Infopaedia
JF-Expert Member
- Oct 28, 2011
- 1,231
- 1,495
Kuna jamaa kasomea majanga ya theluji na ana phd. Huyu nae hapa Bongo anatamba kwamba ni phd holder na anadai aheshimiwe. Ukiwa na impact chanya kwenye jamii yako, wala huwezi ku-demand heshima. Itakuja yenyewe tu. Tatizo wenye phd hudhani watu wana bother na hizo karatasi zao. Watu wana bother na impact yako kwenye jamii.
Sekondari tulisoma hadithi ya kijana aliyechangiwa pesa na jamii yake akasome sheria ili aje kuitetea jamii yake, alipofika kule akasomea lugha na kurudi akiwa na suti kali na mabombastic ya kutosha. Sijui kama mnapata connection ya hiyo hadithi na hizi phd za hawa jamaa!!!. Then wanataka status flani amazing kwenye jamii. Haiko sawa kabisa. Halafu matatizo ya Tanzania na Afrika kwa ujumla, wala hayahitaji phd kuyatatua. Wazungu huko kwao waliyatatua haya matatizo kwa kutumia akili za la saba B. Then yakaja matatizo mengine yaliyohitaji akili za sekondari, wakatumia akili za sekondari kuyatatua. Yakaja matatizo ya digirii, wakatumia digirii zao kuyatatua. Yakaja ya masters na ma-phd na mpaka hivi sasa wana wanayakabili matatizo kabla hayajatokea wala hatujui wanatumia akili gani.
Sasa hapa kwetu kila mwaka linajirudia tatizo hilohilo na linauwa watu, halafu mtaniambia tunahitaji phd kweli!!!!!.
Pale Mbeya ukitoka mjini kuingia Mbalizi barabara ina mteremko mkali na zinatokes ajali za kizembe sana. Basi akatokea mtaalamu akatoa muongozo, juu ya mteremko na chini ya mteremko kuwe na askari wa barabarani wanawasiliana, wanaruhusu magari yashuke kwa zamu. Ndicho kinachoendelea mpaka sasa. Ndio elimu ya vyeti na phd zilipotufikisha. Dah!!