Bongo taxi

BIN BOR

JF-Expert Member
Nov 23, 2010
1,013
407
Hii si utani...imetokea leo nilipochukua taxi toka Magomeni, nikasimama pale Turiani schoo kisha nikaunganisha hadi Shopers plaza.

Mimi : Bei gani hadi hapa?
Driver : Elfu kumi na tano
Mimi: Umepataje jumla hiyo.
Driver : Kutoka Magomeni hadi Turiani School ni elfu tatu, halafu kutoka school hadi hapa ni elfu saba.
Mimi: Sasa inakuwaje elfu kumi na tano?
Driver: Teh, teh, teh, nipe tu hiyohiyo
Mimi: Hiyo hiyo ngapi?
Driver: We nipe tu uliyokuwa nayo blaza.......

Aisee kidogo nimnase kibao
 
Hahaha sasa we ulitaka akwambie kahesabu km.??Embu mlipe mwenzio ameshajichokea kwa jua alafu unamzingua kwa maswali!
 
Ungemwambia mbona we unaenda kwa 350/= ye elfu kumi na tano imetoka wapi... Halafu ukampa jero.......
 
Ha ha ha! Umenikumbusha kuna mtu alitolewa stand ya mkoa ubungo hadi udsm kwa elf 30. Madereva tax jamani!
 
duuuhh pole sana
si borea ungetembea tu hiyo hela ukanywe safari baridi au soda ya tangawizi ka hutumii pombe,,
 
Back
Top Bottom