tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,066
- 27,441
Leo nilikuwa naangalia filamu ya Bongo Movie, kupitia king'amuzi cha Azam Tv, nikakutana na maneno ya kiingereza cha ajabu kilichotumiwa katika tafsiri (subtitles), lengo likiwa kutoa tafsri kwa watazamaji wasiojua kiswahili.
Kuna 'subtitle' ilikuwa inasomeka 'I see tones of blood in your face...what is happen for you?'. Nilipata wakati mgumu kutatafuta tafsri ya hii sentensi. Lakini kwa kuwa mhusika aliyekuwa akiulizwa swali hilo alikuwa na matone ya damu usoni kwake nikakisia kwamba mtafsiri alikuwa na maana ya: 'Naona matone ya damu usoni kwako...nini kimekutokea?'
Subtitle nyingine ni ile iliyokuwa imasomeka: 'Keep quite' ikiwa na maana ya 'Nyamaza'.
Nashindwa kuelewa hawa watengeneza filamu huwatumia watu gani kutafsiri filamu zao. Watakuwa wanamchukua JB, King'wendu au Mrisho Mpoto na kuwapa kazi ya kutafsiri filamu wakati hawajui kiingereza.
Ikiwa wasanii wetu wataendelea kutengeneza filamu za ovyo kama hizi kamwe wasitegemee kazi zao kupata soko la kimataifa. Waendelee tu kuibiwa na wahindi.
:yield: