Bongo ukiwa na PhD lazima uchukiwe

Wabongo wanataka mwenye PhD awe na mawazo kama yake wa darasa la saba.

Yaani wanataka wafanane mawazo, bila hivyo mara ni msaliti, mara PhD fake au elimu haija msaidia.

Mtu unalazimisha wa PhD awe na mtazamo kama wako wa darasa la 7.
Baadhi ya KIWADU ndo hawa kutwa kupost picha safarini mgombani na kuonyesha nyama choma mtandaoni. Inferiority!
 
PhD holder akichumia tumbo kuna shida gani? Mnataka mje kumcheka baadae?
 
Hakuna anaechukiwa Bali lazima ulinganishe kuwa PHD na Yale anayofanya yanalingana ???????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mi naamini kuwa mtu mwenye PhD anauwezo mkubwa kwa kuchambua mambo, kulingana na elimu yake inapaswa awe ni mtu wa kuleta zaidi majawabu yenye tija na ndio maana mnapokuwa kwenye mikutano/ mikusanyiko na wakishajua kuwa wapo watu wa level hiyo ya elimu huwa wanapewa attention ya kiwango kinachostahili kwa sababu inaaminika wanaweza kuleta mchango chanya. Lakini kama unayohiyo PhD halafu hoja zako haziakisi elimu yako ndipo hapo watu wanakuwa na mashaka na wewe.

Niliwahi kwenda nchi mmoja kwenye mafunzo ya muda mfupi (wiki mbili), wawezeshaji walikuwa vizuri sana kwenye uwasilishaji wa mada na hata nje ya mafunzo hayo katika uzungumzaji wao unakuwa na shauku ya kujua huyu mtu ana elimu gani.
Katika kuwafatilia nikagundua wote walikuwa ni PhD holders, lakini haukuna mahali walijitambulisha kwamba mimi ni Dr......, nilifanya kazi ya ku-google majina yao ndo nikapata salutation zao. Nikapata cha kujifunza kwamba tekeleza wajibu wako kwa kiwango chako halafu waache watu wawe na shauku ya kukufahamu wewe ni nani, sio kujikweza mimi nina PhD (" ndo unasikia watu wanasema eti naye Dr.)

Mwisho, PhD ni elimu kubwa sana, tuitendee haki inayostahili.
 
Nilipataga scholarship ya kusoma PhD sasa kuna mzee mmoja Professor nikaenda kumweleza hiyo habari na kumtaka ushauri. Alichoniambia ni kwamba kwa nafasi uliyonayo ambayo hata PhD holders wanaitamani usipoteze muda kwenda kusoma Zaidi, elimu uliyonayo inakutosha usiende kujaza maelimu halafu ukakutana na matarajio tofauti ukawa frustrated. Nilichukua ushauri wake sikwenda na sijutii .

Wengi wa PhD holders walitegemea kupata matokeo makubwa kimadaraka na kifedha na baada ya kukutana na utofauti wanaishia kudata tu. Kuna mmoja aliingia kujenga fensi mpk ndani ya eneo langu sehemu Fulani nilikuwa nimepanunua nimepaacha. Siku niliyoenda akaniletea nyodo wakati mpk huko kwenye hati halali kabisa. Nilichukua Tingatinga nikabomoa mchana kweupe baada ya kujiridhisha kuwa kavamia. Jamaa alipaniki kaenda polisi mie nikaenda kwa wakili wangu na watu wa Ardhi. Kufika pale anasema unajua mie ni Dokta, nikamwambie kajambe ukanye, kama ungekuwa na akili usingeshindwa kusoma Ramani ya kiwanja
Tulimshtaki na alitulipa Fidia
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very true,ukiangalia wasomi wa nje wenye phd hutafuta matatizo ya jamii na kuyasolve wakati huku wanatumia hizo phd kuwatishia watu.
Nitawaona wa maana sasa hivi wakiingia maabara na kutuletea dawa ya corona.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…