Bongo Star Search 2008 Inasikitisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bongo Star Search 2008 Inasikitisha

Discussion in 'Entertainment' started by Mkombozi, Mar 31, 2008.

 1. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #1
  Mar 31, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ndugu wana JF na hasa pia wale waliokua wakifuatilia mashindano ya Kumtafuta mkali wa bong flavour, yaan Bongo Star Search. Nawapongeza BenchMark kwa kuinua vipaji vya wanamuziki. Mpaka sasa wameshafanya mashindano kwa miaka miwili.

  Lakini mashindano ya mwaka huu na wengi mnaweza kukubali hiyo, hayakua huru na haki kabisa. Yaani hayana tofauti na uchaguzi uliofanyika Kenya Mwaka jana mwishoni. Katika mashindaono haya, walikua wanahimiza sana mashabiki kupiga kura kwa mshiriki waliyekua wanayehisi anafaa kuwepo na mwenye kura ndogo hutolewa. Mwaka huu haijulikani washindi walipata kura ngapi, hata mshindi wa mwaka huu hawakuonesha aliwashinda wenzake kwa kura ngapi za mashabiki. Panapokua na kupiga kura halafu kura hazitaji & na haijulikani ni ngapi lakini mshindi anapatikana basi sichelewi kusema mshindi alipangwa. Kwa nini katika kila stage kura hazikuwekwa hadharani? Labda wana JF mnaweza kunisaidia hapo kama hili ni sahihi kura kupigwa, mshindi kutangazwa bila kuonesha amepata kura ngapi!!!!!!!!!!! Inasikitisha kwa kweli, uizi wa kura haupo kwenye uchaguzi wa kisiasa tu, hata kuku kwenye mashindano, kwa nini kuwe na uficho wa kura kwa mashabiki? Huu pia unaweza kua ufisadi wa kura. Nisaidieni hapo. Tukiendelea hivi mashindano haya yatapoteza mashabiki, tunapopiga kura ndiko wanakopata pesa za kuzawadia washindi na faida juu, sasa wanaanza kuleta utani. Inasikitisha sana
   
 2. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #2
  Mar 31, 2008
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Poleni sana wasanii. Ninapoangia hayo mashindano ,na hasa wale majaji nashindwa kuelewa kuwa ndio hivyo inavyokuwa au ni upupu wao. Kwanza hao mashabiki watapiga je kura kwa haki iwapo jaji anacritisize 100%? hao ndio niliwaona watupu wa kwanza .Wanajionyesha wanafahamu muziki kumbe wapi.

  Binafsi sipendi tabia ya ku critisize na kuponda namna wale wanavyofanya. Kwa nini wasitumie lugha ya kiustaarabu zaidi? Hata kama mshiriki hajavutia ,basi sema ..leo umependeza ,ila next time tafadhali jitahidi zaidi....utawasikia wakisema ..kama sio huo mpasuo huna kitu..huna kitu kabisa...

  Mimi naowaona ni kundi tu la wahuni wakiongongozwa na akina Kitine wanajitafutia umaarufu na fedha kupitia kwenu basi. Waambieni ukweli , Je mlikuwa mnalipwa chochote kama alowance?
   
 3. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #3
  Mar 31, 2008
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Nadhani mdau huyu toka kule Michuzi amesema nilichotaka kusema... naomba nimnukuu....

  Kweli, aliyesema kwamba hatukuwa tunatangaziwa washiriki walikuwa wanapata kura ngapi, kila wiki, ametoa mwanga... shindano halikuwa huru na haki, wadhamini wameona, na huu ndio mwaka wake wa mwisho.

  Incidentally, nimesikia kwamba Madam Rita ameweka ka-monopoly fulani kule BASATA, kwamba, yeyote atakayekuja na shindano lenye muelekeo wa ki-star-search, basi, asipewe usajili. Yaani, anataka liwepo shindano moja tu. Je, hii inawezekana? Swali langu zaidi ni, je, ni lazima mashindano yote ya kisanii yasajiliwe BASATA? Kwani what is the meaning of a free market economy? Mbona tunaweka monopolies ndani ya free market economy? What's the point?

  ./MwanaWaHaki
   
 4. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  naona huu ni aina nyingine ya usanii. haiwezekani kweli kura zipigwe halafu mshindi atangazwe bila kujulikana idadi ya kura zilizomfanya ashinde. tena ukiangalia, yule ambaye majaji walikuwa wanamshabikia ndiye huyo aliyeshinda bila idadi ya kura zake kujulikana. sasa sijui huyo mshindi ametokana na kura za watazamaji au majaji????!!!???
   
 5. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  please anyone know Bongo star search website
   
 6. pascal

  pascal Member

  #6
  Mar 31, 2008
  Joined: Oct 12, 2007
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  http://www.bongostars.com/

  Ni kweli kabisa. Binafsi sikufurahishwa kabisa na mtiririko mzima wa shindano hilo lililojipatia umaarufu mkubwa sana hapa Tanzania. Ila ningependa kutoa wito kwa waandaaji waweze kuwa na free and fare mode of getting the winner. As the matter of fact haiingi akilini kuona jinsi majaji wanavyo criticize hao contestant. Natoa wito kwao waangalie Tusker project fame jinsi mashindano yanavyofanywa afu nao waige mfano wa mambo mazuri kutoka hapo.
  Kwa wanaohitaji website ya bongo star search ndo kama hiyo hapo juu.....
  http://www.bongostars.com/
  Ni hayo tu kwa leo.
   
 7. DMussa

  DMussa JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 1,301
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Nina uhakika haya mashindano kwa mwaka ujao yatakosa washabiki kwa sababu hizohizo....
  Hakuna haja ya kupiga kura kama kura zenyewe hazihesabiwi!!! Nina wasiwasi sana na uadilifu wa waandaaji wa mashindano haya.. yawezekana aliyeshinda mwaka jana majaji hawakupendezwa nae kwa hiyo wakaona kura wazihesabu kwenye background ili waweze kuzimaneuever!!!!
  Yangu macho lakini haikuwa transparent competition hata kidogo!!
   
 8. Manda

  Manda JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2008
  Joined: Sep 24, 2007
  Messages: 2,075
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nilidhani kuwa ni mimi peke yangu who i was dissappointed na zile results, na i was thinking nikija humu JF leo nianzishe thread ya kuhusu BSS.
  Yep, kama tulio wengi i think benchmark inabidi wabadilishe baadhi ya mambo ktk mchakato wa kumsaka mshindi, binafsi naona kuna umhimu mkubwa wa kuwa wanatangaza kura za washiriki kuwa wamepata ngapi kabla ya kuwaengua, au wanaogopa TUTAWAPIGIA HESABU WANACHUMA SH. NGAPI?
  Manake bila hivyo wana weza kuwa wana-alter matokeo sisi bila kuja, mfano kama siku ya fainali, dont tell me kuwa kura ambazo zilikuwa zinapigwa the SAME time fainali inaendelea zilihesabiwa pia katika kuamua nani mshindi!
  Nani mkali, kati ya MWIMBAJI[ misoji] na MWANAMZIKI[rogers]?...(Ni mtizamo tu washkaji msijenge chuki-Afande Sele)
   
 9. M

  Mtu Kwao JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2008
  Joined: Jan 15, 2008
  Messages: 258
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  MKALI MWANAMUZIKI ROGERS BWANA .MI Sitaki kuamini alishindwa na watu niliokuwa nao walisema wangeamini tu kama kura zingeonyeshwa kama mwaka jana.Nahili rita alilijua ndio maana akficha mana mwaka jana walimtaka leah mudy ikasindikana wakaona dawa ni kutotangaza kura mwaka huu.WAO KWAO MSHINDI NI misoji kwetu sisi ni rogers na tunamtaka arecord nyimbo zake soon tuweze kumwonyesha rita na akina master j mshindi ni nani..Kwa ushairi hatuwezi kumchangia huyu kijana arecord albam soon? ni mtazamo wangu tu wana jf
   
 10. M

  Mkombozi JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 626
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Ni wazi kwamba kulikua na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na uteuzi wa mshindi. Kuna kila harufu ya ufisadi na udanganyifu kwa kila stage ya mashindano haya. Mshindi anatangazwa wakati kura zinaendelea kupigwa bado, pia kutotangaza kura ni kupanga matokeo. Hii inafanana kidogo ya uchaguzi wa nchi jirani. Cha msingi baraza la sanaa pia linapaswa kuwajibika kwa kushindwa kusimamia vizuri uendeshaji wa mashindano haya. Baraza likijiuzulu sio vibaya sana kwa kushindwa kazi.Ieleweke pia hii ni biashara, kura tunazopiga tunakatwa hela,matangazo ya biashara na viingilio mlangoni ni mamilioni ya hela, ndio hizo hizo hutumia kuwalipa allowance,na washindi. Leo hii napiga kura na ninakatwa hela halafu wanaleta utani, pia Benchmark iwajibike kwa kua na baadi ya Majaji wenye wiwango vya chini, wangekua ni viwango vya wastani au juu wangeyaona haya yote. Pia wangeacha kuangalia eti mwele zako nimezimind, mpasua uko safi,Mmwaa weekend,sauti lako bovu haliyanifikisha n.k. Tuamke

  Soma Hii Kutoka Global Publishers

  Shindano lenye umaarufu mkubwa hivi sasa nchini la kumtafuta msanii chipukizi mwenye kipaji cha muziki, Bongo Star Search (BSS), limeingia lawamani kwa kuonesha kumjua mshindi mapema, katika fainali zilizovuta hisia za wengi zilizofanyika kwenye Hoteli ya Blue Pearl, iliyopo ndani ya jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam, Ijumaa iliyopita.Licha ya lawama hiyo, lakini wananchi wengi bado wanaliunga mkono na kulikubali shindano hili, hasa pale lilipompa taji mwaka jana Mtoto wa Bagamoyo, Jumanne Idd katika fainali zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.
  Ikumbukwe kuwa ni ufanisi uliooneshwa na waratibu wa shindano hilo ambalo lipo chini ya Kampuni ya Benchmark Production mwaka jana, ndiyo uliolijengea heshima na kuwafanya watu wengi kulifuatilia na kutumia muda wa hewani wa simu zao kwa kutuma sms kuchagua washindi.

  Lawama zinazotolewa kwa fainali za safari hii, ni kauli zilizokuwa zikitolewa na majaji wakati washiriki walipomaliza zamu zao za kuimba, ambapo ilionekana majaji tayari walikuwa wanamjua mshindi atakuwa nani katika fainali za mwaka huu, licha ya ukweli kwamba kura zilikuwa zikiendelea kupigwa.

  KAULI ZA MAJAJI ZILIKUWA HIVI!
  Alipomaliza kutupa kete yake ya pili, mshiriki nambari 03, Rogers Lucas, jaji ambaye ni mwanamuziki mkongwe John Kitime, alimuambia kuwa baada ya BSS, asiache muziki. Ukiiangalia sentensi hiyo na kuichambua neno kwa neno, utagundua kuwa Kitime alikuwa na matokeo yanayoonesha kwamba Rogers si mshindi.

  Kauli ya Jaji Mkuu, Madam Rita, nayo inathibitisha haya! Mara baada ya Rogers kumaliza kuimba, alimuambia kuwa laiti BSS ingekuwa inapata washindi wawili, naye angekuwemo. Sentensi hiyo nayo ilikuwa inaweka wazi kuwa mshindi alikuwepo ambaye wao walishamjua mapema.

  Aidha, kauli za majaji Salama Jabir na Joachim Kimario ‘Master Jay’ walipokuwa wanawaponda washiriki Yohana Simon na Maangaza Nyange, kuwa waliimba chini ya kiwango, ni wazi ziliashiria kuwa mshindi wa kwanza mpaka wa tano, walikuwa wanamjua.

  WATANZANIA KUHIMIZWA KUPIGWA KURA
  Matokeo yalijulikana kabla ya kuingia Blue Pearl, lakini bado Watanzania walikuwa wakihimizwa kupiga kura ili kuchagua washindi. Kwa utaratibu huu, majaji hawakupaswa kuonesha wanamjua mshindi wakati kura zikiendelea kupigwa, kwani kitu chochote kingeweza kutokea na kubadilisha matokeo ya awali.

  MAJAJI
  Majaji Salama Jabir na Master Jay wanapaswa kujirekebisha na kuacha tabia zao za ‘kukandia’ katika shindano lenye hadhi kubwa sasa kama BSS. Madam Rita anatakiwa kuliangalia sauala hili mapema na ikiwezekana, mwaka ujao awapige chini na kuwachukua watu wenye heshima zao ambao watakidhi hadhi ya shindano.

  Jaji msema hovyo wa nini? Anayeponda badala ya kutoa ushauri ni kwanini aendelee kuwepo? Alitumia busara gani Master Jay kwa kumuambia Maangaza kuwa zaidi ya mpasuo wa nguo yake, hana anachoweza katika muziki. Hii ni kauli ya kimuziki au ‘kukandia’?

  Walishamjua mshindi mapema, ilikuaje wamponde Yohana mpaka kumkatisha tamaa, wakati mashabiki walikuwa wakimshangilia kwa nguvu? Madam Rita anatakiwa kutafuta majaji wanaoweza kutoa ushauri hata kisaikolojia, na siyo kukatisha tamaa. Wanaokosoa kwa kujenga na si wapondaji.

  UKUMBI
  Kamati ya maandalizi haikufikiria kwa makini kuhusu ukumbi muafaka wa shughuli kubwa kama ile. Ukumbi wa Blue Pearl ni mdogo na una joto jingi kiasi kwamba mashabiki walioingia walii shia kupata mateso badala ya kuburudika. Idadi ya watu waliobaki nje huku wakiwa na tiketi zao mkononi, ilikaribiana na ile ya waliokuwemo ndani, kwahiyo kuna watu waliolipa hela bila kuona shoo.

  JUKWAA
  Katika kipengele hiki, waandaaji wanastahili pongezi kwakuwa lilitengenezwa kimataifa na kumuwezesha kila mtu aliyepata nafasi ya kuingia ndani, kuona shoo bila matatizo.

  SAFARI NDEFU
  Madam Rita anastahili pia pongezi kwa kuianzisha BSS na kuifikisha hapa ilipo. Amewafungulia milango vijana wenye vipaji na kuweza kujipatia ajira. Mwaka jana alionesha mfano, mwaka huu pia amejitahidi, ukichanganya na kuwaleta wasanii ndugu kutoka Jamaica, Naila na Nyanda Thorbourne a.k.a Brick & Lace, ni safari ndefu kweli.

  JUMANNE IDD NA MISOJI NKWABI NI NDUGU
  Wanatoka kijiji kimoja ndani ya Wilaya ya Bagamoyo, Pwani. Na baada ya Misoji kutangazwa mshindi, Jumanne ‘alitusapraizi’ kuwa ‘mdada’ huyo ni ndugu yake kwasababu wanatoka kata na kijiji kimoja pia huwa wanaitana kaka na dada
   
 11. J

  Jafar JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2008
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mimi nadhani nia ilikuwa ni kukuza vipaji na sio kipaji kimoja. Kama hivyo ndivyo basi wale wote walioingia top 10 walikuwa washindi tayari. Maana wanaweza kutoka pia na kumshinda mshindi katika soko. Ukiondoa hiyo kasoro ya kutotangaza idadi ya kura mara baada ya mshindi kutangazwa, product ya mwaka huu ilikuwa nzuri, well organised and more sponsored than last year.

  Kuna yule jamaa amesema eti wajifunze Tusker Fame, mweeeee kule ndio uozo kabisa, kura hazitangazwi, ukabila, lile shindano kila mwaka (hata miaka kumi mbele, kama walivyokuwa vatikani zamani) mshindi atatoka Kenya.

  Good start Madame Rita but continously improvement is what is required.
   
 12. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2008
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ingekuwa vipi wakawagroup Contestants gospel,reggae,hiphop,bongo flava,soul na taarab(maangaza)
  [​IMG]
   
 13. J

  Jafar JF-Expert Member

  #13
  Mar 31, 2008
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Mar 31, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  tena imefika wakati sasa waandaaji wa shindano hili wakaweka wazi vigezo ambavyo vinatumika kumpata mshindi, kwa sababu watu wanaopiga kura hivi sasa wanafanya hivyo bila kujua wanachopaswa kuangalia kwa msanii ni kitu gani. si ajabu mtu kama Jumanne Iddi alishinda kutokana na kuchezacheza bila mpango katika steji lakini si mtu wa kipaji cha mjuziki. kwa muda ambao amekuwepo katika game amethibitsha kuwa alikuwa muigizaji zaidi kuliko msanii
   
 15. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #15
  Mar 31, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,320
  Likes Received: 5,611
  Trophy Points: 280
  sio kweli kabisa kuwa jumanne iddy na misoji wanatoka kijiji kimoja bagamoyo sio kweli mimi namjua sana huyu misoji...anakaa karibu sana an stand ya bagamoyo..ambayo ni mpya...karibu sana pia na barabara kwenda dar...na huyo jumemnne iddy hajulikani bagamoyo mjini anakaa km 40 kuelekea msata...vijijini sana ...ila pale mjini hajulikani kabisaaaaaaaa
   
 16. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #16
  Mar 31, 2008
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
 17. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #17
  Mar 31, 2008
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,500
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mshindi wa BSS mwaka huu nimemjua leo hii kupitia JF kwa sababu nilishaacha kuangalia mashindano hayo kwenye TV siku nyingi. Kuna siku tulikuwa tunaangalia shindano hili nyumbani, Binti yangu mdogo wa miaka 9 alipendezwa na jamaa mmoja aliyeingia kwenye stage. Lakini kashfa na maneno ya kejeli yaliyotoka kwa majaji, yalimshtua maana aliniuliza maswali ambayo sikuwa na majibu nayo. Kwa bahati mbaya hata comment niliyotuma kwa sms kwa namba iliyokuwa naonekana kwenye screen, haikujibiwa. Huo ndio ulikuwa mwisho wangu wa kuangalia BSS. Hawa majaji wanajifanya wanajua sana, lakini sisi tuliowapokea mara ya kwanza mwaka juzi pale Giraffe Ocean view hotel, tunajua wote walivyokuwa washamba; leo wamesahau kule walikotoka na hawataki wenzao nao waibuke. For sure, mashindano ya BSS yanazidi kupoteza ummarufu.
  LENGO LA SHINDANO NI ZURI - MAJAJI MJIREKEBISHE NA HASA KAULI ZENU
   
 18. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #18
  Mar 31, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mi wamenichekesha tu walivyowaleta "Brick and Lace" na kuwa tout kama ma supersta fulani hivi wakati huko JamDown hawa ni kama hao wanaoshindana tu, labda wamewapita kidogo tu.

  I guess as long as they look cute and are from Jamaica its all good, wakaenda kuwatafuta the cheapest artist ambao hata albamu hawana na wametemwa kwenye label yao na hawana hata wimbo mmoja kwenye charts zenye akili.

  Kama wamefanya hivyo kwa kikundi walichokileta kutoka Jamaica sitashangaa wakifanya madudu nyumbani.
   
 19. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #19
  Mar 31, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135

  Pole sana wewe na bintiyo,

  Hiyo inaitwa Simon Crowell Syndrome, jaji hawezi kuwa mzuri mpaka awe demeaning na sarcastic.Copycats wa American Idol katika culture ambayo sarcasm is not understood and more importantly frowned upon.

  Monkey see, monkey do!
   
 20. a.9784

  a.9784 Senior Member

  #20
  Mar 31, 2008
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bench Mark mmeoza,kwa nini mmewadanganya wananchi kupiga kura kwa washiriki wanaowataka halafu msitoe matokeo kwa wapiga kura,huu ni wizi wa waziwazi mnatakiwa kufikishwa mahakani.

  Halafu katika watu zaidi ya milioni 39,mlikua na kigezo gani cha kuwatumia majaji walewale tena wasikua wastaarabu hata kidogo.Unapomwita Salama Jabir kuwa jaji,hivi unabomoa au unajenga?Huyu ni mtu wa kukashifu wasanii wanaochipukia.Hivi salama ungeku mzuri sijui ingekuaje jamani.Mtu akikosea ni kumsahihisha na sio kumponda kama majaji wa bss.Yaani hawa majaji utazani wanatoka Ulaya.

  Tabia ya kupanga matokeo mapema,BSS mtakua mmetoka nje ya mstari,badala ya kusaka vipaji,mtakua mnapoteza vipaji.

  Kwa hili Rita umeluz mtu wangu
   
Loading...