapinzani walishadharau kazi za ulinzi na usalama wa Tanzania,walisema kwa kinywa chao kwamba hawaamini upelelezi wa Tanzania.Sasa wanataka rais aongee nini wakati wao walishajitenga kitambo au hawayakumbuki maneno yao.Wanadhani rais hayaoni hayo?anaamua kunyamaza kwa kuwa wanamdharau sana,sasa amewaacha wapambane wenyewe wanamsema na siku zote wangekuwa kama alivyoandika huyu meya angekuwa rafiki sana rais maana yeye siku zote anasema yeye ni rais wa wote na sio chama.
 
Kila jambo lina mwisho wake tuwe wapole kwa sasa inakua ni kama kelele za mbu nje ya net Kuna zidi kucha kila siku hamna kinqchoendelea
 
Hili ni andiko bora kwa mwezi huu wa may 2019. Nimependa hiyo hadithi imenifikirisha mbali sana!
 
Rubbish post from Samwel Mdodo, Umeandika takataka tu unastahili kupimwa akili.
 
Wote waliopewa mamlaka na madaraka ya kulevya wakae mkao wa kula kabisa..
Ule muda muafaka unazidi kukaribia kwa kasi sana!
 
Ndio Siku ya kwanza nasikia upinzani uki mtaja Rais kwa heshima bila background ya kejeli,na laiti mngekua mnajua Rais anatakiwa kutritiwa tofaut na viongozi wengine..kama Hadithi isimuliavyo basi nadhani nchi yetu ingekua salama lakini nyie mmekua mkimkejeli Rais na kumtamkia maneno mabaya mabaya yasio hata vumilika,ndio mana hata yeye anashindwa tamka maneno mazuri na Walinzi wake wanazunguka nae muda wote wanamsikia hata akilalamika kuhusu vyombo vya ulinzi vinaposhindwa fanya majukumu yao,ndio mana kama hadithi isimuliavyo Hutokea mambo kama hayo.

Tukumbuke huyu ni Rais hata kama mnamkosoa tumieni lugha laini maana kwa kufanya hivyo mtaokoa wengi lakini kwa kuendelea kuropoka na kumuudhi Rais bado walinzi na vyombo vya usalama havitakubali kuskia Rais akisononeka,yatafanywa ya kwenye hadithi,jambo ambalo si zuri ktk nchi yetu.

Nina uhakika upinzani wa nchi hiii ndio source ya wasiojulikana, Mmejigawa na Rais as if mna Rais wenu mnamkumbuka Rais kwenye matatizo tu ila yakipita mnamuanzia tena jambo ambalo nafikiri Mjitafakari na ifike mahali mpambane wenyewe na mawaziri na wabunge Rais ni wa wote,kumu attack RAIS ndio mnasababisha Rais asononeke na walinzi wakimuona Mshua anasikitika lazima waFanye Yao maana vyombo vyenyewe vya usalama ndio hivyo majukumu vinafanya mpk viambiwe.

Boniphace leo umeongea vizuri,hata Rais akisoma ataona YES hapa nisaidie hiii kitu,ila siku zingine zoteee mnaongea Kejeli,mnaongea Dharau yani mnachanganya kila kitu kwenye sentensi MOJA,siku mtakayogundua UMUHIMU WA rais NCHI ITAKUA salama...wakati mwingine Rais anaona yanayotokea ila anamua kuwaaacha maana kazi yenu kulalamika uCHUNGUZI WA KIMATAIFA sijui upelelezi utoke wapi,Rais anawaangalia TU

Mnajifanya mnajua sana basi anawaacha awaone hao wachunguzi wataletwa na nani na watapitia wapi,wakati ilikua ni simple TU kuwa wapole na kumuomba RAIS ATUSAIDIE HILI JANGA LA WASIOJULIKANA ni akina nani,tatizo tunamdharau rais na kumuona hana solution mplk watu wa nnje waje ndio walete solution,wataingia nchi ipi??

Upinzani amueni leo kumtoa Rais ktk matusi yenu mpeni heshima yake alafu tuone Kama akisema leo KESHO NATAKA WALIOMPIGA RISASI LISSU NIWAONE TUONE KAMA HAWATOPATIKANA,nENO LA RAIS NI TIBA kama umelitambua hilo basi TUMUHESHIMUNI.
MWENYEKITI KIKOSI KAZI CHA MAUAJI NA UTEKAJI NCHINI MANAGUA CHINI YA DR. BURSHEETY
 
Ulisema zimejengwa hospitali 67, nikakuambia kutaja ni rahisi hata na idadi ya uongo. Ili udhibitishe usemacho na sio kuwa kasuku kama wengine, weka list ya hizo hospitali 67. Naona huna jipya zaidi ya kuleta porojo. Ni vyema ukakaa kimya maana huna ujualo zaidi ya kupiga propaganda mfu hapa jukwaani.
Haya haijajengwa hata moja, you must be happy now.
 
Haya haijajengwa hata moja, you must be happy now.

Suala la kujengwa hilo halina ubishi, tatizo ni idadi. Sasa ww unayejifanya unajua mpaka na idadi tuwekee list hapa. Kinyume na hapo uache kimbelembele.
 
Suala la kujengwa hilo halina ubishi, tatizo ni idadi. Sasa ww unayejifanya unajua mpaka na idadi tuwekee list hapa. Kinyume na hapo uache kimbelembele.
Serikali haijajenga kabisa, sherehekea sasa.
Kimbelembele naacha ila na wewe uache wivu, na roho mbaya kwa serikali hii inojitahidi. Idadi imetolewa na wizara ya afya na msemaji wa serikali alitweet, sio mimi, sasa kama ww unataka wabishia, sawa.
 
Ni hivi, serikali inapika data, sio wizara ya afya au msemaji wa serikali wote ni hao hao. Ingetosha kusema tu wamejenga hospitali, mambo ya idadi yanahitaji ushahidi ambao sio ww wala hao serekali wametuwekea tujiridhishe. Ni kweli serekali hii inajitahidi lakini deni la taifa nalo limepanda sana, huku miradi hiyo ikiwa hailingani na deni hilo kulingana na takwimu za makusanyo tunazolishwa.

Nina uhakika huna lolote unalojua kuhusu deni la taifa kwani unalishwa habari nusu, huku ukinyimwa uhalisia wa mambo na akili yako imeishia kwenye hicho unacholishwa bila kujiongezea.
 
Ndio Siku ya kwanza nasikia upinzani uki mtaja Rais kwa heshima bila background ya kejeli,na laiti mngekua mnajua Rais anatakiwa kutritiwa tofaut na viongozi wengine..kama Hadithi isimuliavyo basi nadhani nchi yetu ingekua salama lakini nyie mmekua mkimkejeli Rais na kumtamkia maneno mabaya mabaya yasio hata vumilika,ndio mana hata yeye anashindwa tamka maneno mazuri na Walinzi wake wanazunguka nae muda wote wanamsikia hata akilalamika kuhusu vyombo vya ulinzi vinaposhindwa fanya majukumu yao,ndio mana kama hadithi isimuliavyo Hutokea mambo kama hayo.

Tukumbuke huyu ni Rais hata kama mnamkosoa tumieni lugha laini maana kwa kufanya hivyo mtaokoa wengi lakini kwa kuendelea kuropoka na kumuudhi Rais bado walinzi na vyombo vya usalama havitakubali kuskia Rais akisononeka,yatafanywa ya kwenye hadithi,jambo ambalo si zuri ktk nchi yetu.

Nina uhakika upinzani wa nchi hiii ndio source ya wasiojulikana, Mmejigawa na Rais as if mna Rais wenu mnamkumbuka Rais kwenye matatizo tu ila yakipita mnamuanzia tena jambo ambalo nafikiri Mjitafakari na ifike mahali mpambane wenyewe na mawaziri na wabunge Rais ni wa wote,kumu attack RAIS ndio mnasababisha Rais asononeke na walinzi wakimuona Mshua anasikitika lazima waFanye Yao maana vyombo vyenyewe vya usalama ndio hivyo majukumu vinafanya mpk viambiwe.

Boniphace leo umeongea vizuri,hata Rais akisoma ataona YES hapa nisaidie hiii kitu,ila siku zingine zoteee mnaongea Kejeli,mnaongea Dharau yani mnachanganya kila kitu kwenye sentensi MOJA,siku mtakayogundua UMUHIMU WA rais NCHI ITAKUA salama...wakati mwingine Rais anaona yanayotokea ila anamua kuwaaacha maana kazi yenu kulalamika uCHUNGUZI WA KIMATAIFA sijui upelelezi utoke wapi,Rais anawaangalia TU

Mnajifanya mnajua sana basi anawaacha awaone hao wachunguzi wataletwa na nani na watapitia wapi,wakati ilikua ni simple TU kuwa wapole na kumuomba RAIS ATUSAIDIE HILI JANGA LA WASIOJULIKANA ni akina nani,tatizo tunamdharau rais na kumuona hana solution mplk watu wa nnje waje ndio walete solution,wataingia nchi ipi??

Upinzani amueni leo kumtoa Rais ktk matusi yenu mpeni heshima yake alafu tuone Kama akisema leo KESHO NATAKA WALIOMPIGA RISASI LISSU NIWAONE TUONE KAMA HAWATOPATIKANA,nENO LA RAIS NI TIBA kama umelitambua hilo basi TUMUHESHIMUNI.

Nashukuru kwa bandiko refu lenye wingi wa busara na nidhamu ya woga ndani. Ni hivi hayo wapinzani wanayotaka rais atekeleze ni wajibu wake wa urais sio hisani. Ukiona rais anataka kutekeleza wajibu wake kama hisani basi ujue hakustahili nafasi hiyo. Hapa ulichoonyesha ni kwamba rais anajua kinachoendelea lakini anakaa kimya kwasababu wapinzani hawajinyenyekezi kwake! Nilazima wapinzani wajinyenyekeze ndio wasikutane na madhila wanayokutana nayo?

Kuna watu watu wengi sana wanaojipendekeza na kijinyenyekeza kwa rais, tunadhani hao wanatosha sio lazima watu wote wawe hivyo kwani hiyo sio balance of nature na ni kutaka kujenga taifa la wanafiki na waoga. Rais sio Mungu japo kweli ana madaraka kiasi kwamba utake anyenyekewe. Anaheshimika vya kutosha, lakini usitake anyenyekewe katika kutekeleza wajibu ambao analipwa, labda kama aliingia kwenye madaraka hayo bila kujua job description yake. Kama unaonyesha wapinzani wanafanyiwa madhila ambayo yana baraka za rais ni sawa, lakini hakuna jambo lisilokuwa na mwisho. Atakaa madarakani na muda wake utaisha na mambo yatabadilika, ila yeye atahukumiwa kwa kutaka madaraka ambayo hakuwa na uwezo nayo.
 
Ngoja nimalize kufuturu kwanza, alaf niwasomee albadir watekaji wote wajitaje wenyewe kwa matukio waloyafanya wakiwa katika mikutano ya hadhara. Namuomba Mungu aniongoze vema tufanikiwe
Dini na uchawi wapi na wapi labda Ally Hapi
 
Na Boniface Jacob

View attachment 1092764

LEO ikiwa ni siku ya tano tangu kijana Mdude Nyagali (Mdude Chadema) atoweke katika mazingira ya kutatanisha, hatimaye tunamshukuru Mungu amepatikana. Inauma kwa sababu amepatikana akiwa ameumizwa vibaya sana.

Pamoja na yote, ipo faraja. Ni kwamba haki inakuja na itatendeka kwa waovu. Watalipa gharama ya kumteka na kumshikilia Mdude siku nne na kumuumiza vibaya. Watalipa gharama ya kuwateka Ben Saanane, Simon Kanguye, Azory Gwanda na kadhalika. Watalipa gharama ya kumpiga risasi Tundu Lissu.

Wamemuumiza Mdude. Wamemuumiza sana. Kwa kujikumbusha tu, siku nne zilizopita magari mawili aina ya Nissan Patrol na Toyota Land Cruiser, yalivamia ofisi ya Mdude, Vwawa, Songwe, wakamchukua kimabavu na kutokomea naye kusikojulikana.

Tukio la Mdude limenifanya nikumbuke simulizi fulani kipindi cha uongozi wa Rais Jakaya Kikwete. Mzee wetu, marehemu Reginald Mengi, kipindi hicho alikuwa kwenye malumbano na mfanyabiashara mmoja mkubwa. Wakati wa malumbano hayo, mzee Mengi alilalamika ni kwa nini Rais Kikwete hakutia neno lolote.

Mzee Mengi alisimulia hadithi ambayo naileta hapa leo ili iongeze tafakuri kipindi hiki cha matukio ya utekaji.

Alisema: "Palikuwa na Mfalme huko sehemu za mbali. Zamani kidogo, Mfalme alikuwa katika ziara ya kutembelea vijiji vyake. Akawa na msafara uliojumuisha viongozi wa chini yake pamoja na vikosi vya ulinzi wa Mfalme.

"Walipofika katika kijiji kimoja cha njiani, Mfame akaamuru msafara usimame. Viongozi wa chini yake walishangaa kuona Mfalme anamuita mzee mmoja wa makamu aliye kuwa dhaifu, fukara na mchafu sana.

Mtu yule alipomsogea jirani, Mfalme ambaye alimuuliza ''hivi wewe mzee bado upo tu'', yule mzee akajibu 'ndiyo nipo Mfalme', Mfalme akatikisa kichwa na kumuaga kwa kumwambia 'sawa niache niendelee na safari yangu nimechelewa niendako,' kisha msafara ukaendelea."

Mzee Mengi aliendelea kusimulia: "Basi Mfalme baada ya kumaliza ziara na kurudi kwake, siku kadhaa zilipita, yule mzee alivamiwa na vikosi vya ulinzi vya Mfalme na kupelekwa msituni, lakini wakiwa wanamtesa mateso makali karibu kutoa uhai wake yule mzee alipata nafasi ya kuwauliza watesi wake.

"Aliwauliza 'mbona mnanifanyia hivi, nimemkosea nani nimuombe anisamehe?' Wale vijana wa vikosi vya ulinzi wa Mfalme wakamjibu *'mkuu ametutuma Tukuue'* . Kweli wakamuua. Kikapita kitambo, Mfalme akapata habari kuwa yule mzee uliye simama kumsalimia, ameuawa na mwili wake umetupwa msituni.

"Mfalme akastaajabu sana, bila kuchukua muda Mfalme akaita wakuu wake wote wa vyombo vya ulinzi na kuamuru wampe Majibu ni nani aliye muua mzee yule. Alitaka muuaji akipatikana aadhibiwe mbele ya wananchi.

"Mkuu wa ulinzi akanyoosha mkono. Akamjibu mfalme 'Mkuu ni sisi na vikosi vyetu vya siri ndiyo vimefanya hivyo'. Mfalme akashangaa akamuuliza Mkuu wa ulinzi sababu ya kumuua mzee ni ipi. Mkuu wa Ulinzi akajibu bila kusita 'tulikusikia ukishangaa mtu yule kuendelea kuwa hai, tukajua hastahili kuishi, isije siku nyingine ukamkuta mahala pale na kusononeka tena'. Mfalme akang'aka.

"Akasema kwa ukali, 'nilishangaa mtu yule kuwa hai sababu tunafahamiana siku nyingi tangu enzi za utoto. Sikuwahi kumuona wala kujua yupo wapi, maana wazee wa umri wake wengi walishafariki dunia kwa magonjwa na sababu mbalimbali, nikaona ajabu yeye kubakia na umri mkubwa kama ule. Nilikuwa nimeshapanga nimuite nimpatie msaada ajikwamue na umasikini'.

"Wakuu wa ulinzi wakabaki vichwa chini wakose cha kufanya wala kujibu. Lakini ukweli walichofanya walikuwa sahihi sababu ilikuwa ni sehemu ya majukumu yao kusikiliza na kutii kila neno litokalo kinywani kwa Mfalme."

Imepita miaka 11 tangu mzee Mengi atoe hadithi hii, lakini bado inaleta fundisho kuwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mara zote vipo kumfurahisha kiongozi wake. Hata hivyo, si mara zote vyombo hivyo vinapokuwa vimekiuka au kwenda kinyume na taratibu zao za kazi yanakuwa maagizo ya Mfalme.

Wapo watu katika vyombo hivyo huangalia kinywa cha Mkuu na kutafsiri kila neno litokalo kwake watakavyo ili tu wamfurahishe.

Mkuu anaweza asijue nyuma kinachoendelea kwa vyombo hivyo kuwa katika kumtafutia furaha vinaumiza kiasi gani wananchi wake anaopaswa kuwalinda muda wote.

Mfano hai ni hapa kwetu katika ziara ya Rais wetu John Magufuli akiwa mkoani mbeya Wilaya ya Mbarali, mtu mmoja alizidiwa na midadi (mizuka ) na kujikuta anapiga kelele kwa kuongea hovyo wakati mheshimiwa Rais anaongea, kitendo kile kilimkwaza sana Rais ambaye aliagiza ashughulikiwe ili ajifunze.

Nikasema Mungu wangu, amekwisha!
Sababu nilijua katika mafundisho aliyokuwa anaenda kupewa huko faragha wala hatujui atapewa na polisi, jeshi au walinzi wa Rais ambao ndiyo wana jukumu la kulinda usalama na utulivu wa ziara ya Rais.

Natamani hata leo Rais apige simu aulize mtu yule yupo wapi? Walimuachia au bado? Au RPC amemuweka korokoroni kusubiri maelekezo ya kumtoa? Je kama yupo salama, Najua hakuna askari wa chini anaweza kumtoa mtu yule arudi uraiani. Maana amri ya kumpeleka huko kwenye mafundisho imetolewa na Amiri Jeshi Kkuu.

Mbaya zaidi hukohuko Mbeya baada tu ya Rais kumaliza Ziara yake ghafla ikaja taarifa mbaya ya kutoweshwa kijana na mwanasiasa chipukizi Mkoa jirani.

Kwa hadithi hii pia tunajifunza kuwa Mkuu wa Nchi kinywa chake ni tiba. Kinaweza kumponya yeyote au kikawa sumu na kumuangamiza yeyote bila yeye kujua au kwakujua.

Binafsi kupitia hadithi hii nimejifunza kuwa si kweli kwamba mara zote kutoweka kwa watu kuna baraka za Mkuu wa Nchi(Rais) au Wakuu wa Vyombo Vya ulinzi(DGIS,IGP,CDF,CGP,au CGM). Baadhi ya watu wa chini yao kwa utashi wao wanapolenga kuwafurahisha mabosi zao, hutenda ukatili bila kujua ndiyo wanawatia Doa au kuwafanya wachukiwe.

Mara nyingine yaweza kuwa ni maadui wa nje ya nchi kwa dhumuni la kutufarakanisha tusipendane sisi kwa sisi ili tupoteze Umoja wete

Basi kwa dhana hizi zote mbili zinazomtenga Rais wetu na uovu huu, tunaomba japo Rais awe anatoka hadharani kukemea au kutoa msimamo wake kama Baba Mfariji, mlezi wa Taifa na Mlinzi namba 1 wa mali na uhai wa sisi watu wake na Roho zetu zitapona

Hii itasaidia sana kuwarudisha nyuma wote wenye nia ovu wa ndani au nje ya nchi. Kama alivyokuwa akifanya Rais Kikwete hata pale vyombo vyake vya Dola vilipotuhumiwa, bado yeye kama Mfariji Mkuu alikuwa wa kwanza kufika hospitali na kutoa pole kwa wahanga kama aliyekuwa kiongozi wa Chama cha Madaktari, Dk Stephen Ulimboka, mwandishi wa habari mwandamizi, Absalom Kibanda na wengine wengi wa namna hiyo.

Tunamshukuru Mungu Mdude amepatikana. Tuendelee kupaza sauti ili na wengine ambao hawajapatikana wapatikane.
Tuungane kumuomba Rais wetu atoe neno iwe salama kwetu.

BONIFACE JACOB
MSTAHIKI MEYA UBUNGO
MEI 9, 2019
Huyo anaye mpangusa damu mbona hajavaa kinga mikononi? Anaweza akajiambukiza/akamuambukiza magonjwa? Awe makini!
 
Huu utawala ni wa laana, tutalia na kusaga meno.
 
Back
Top Bottom